DIWANI MWASHITETE AYATAJA MABILIONI YA RAIS DKT,SAMIA YALIVYOING’ARISHA KATA YAKE
MAKALA ‘’Wanaomsema vibaya Rais Dkt,Samia wakapimwe akili,amegusa kila sekta kujenga miradi,imeturahisishia kupunguza hoja kwa wananchi wakati wa kuomba kura’’. Na Ibrahim Yassin,Songwe DIWANI wa kata ya Harungu wilayani Mbozi mkoani Songwe Maarifa Mwashitete,amemsifu Rais Dkt,Samia Suluhu kwa kujenga miradi iliyogusa jamii katika idara zote huku akiwaponda wanaomsema vibaya Rais akidai kuwa wakapimwe akili. Mwashitete aliyedumu nafasi hiyo kwa mihura miwili ambapo miaka mitano iliyopita alikuwa diwani kupitia chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) ambapo pia alikuwa mwenyekiti wa vijana mkoani humo,alipohamia CCM aliukwaa tena udiwani. Alisema kata yake ina vijiji 6,vitongoji 31 ikiwa na wakazi zaidi ya 30,000 ambao awamu zilizopita walikuwa wakikabiliwa na changamoto nyingi zilizopatiwa majibu katika awamu ya sita,kwa kujengewa miradi sekta zote. Alisema katika utawala wake wa miaka mitano chini ya Rais Samia kata yake imenufaika zaidi kwa kuletewa mabilioni ya fedha kujenga mir...