WANAFUNZI WACHEKELEA DARASA LA MAABARA KUSHEHENI VIFAA,WAMTAJA RAIS DKT,SAMIA.



Na Ibrahim Yassin,Mbozi

‘’Ilikuwa ngumu wanafunzi kupenda masomo ya Sayansi kutokana na kutokuwepo kwa vifaa,baada ya Rais Samia kutupa vifaa wanafunzi wanayapenda masomo,ufauru umeongezeka,diwani Mwashitete akiwezesha vyakula’’

UKOSEFU wa Darasa la maabara na vitendea kazi vya kujifunzia kwa vitendo masomo ya Sayansi chanzo wanafunzi nchini kutoyapenda masomo ya Sayansi,imeelezwa.

Masomo ya Sayansi yanaumuhimu mkubwa kwa wanafunzi ambapo baadhi ya wanafunzi wanagoma kuyasoma masomo hayo wakidai ni magumu na kupelekea kuchagua masomo mengine.

Kutokana na hali hiyo,Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt,Samia Suluhu imeweka utaratibu mzuri wa kujenga madarasa mapya yakiwemo ya Maabala na vifaa vyake hali iliyorudisha hali kwa wanafunzi kuanza kuyapenda masomo hayo.

Mwandishi wa kituo hiki jana alifika katika wilaya ya Mbozi mkoani Songwe na kutembelea shule zilizopo kata ya Harungu na kujionea darasa la maabara likisheheni vifaa muhimu vya kujifunzi kwa matendo wanafunzi.

Jeremiah Petro mwanafunzi wa shule ya sekondari Harungu alisema yeye na wenzake wanajisikia vizuri kusoma kwa vitendo baada ya darasa la Maabara kuwepo vifaa muhimu hali inayowapa matumaini ya kupata madaraja ya juu wa alama A.

Magerina Mwmgoge mwanafunzi sekondari hiyo,alisema wenzao waliohitimu kidato cha nne mwaka jana walipata ufaru mzuri masomo ya sayansi,hali iliyowapa matumani na wao kuingia kwa miguu miwili kusoma masomo hayo wakiwa na uhakika wa kupata lama A.



Alisema uwepo wa vifaa kunawasaidia kusoma kwa vitendo na muelekeo unaonekana,na kuwa anaiomba serikali iongeze maradufu vifaa vingine ili kuwaongezea Morali wanafunzi kuyapenda masomo hayo,huku wakimuahidi Rais Dkt,Samia ufauru wa alama A.

Mwl,Elinah Mwalwende Mkuu wa shule hiyo,alisema awali mazingira hayakuwa rafiki kwa wanafunzi kuyapenda masomo hayo,lakini awamu hii ya Rais Dkt,Samia Suluhu imeweza kuboresha mazingira rafiki mashuleni na kuamsha hali ya watoto kupenda shule.

Alisema katika darasa la Maabara limewekewa vifaa vya kutosha na toka vifaa viwekwe hakuna mwanafunzi anayefeli na kuwa diwani Mwashitete naye amekuwa mtari wa mbele kutembelea shule hiyo pamoja na kuleta vyakula.

Diwani wa kata ya Halungu,Mcg,Maarifa Mwashitete mbali na kuwapongeza walimu kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kuwafaurisha wanafunzi,alisema mazingira yaliyopo ni moja ya sababu pia ya kuwafanya wanafunzi wapende masomo hayo.

Mchungaji Mwashitete alisema ana kila sababu ya kuipongeza serikali ya Rais Dkt,Samia kwa kujenga shule mpya na kuboresha miundombinu ikiwemo madarasa ya maabala na kuweka vifaa vya kujifunzia huku akimuahidi Rais Samia ufaru mzuri watakao upata wanafunzi hao.

Kata ya Halungu ni moja ya kata kubwa wilayani Mbozi ambayo ilikuwa ikikabiriwa na changamoto nyingi awamu za nyuma,lakini awamu hii ya sita kila sekta imeboreshwa hali iliyopunguza hoja za maswali kwa wananchi dhidi ya viongozi wa kuchaguliwa.



Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa