NAUWASA wautambulisha mradi wa maji wa Mil.815
Na Israel Mwaisaka,Rukwa MAMLAKA ya maji mjini Namanyere NAUWASA imeutambulisha rasmi mradi wa upanuzi na uboreshaji wa maji Namanyere wenye thamani ya Tshs,mil.815 Akiutambulisha mradi huo kaimu mkurugenzi mtendaji NAUWASA Hamisi Honero amesema kuwa mradi huo umekwisha anza kutekeleza baada ya mchakato wa kuwapata wazabuni mbalimbali wa kutekeleza mradi huo kuwapatikana. Amedai kuwa katika kiasi hicho cha fedha cha mil.815 wao mpaka sasa wameshapata Tshs,Mil.700 na kuwa milioni 115 iliyobaki itaingia wakati wowote huku mradi huo ukiendelea kutekelezwa. Honero amesema kuwa katika mradi huo kuna shughuli nyingi zinatarajia kufanyika ambazo ni kujenga tank lenye ujazo wa lita 100.000 litakalokuwa juu ya mnara wa mita 9,kujenga nyumba 5 za mitambo katika maeneo ya Mabatini,Misunkumilo,Majengo na Nakambili. Kazi nyingingine ni ujenzi wa Chemba,uchimbaji wa visima vitatu,ununuzi wa mabomba yenye urefu wa km 15 kata zote,ununuzi wa pump 5,utafiti wa maji chini ya ardhi,usafishaji na upimaji...