Posts

Showing posts from September, 2024

WADAU WATOA YA MOYONI WAKIKOSHWA NA MIRADI YA RUWASA NA TARULA-RAIS SAMIA-RAS SENEDA WATAJWA.

Image
Na Ibrahim Yassin,Songwe SIKU chache baada ya mwenge wa uhuru kufika na kukagua miradi ya maendeleo hususani miradi muhimu ya miundombinu ya barabara na madaraja na ile ya maji,wananchi wametoa ya moyoni baada ya miradi hiyo kumkosha mkimbiza mwenge kitaifa. Mkoa wa Songwe ni moja ya mikoa mipya nchini uliomegwa kutoka mkoa wa Mbeya Octoba 18/2015 ikiwa na wilaya 4 na halmashauri  5 yaani Ileje,Momba,Tunduma,Mbozi na Songwe na wilaya 4 ambazo ni Momba,Songwe,Ileje na wilaya mama ya Mbozi. Mkoa una kata 94,vijiji 307 huku ikiwa na wakazi 1.344,687 kati ya hao wanaume ni 643,679 wanawake ni 701,008 ambapo idadi kubwa ya wakazi ni wakulima na wafugaji,hii ni kwa mujibu wa sense ya watu na makazi. Kwa mwaka 2022/23 Rais Dkt,Samia alitoa Tsh,Bilioni 20.9 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya barabara,na mwaka 2023/2024 alitoa Bilioni 17, Kwa upande wa miradi ya maji Rais Dkt,Samia mwaka 2023/24 baada ya kutoa fedha wakala ulipanga kutekeleza jumla ya miradi 1,546 katika mikoa 25 nchini ikiw...

WADAU WATOA YA MOYONI WAKIKOSHWA NA MIRADI YA RUWASA NA TARURA-RAIS SAMIA-RAS SENEDA WATAJWA

Image
NaIbrahim Yassin,Songwe SIKU chache baada ya Mwenge wa uhuru kufika na kukagua miradi ya maendeleo hususani miradi muhimu ya miundombinu ya barabara na madaraja na ile ya maji,wananchi wametoa ya moyoni baada ya miradi hiyo kumkosha mkimbiza mwenge kitaifa. Mkoa wa Songwe ni moja ya mikoa mipya nchini uliomegwa kutoka mkoa wa Mbeya Octoba 18/2015 ikiwa na wilaya 4 na halmashauri 5 yaani Ileje,Momba,Tunduma,Mbozi na Songwe na wilaya 4 ambazo ni Momba,Songwe,Ileje na wilaya mama ya Mbozi. Mkoa una kata 94,vijiji 307 huku ikiwa na wakazi 1.344,687 kati ya hao wanaume ni 643,679 wanawake ni 701,008 ambapo idadi kubwa ya wakazi ni wakulima na wafugaji,hii ni kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi. Kwa mwaka 2022/23 Rais Dk,Samia alitoa Tsh,Bilioni 20.9 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya barabara,na mwaka 2023/2024 alitoa Bilioni 17, Kwa upande wa miradi ya maji Rais Dkt,Samia mwaka 2023/24 baada ya kutoa fedha wakala ulipanga kutekeleza jumla ya miradi 1,546 katika mikoa 25 nchini ikiwem...

TUTUNZE MAZINGIRA KWA TAIFA ENDELEVU.

Image
Na Ibrahim Yassn Rukwa ZAIDI ya Milioni137  zitatumika kutengeneza vitalu vya miti katika hifadhi ya msitu wa mbizi kwa lengo la kupata miche itakayopandwa na taasisi mbalimbali kwa ajili ya uboreshaji wa mazingira katika mkoa wa Rukwa. Akitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi huo muhifadhi mkuu wa msitu wa mbizi (TFS) katika halmashauri ya manispaa ya Sumbawanga Egnasi Lupala amesema zaidi ya miti laki nane imepandwa ikiwa mradi huo unalengo la kuotesha miche milioni moja na laki mbili na hamsini kwa lengo la kuhifadhi mazingira. "Msitu wa mbizi unaekali 14.7 ili kuendeleza uhifadhi wa mazingira tunalengo la kupanda miti milioni moja na laki mbili na hamsini na mpaka sasa tumefanikiwa kupanda kuotesha miche laki nane . Naye kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Godfrey Mnzava amesema serikali inaunga mkono jitihada zina zofanywa na taasisi binafsi katika suala la kukuza maendeleo ya nchi. Akizungumza baada ya kutembelea kiwanda cha kuchakata minofu ya samaki cha Alpha Tanganyika Fravo...

TEHAMA WATAKIWA KUDHIBITI MIFUMO YA KAMERA.

Image
Na Ibrahim Yassin.Rukwa MWENGE wa uhuru umeweka jiwe la msingi la uwekaji wa kamera za CCTV za utoroshwaji wa mapato katika Kijiji cha Mwimbi kata ya Mwimbi wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa zitakazosaidia kudhibiti utoroshwaji wa mapato yatokanayo na mazao katika halmashauri hiyo. Akizungumza jana kiongozi wa mbio za mwenge wa Uhuru kitaifa Godfrey Mnzava alisema ni wakati sasa wataalamu wa tehama kuhakikisha wanaendelea kudhibiti mifumo hiyo pamoja na kukomesha vitendo vya watu wanao haribu mifumo hiyo. " Niwatake tehama hakikisheni hakuna anaeingilia mifumo ya kamera maana teknolojia inavyokuwa hata wasiyoitakia mema nchi yetu nao wanajaribu kuendana na teknolojia hiyo"amesema Mnzava. Wakati huo huo Tsh, milioni 436,567,205 zimetatua kero ya maji katika kijiji cha Kalaela kata ya Nsundu wilaya ya Kalambo kwa ujenzi wa tanki la maji utakao hudumia kaya zaidi ya 2000 wa kijiji hicho. Akizungumza kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Godfrey Mnzava aliwataka wananchi kutunza miundo...

Kayogolo achaguliwa tena kuwa Makamo Mwenyeki halmashauri Nkasi

Image
Na Israel Mwaisaka,Nkasi BARAZA la Madiwani wa halmashauri ya wilaya Nkasi limemchagua Stephen Kayogolo kuwa makamo mwenyekiti wa halmashauri. Madiwani hao Kwa kauli Moja walitoa tamko la Kayogolo kuwa makamo mwenyekiti akiwa ni mgombea pekee kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambapo CHADEMA wao hawakupeleka mgombea kwenye kinyang'anyiro hicho. Pia Nestory Kaloto diwani wa kata ya Namanyere amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa kamati ya Uchumi,Ujenzi na Mazingira na Carolina Makandi diwani wa kata ya Paramawe amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa kamati ya Elimu,Afya na Maji. Kayogolo Kwa upande wake amewashukuru Madiwani wenzie Kwa kumpa kura zote na kuwa Imani waliyokuwa nayo Madiwani wenzie kwake atahakikisha atawatumikia vema katika nafasi hiyo Kwa kumshauri mwenyekiti wa halmashauri vyema Ili kuweza kuyafikia malengo. Mwenyekiti wa halmashauri Pankrasi Maliyatabu Kwa upande wake amewataka Madiwani kuendeleza kazi kubwa waliyoianza ya kuhakikisha halmashauri inaongeza makusanyo yake kwa k...

Mwenge walidhishwa na miradi ya Tarura na Ruwasa Songwe

Image
Na Ibrahim Yassin,Songwe KIONGOZI wa mbio za mwenge kitaifa Godfrey Mzava amekoshwa na usimamizi mzuri uliotukuka katika miradi ya maji inayotekelezwa na mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira (Ruwasa ) na wakala wa barabara vijijini na mijini (Tarura) ambapo mameneja wa taasisi hizo wamepongezwa kuzitendea haki fedha za serikali. Mzava katika ukaguzi wa miradi hiyo akianzia wilayani Songwe aliridhishwa na ujenzi wa mradi wa maji uliokuwa ni kero ya muda ya mrefu katika kata ya Kanga baada ya serikali kutoa Milioni 144 kujenga mradi ambao umetajwa kuwa ni muoarobaini kwa wakazi wa eneo hilo. Kutokana na kero hiyo ya muda mrefu kwa wakazi wa vijiji vitatu imetatuliwa baada ya Serikali kutoa Tsh, 144.040,799.33 kujenga mradi huo kumaliza changamoto hiyo. Mbali na mradi huo mradi mwingine ulizinduliwa wilayani Momba ambapo kiongozi huyo aliridhishwa kwa usimamizi uliotukuka na baada ya hapo siku iliyofuata mwenge ulienda wilayani Mbozi na ukakagua mradi wa maji Ukwile. Mradi huo wa U...

Miradi ya Tarura Na Ruwasa ilivyomkosha kiongozi wa mbio za Mwenge mkoani Songwe

Image
Na Ibrahim Yassin,Songwe KIONGOZI wa mbio za Mwenge kitaifa Godfrey Mzava amekoshwa na usimamizi mzuri uliotukuka katika miradi ya maji inayotekelezwa na mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira (Ruwasa ) na wakala wa barabara vijijini na mijini (Tarura) ambapo mameneja wa taasisi hizo wametwa kuzitendea haki fedha za serikali. Mzava katika ukaguzi wa miradi hiyo akianzia wilayani Songwe aliridhishwa na ujenzi wa mradi wa maji uliokuwa ni kero ya muda mrefu katika kata ya Kanga baada ya serikali kutoa Milioni 144 kujenga mradi ambao umetajwa kuwa ni muoarobaini kwa wakazi wa eneo hilo. Kutokana na kero hiyo ya muda mrefu kwa wakazi wa vijiji vitatu imetatuliwa baada ya Serikali kutoa Tsh, 144.040,799.33 kujenga mradi huo kumaliza changamoto hiyo. Meneja wa mkoa anayesimamia taasisi ya maji safi na usafi wa mazingira (Ruwasa) Mhandisi,Charles Pambe na meneja wakala wa barabara mijini na vijijini Tarura Mhandisi Kilian Haule pamoja na mameneja waliopo wilayani wametajwa kufanya kazi ...

MADIWANI NKASI WATAKIWA KUWA CHACHU YA UKUSANYAJI WA MAPATO

Image
Na Israel Mwaisaka,Nkasi Madiwani wa halmashauri ya wilaya Nkasi wametakiwa kuongeza nguvu ya usimamizi Kwa Maafisa Watendaji wa kata zao kuhakikisha kwamba Kasi ya ukusanyaji wa mapato inaongezeka. Hayo yamesemwa na mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya Nkasi Pankrasi Maliyatabu kwenye kikao Cha Baraza la Madiwani Leo ambapo amedai kuwa Moja ya jukumu lao kubwa katika utekelezaji wa majukumu yao ni pamoja na suala la Zima la kuhakikisha katika maeneo Yao makusanyo ya halmashauri yanapatikana. Amedai kuwa Ili halmashauri iweze kupata uwezo wa kushughulika na uendelezaji wa Miradi mbalimbali ya maendeleo katika maeneo Yao ni lazima fedha iwepo na hili kuweza kufanikisha katika Hilo ni lazima kuwepo na makusanyo,hivyo ni lazima kila Mmoja aone kwamba ukusanyaji wa mapato ni jukumu lake Kwa kuwasimamia na kutoa ushirikiano wa kutosha Kwa Watendaji wao. Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri Afraha Hassan Kwa upande wake amedai kuwa suala la upotevu wa mapato Kwa Watendaji wa kata amelipata na k...

Kijiji chapata maji toka kianzishwe mwaka 1980, Wananchi wafurahia

Image
Na Ibrahim Yassin,Songwe Zaidi ya wananchi 7.000 wa vijiji vilivyopo kata ya Ukwile wilaya ya mbozi mkoani Songwe wameanza kunywa maji safi na salama baada ya miaka 40 tangu kijiji hicho kianzishwe mwaka 1980 . Jambo hili limefahamika jana baada ya mwenge wa uhuru kuzindua rasmi mradi wa maji katika kijiji cha chimbuya uliogharimu zaidi ya shingi million 500. Ester Mbwete mkazi wa Chimbuya amesema ana kila sababu ya kuipongeza serikali kwa kukamilisha mradi huo kwani wataondokana na homa za matumbo kwani toka mwaka 1980 kijiji kilipoanzishwa hawakuwahi kuwa na huduma hiyo. Happiness Mgetta mkazi wa Chumbuya amesema wakati mradi huo unaanzishwa waliona ni kama ndoto lakini tayari mradi umekamilika na kuzinduliwa na Mwenge wa uhuru hivyo anaipongeza serikali kukam ilisha mradi huo. "Wakati mradi unaanzishwa wahandisi kutoka mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira walikuwa wanafika mara kwa mara kufuatilia mradi huu hadi leo tunakunywa maji safi , ni jambo la kumshukuru Mungu...

KIONGOZI WA MBIO MWENGE AAGIZA UJENZI WA DARAJA MTO ISENGA UHARAKISHWE NA UBORA UZINGATIWE.

Image
Na Ibrahim Yassn Songwe.  WANANCHI kata ya Chitete Wilayani Ileje Mkoani Songwe wataondokana na adha ya kivuko katika mto Isenga Ikumbilo ambao unaunganisha vijiji zaidi ya  7 kutokana na ujenzi wa daraja la kudumu kujengwa ambalo linatarajiwa kumalizika Januari 2025 . Kwa muda mrefu wananchi walikuwa wakikumbwa na kadhia hiyo hasa nyakati za mvua za masika lakini serikali ya awamu ya sita imepeleka fedha kujenga daraja hilo. Elizabeth Kandonga mkazi wa Ikumbilo amesema  kukamilika kwa daraja hilo wataondokana na adha iliyopo hasa kipindi cha mvua kutokana na mto huo kujaa maji huku daraja hilo likisababisha wananchi kusombwa na maji na wengine kupote za maisha. Gordon Kibona mkazi wa Chitete amesema Daraja hilo litakuza uchumi kwani vijiji 7 ambavyo vilikuwa vikikosa mawasiliano nyakati za mvua sasa vitafunguka  Wananchi hao wameyasema hayo leo September 4/2024 wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi kati ka daraja hilo ambalo linagharimu kiasi cha Shilingi Milioni 447 likisimamiwa na Wak...

RPC Songwe amtembelea mzee Mkisi Mwalimu mstaafu wa chio cha Polisi Moshi

Image
Na Ibrahim Yassn, Songwe IMEELEZWA kuwa jamii nchini inatakiwa kujenga utamaduni wa kuwaenzi wazee ili kuwatia moyo kutokana na kazi kubwa waliyoifanya ya kulitumikia Taifa. Kauli hiyo imetolewa leo Septemba 3,2024  na kamanda wa polisi mkoani Songwe Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Augustino Senga wakati akizungumza na Dira Kamilifu. Amesema wazee ni dhahabu hivyo ukiwepo utaratibu wa kuwatembelea na kupokea ushauri wao mambo yatakwenda vyema huku baraka zikitawala katika mioyo. Kamanda Senga amesema yeye ni muumini wa kufanya hivyo na anajisikia fahari kuwatembelea wazee waliomtangulia huku akipokea mawazo na ushauri unaomsaidia kuongeza uwajibikaji uliotukuka. "Najisikia fahari ninapozungumza na wazee kupokea mawazo yao na kuyafanyia kazi, siku ya Agosti 31 mwaka huu nilienda kumtakia hali mzee Mkisi na kupokea mawazo mbalimbali kutoka kwake, ni vyema tukajenga utaratibu huu tuwape faraja wazee wetu"amesema. Hata hivyo kamanda Senga aliongozana na Afisa Mnadhim...

Mapokezi ya Mwenge wa uhuru Songwe ulivvyoleta shangwe kwa Wananchi

Image
Na Ibrahim Yassin,Songwe. MAAFISA, wakaguzi na askari wa vyeo mbali mbali wakidumisha ulinzi na usalama katika mapokezi ya Mwenge wa Uhuru uliopokelewa Kijiji cha Ifwenkenya wilayani Songwe mkoani Songwe tarehe 31 Agosti, 2024. Katibu Tawala Mkoa wa Songwe Happyness Seneda kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Songwe Mhe. Daniel Chongolo amepokea Mwenge wa Uhuru ukitokea Mkoa wa Mbeya. Seneda ameeleza kuwa Mwenge wa Uhuru ukiwa Mkoani Songwe utakimbizwa Kilomita 634.2 kati ka wilaya 4 na halmashauri 5 za na utatembelea, utakagua na kuzindua miradi mbalimbali ya maen deleo 46 yenye thamani ya zaidi ya Bilioni 18. Mwenge wa Uhuru umepokelewa katika uwanja wa Shule ya Msingi Ifenkenya wilaya ya Songwe tayari ukiwa salama kwa ajili ya kukimbizwa Mkoani humo. Mwenge huo utaanza halmashauri ya Songwe,Mo mba,Mbozi Ileje na Tunduma huku kila halmashau ri ikifanywa maandalizi ya kutosha kuhakikisha mambo yanaenda sawa. Wananchi kwa upande wao  wameungana na viongozi mbalimbali kuhudhuria mapokezi hay...

Mradi wa maji wa Mil.144 wazinduliwa na mbio za Mwenge

Image
Na Ibrahim Yassin,Songwe KERO ya muda ya mrefu ya uhaba wa maji kata ya Kanga wilayani Songwe mkoani hapa imepatiwa majibu baada ya serikali kutoa Milioni 144 kujenga mradi ambao umezinduliwa na mbio za mwenge. Kutokana na kero hiyo ya muda mrefu kwa wakazi wa vijiji vitatu imetatuliwa baada ya Serikali kutoa Tsh, 144.040,799.33 kujenga mradi huo kumaliza changamoto hiyo. Akizungumza jana mbele ya mkimbiza mwenge kitaifa ,Mkuu wa wilaya hiyo Solomon Itunda alisema kwa muda mrefu wananchi walipata shida kwa kukosa maji safi lakini serikali ya awamu ya sita chini ya Dkt, Samia imesikia kilio chao na kuwafuta machozi. Alisema serikali imemtua mama ndoo kichwani baada ya kero ya muda mrefu kwani Rais Dkt.Sam ia amekuwa msikivu na anajali shida za wananchi hivyo aliwataka wananchi kuutunza mradi. Akizungumzia mradi huo meneja wa wakala wa maji na usafi wa mazingira (RUWASA) wilayani Songwe Boniface Mfungo alisema mradi huo unatekelezwa kwa gharama ya Tsh, 488.930,43 7.64. Alisema mradi wa ...