Posts

Showing posts from July, 2025

KAMATI YA MAAFA YA WILAYA YATAKIWA KUWA TAYARI WAKATI WOTE KUWEZA KUKABILIANA NA MAAFA

Image
Na Israel Mwaisaka, Sumbawanga Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga na Mwenyekiti wa Kamati ya Usimamizi wa Maafa ya Wilaya, Mhe. Nyakia Ally Chirukile amezindua rasmi mafunzo ya usimamizi wa maafa kwa wajumbe wa kamati za wilaya hiyo, akisisitiza umuhimu wa kuwa tayari kabla ya majanga kutokea. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mafunzo hayo yaliyofanyika kwa ushirikiano kati ya Ofisi ya Waziri Mkuu – Idara ya Menejimenti ya Maafa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP), Chirukile amesema kuwa maafa kama maporomoko ya ardhi, mlipuko wa kipindupindu, radi na ajali za majini yameathiri jamii na uchumi wa wilaya hiyo. “Kuchukua hatua kabla ya majanga ni nafuu zaidi kuliko kushughulika na athari. Mafunzo haya ni nyenzo ya kuongeza ufanisi wetu katika kuzuia na kukabili majanga,” amesema Mhe. Chirukile. Kwa upande wake Kanali Selestine Masalamado kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu – Idara ya Maafa, amesema mafunzo hayo ni utekelezaji wa Sheria ya Usimamizi wa Maafa Na. 6 ya mwaka 2022, na yana ...

WASIMAMIZI WA UCHAGUZI NGAZI YA JIMBO WAMETAKIWA KUFUATA KANUNI NA MAELEKEZO YA TUME KUEPUSHA MALALAMIKO NA MIGOGORO

Image
Na Israel Mwaisaka,Rukwa WASIMAMIZI  wa uchaguzi kutoka ngazi ya mikoa na majimbo ya Rukwa na Katavi wameaswa kusoma katiba,sheria,kanuni.taratibu na miongozo mingine ili iwawezeshe kutekeleza vyema majukumu yao yatakayowezesha kufanikisha uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba,2025. Hayo yamesemwa na mjumbe wa tume huru ya taifa ya Uchaguzi  (INEC) Magdalena Rwebangira alipokuwa akifungua mafunzo kwa waratibu wa uchaguzi,wasimamizi wa uchaguzi na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ndani ya jimbo yakiwa na lengo la kuwawezesha kuwajibika kwa weredi mkubwa katika mchakato mzima wa uchaguzi. Alisema kuwa anatambua kuwa zoezi zima kuelekea uchaguzi mkuu ni mchakato mkubwa ,hivyo ni muhimu kufuata katiba,sheria,kanuni na miongozo ikiwa ni pamoja na kuvishirikisha vyama vyote vya siasa vyenye usajiri  kamili katika hatua zote kwa kuzingatia matakwa ya kikatiba,sheria,kanunu na taratibu zilizowekwa. Amedai kuwa ni muhimu kwa Wasimamizi hao kujiepusha kuwa sehemu ya chanzo cha migogoro,Mala...

WANANCHI SONGWE WACHEKELEA VIFAA TIBA,WAMTAJA RAIS DKT,SAMIA.

Image
BIIION150 ZA RAIS DKT,SAMIA ZATUMIKA UNUNUZI WA VIFAA TIBA  KATIKA UTAWALA WAKE.                                         MAKALA Na Ibrahim Yassin,Songwe ‘’uwepo wa vifaaa tiba zikiwemo mashine za kisasa umepunguza msongamano wa wagonjwa kutibiwa kwa waganga wa tiba za jadi,ambao wengi wao walipoteza maisha,Rais Dkt,Samia ametupa matumaini ya kuishi’’. IMEELEZWA kuwa uwepo wa vifaa tiba zikiwemo mashine za kisasa katika vituo vya kutolea tiba halmashauri ya wilaya ya Songwe kumepu nguza vifo kwa baadhi ya wagonjwa hasa mama wajawazito walioenda kutibiwa kwa waganga wa tiba za kienyeji, Dira kamilifu  imeelezwa. Wakizungumza jana kwa nyakati tofauti wilayani humo,wakazi wa wilaya hiyo,wameeleza kuwa wamepata matumaini mapya kutokana na mabore sho makubwa yaliyofanyika kwenye vituo vya kutolea tiba baada ya serikali ya awamu ya sita kufunga mashine za kisasa. Amos Zakayo mkazi wa Mkwajuni,amesema wilaya ya Songwe ni moja ya wilaya mpya nchini zilikokuwa zikikabiliwa na upungufu wa vifaa t...

BIL 6.830.ZA RAIS DKT SAMIA ZATUMIKA KUJENGA VITUO VYA KUTOLEA TIBA NA UNUNUZI WA VIFAA.

Image
                        MAKALA ‘’serikali ya awamu ya sita umeondoa vifo vya mama na mtoto,kwa kujenga zahanati kila kijiji,kituo cha afya kila kata na hospital ya wilaya,awali tulitibiwa kwa waganga wa kienyeji na wakunga wa jadi,wengi walipoteza maisha hasa watoto baada ya kuzaliwa’’ Na Ibrahim Yassin,Songwe MAELFU ya wakazi wa wilaya ya Songwe mkoani hapa,hasa wajawazito waliokuwa wakitegemea kuzalishwa na wakunga wa jadi wamepata matumaini mapya baada ya serikali kujenga hospitali ya kisasa ikiwa na vifaa tiba. Wilaya ya Songwe ni moja ya wilaya 5 mkoa wa Songwe yenye post kodi namba 54100, Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 229,219   . Katika wilaya ya Songwe maeneo maarufu ni Mkwajuni ambako ndio makao makuu ya wilaya. Saza ni eneo maarufu kwa uchimbaji madini na kuna mgodi mkubwa wa Shanta Gold Mine, Kanga na Mbangala. Ilianzishwa mwaka 2015 ikiwa imepakana na wilaya ya Momba mkoani hapa na Milele mkoani Katavi upande wa chini na upande wa chini imepakana na wilaya y...

MADEREVA WASHINDWA KUJIZUIA UJENZI BARABARA ZA MCHEPUO ZILIVYOPUNGUZA AJALI.

Image
  WAOMBA UJENZI USOGEZWE MAENEO YOTE KOROFI HADI TUNDUMA--   Na Ibrahim Yassin,Songwe   ‘’kipndi cha nyuma kulikuwa na ajali za magari zilizoua watu mfululizo,Rais Dkt,samia alileta fedha kujenga barabara za mchepua zilizopunguza ajali’’.   Na Ibrahim Yassin,Songwe   KATIKA kuhakikisha ajari za mara kwa marazinamalizwa,serikali ya awamu ya sita katika bajeti ya Mwaka 2024—2025 kupitia wizara ya ujenzi ilitenga fedha kwa ajili ya ukarabati wa miundombinu ya barabara mkoani humo.   Barabara ya Tanzam inategemewa na nchi nyingi za kusini mwa afrika na imekuwa ikitumika na magari mengi hasa ya mizigo (Maroli) ambapo imekuwa ikipatwa na changamoto za foreni na ajali.   Kutokana na umuhimu wa barabara hiyo serikali imeamua kujenga njia za mchepuko ili magari yakiwa mengi kuhepuka foreni na ajali mengine yanachepuka kupita njia hizo hali iliyoongeza usalama zaidi. Godwin moyo,dereva wa Roli namba BAZ 1033 kutoka nchini Zambia anasema serikali ya Tanzania imefanya kitu kizuri kujenga barabara ...

WANANCHI SONGWE WACHEKELEA VIFAA TIBA,WAMTAJA RAIS DKT,SAMIA.

Image
Na Ibrahim Yassin,Songwe ‘’uwepo wa vifaaa tiba zikiwemo mashine za kisasa umepunguza msongamano wa wagonjwa kutibiwa kwa waganga wa tiba za jadi,ambao wengi wao walipoteza maisha,Rais Dkt,Samia ametupa matumaini ya kuishi’’. IMEELEZWA kuwa uwepo wa vifaa tiba zikiwemo mashine za kisasa katika vituo vya kutolea tiba halmashauri ya wilaya ya Songwe kumepu nguza vifo kwa baadhi ya wagonjwa hasa mama wajawazito walioenda kutibiwa kwa waganga wa tiba za kienyeji, Dira kamilifu  imeelezwa. Wakizungumza jana kwa nyakati tofauti wilayani humo,wakazi wa wilaya hiyo,wameeleza kuwa wamepata matumaini mapya kutokana na mabore sho makubwa yaliyofanyika kwenye vituo vya kutolea tiba baada ya serikali ya awamu ya sita kufunga mashine za kisasa. Amos Zakayo mkazi wa Mkwajuni,amesema wilaya ya Songwe ni moja ya wilaya mpya nchini zilikokuwa zikikabiliwa na upungufu wa vifaa tiba na hata watumishi kwa muda mrefu,akieleza katika awamu ya sita wameshu hudia vifaa tiba vikiwekwa zikiwemo  mashine za kisas...

SERIKALI YAWAHAKIKISHIA WANANCHI KUBORESHWA KWA MPAKA WA KASESYA

Image
Na Baraka Lusajo,Rukwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Makongoro Nyerere amesema Serikali inakusudia kuanza uboreshaji wa mpaka wa kasesya unaounganisha kati ya nchi ya Tanzania na Zambia ikiwa ni pamoja na kukamilisha ujenzi wa Barabara ya Matai Kasesya kwa kiwango cha Lami. Ameyasema hayo baada ya kutembelea Kituo cha forodha cha Kasesya Wilayani Kalambo Mkoani humo na kusema serikali katika mwaka wa fedha 2025/2026 inakusudia kuanza ujenzi wa majengo mapya ya Taasisi za umma ikiwemo kituo cha polisi, uhamiaji , majengo ya ukusaji mapato (TRA) Pamoja na nyumba za watumishi. Licha ya hilo Mkuu wa Mkoa aliwahakikishia wananchi Wilayani humo kukamilishwa kwa Barabara ya Matai Kasesya ikiwa ni Pamoja na kuboreshwa kwa bandari ya Kabwe kwa lengo la kurahisisha usafirishaji wa mizigo Kwenda katika nchi jirani ikiwemo Kongo, Zambia na Burundi. Hata hivyo kwa mwaka wa fedha 2024-2025 kituo cha forodha Kasesya Wilayani Kalambo kilifanikiwa kuvuka lengo la ukusanyaji wa mapato kwa kukusanya kiasi cha sh...

Wananchi wahamasishwa matumizi ya lishe bora kulinda afya

Image
Na Israel Mwaisaka,Nkasi Katika kukabiliana na changamoto za kiafya zinazotokana na lishe duni Wataalamu wa afya wameyatumia maadhimisho ya siku ya afya na lishe ya kijiji katika kutoa elimu ya lishe ikiwa ni pamoja na kuwapatia vipimo mbalimbali vya kiafya Ili kufahamu hari za afya zao. Akizungumza na Wananchi wa kijiji cha Majengo afisa lishe wa wilaya Nkasi Theresia Matoke amesema kuwa bado Kuna changamoto kubwa ya lishe katika jamii na kuwa kutokana na Hilo ndiyo maana wao wameamua kuitumia siku hiyo ya afya na lishe ya kijiji katika kutoa elimu mahususi kwa nadharia na vitendo. Amezitaja changamoto za kilishe kuwa ni utapiamlo,upungufu wa virutubisho, vitamin na madini na kupeleka kukosekana kwa damu na Wanawake kupata shida wakati wa kujifungua ikiwa ni pamoja na uzito uliopitiliza unaosababisha magonjwa ya yasiyo ya kuambukiza. Matoke ameitumia siku hiyo kuitaka jamii kuhakikisha kuwa inajenga utamaduni wa kupima afya zao Kila wakati ikiwa ni pamoja na kuthibitisha kwamba chaku...

MAKONGORO AFUNGUA JENGO JIPYA LA TAWI LA TCB SUMBAWANGA, APONGEZA KUIMARIKA KWA HUDUMA ZA KIFEDHA.

Image
Na Israel Mwaisaka, Rukwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa,  Charles Makongoro Nyerere, ameipongeza Benki ya Biashara Tanzania (TCB) kwa kuendelea kuimarisha huduma za kifedha nchini, wakati wa uzinduzi wa jengo jipya la benki hiyo Sumbawanga. Akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa Jengo hilo iliyofanyika jana Julai 10, 2025 Makongoro amesema kuwa uzinduzi wa jengo hilo ni ushahidi wa dhamira ya benki hiyo katika kusaidia maendeleo ya kiuchumi kwa wananchi, hasa wajasiriamali wadogo, wa kati na wakubwa, wanawake na vijana hususani waishio vijijini. "Tukio hili la kihistoria linaashiria mafanikio makubwa ya benki hii, na hatua muhimu kuelekea ujumuishi wa huduma za kifedha, ukuaji wa uchumi, na maendeleo ya Taifa," alisema RC Makongoro. Mkuu huyo wa mkoa ameishukuru TCB kwa kuguswa na changamoto za kijamii mkoani Rukwa kwa kusaidia sekta za elimu na afya, akisisitiza kuwa huo ni mfano wa taasisi inayowekeza katika ustawi wa jamii. Kwa upande wake, Afisa Mtendaji Mkuu wa TCB,  Adam Mihay...

Mwanafunzi matatani kwa kumuua mdogo wake wakicheza mchezo wa kupigana kwa fimbo

Image
Na Israel Mwaisaka, Nkasi Jeshi la Polisi la Polisi mkoani Rukwa linamshikilia Mwanafunzi wa kidato cha kwanza shule ya sekondari Mtenga wilayani Nkasi mkoani Rukwa Samwel Kayoka (16)kwa tuhuma za mauaji baada ya kumuua mdogo wake Jackson Kayoka (14) kwa fimbo walipokuwa wakicheza mchezo wa kupigana kwa fimbo. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kamanda wa Polisi mkoani Rukwa SACP Shadrack Masija ni kuwa tukio Hilo limetokea Jana majira ya saa sita mchana katika kijiji cha Mtenga "A" wakati Watoto hao walipokuwa wakicheza kwa kupigana na fimbo na Katika mchezo huo marehemu alipigwa na fimbo kichwani na kudondoka chini. Alisema kuwa baada ya marehemu kuanguka chini na kupoteza fahamu alichukuliwa na kukimbizwa katika Zahanati ya Mtenga na wakati jitihada za kumpatia matibabu zikiendelea alipoteza maisha. Kamanda Masija alidai kuwa wao kama jeshi la Polisi kwa sasa wanaendelea kumshikilia Mtoto huyo huku wakiendelea na uchunguzi wa kina juu ya tukio Hilo na kuwa baaba ya h...