Posts

Showing posts from November, 2023

Mwanamke auawa kwa imani za kishirikina

Image
Na Israel Mwaisaka, Sumbawanga MWANAMKE aliyefahamika kwa jina la Mwashi Salita (60) mkazi wa Kijiji cha Chombe wilayani Sumbawanga mkoani Rukwa ameuawa kwa kukatwa mapanga kutokana na Imani za kishirikina. Tukio hilo lilitokea Novemba 20 majira ya saa 1 za usiku ambapo watu wasio fahamika walimvamia mwanamke huyo nyumbani kwake na kisha kumkata mapanga na kukimbilia kusikojulikana. Akitoa taarifa za tukio hilo jana Kamanda wa Polisi mkoani humo, Shadrack Masija alisema kuwa watu hao walikwenda nyumbani kwa marehemu wakiwa na silaha mbalimbali za jadi ambapo walipofika walimkuta akiwa na wajukuu wake kisha walimvamia na kuanza kumpiga. "kabla ya watuhumiwa hao kumkata mapanga, walimpiga kichwani kwa kutumia kitu butu, kitendo kilichosababisha kuanguka chini na kushindwa kupata msaada kwa kua aliokua nao walikua ni watoto kisha wakamkata mapanga katika sehemu mbalimbali za mwili wake" alisema. Baada ya kumkata mapanga walimsababishia majeraha makubwa yaliyovuja damu nyingi na...

ST.Anselim yawanoa vijana elimu ya ufundi na Wazazi watakiwa kuwapeleka watoto wao shule za ufundi

Image
Na Israel Mwaisaka,, Nkasi MKURUGENZI wa chuo cha ufundi cha St Anselim Vocational training Centre kilichopo Chala ambaye pia ni Paroko wa Parokia ya Chala wilayani Nkasi mkoani Rukwa Anselim Kashatila amesikitishwa na kitendo cha vijana waliokuwa wakisoma chuo hicho kuacha masomo na kwenda kuzurura mtaani licha ya masomo yao kutolewa bure chini ya wafadhili kutoka nchini Ujerumani. Akizungumza jana kwenye mahafali ya kwanza ya chuo hicho amesema kuwa yeye katika urafiki na wenzake walioko Ujerumani walimwambia wamusaidie nini ndipo yeye alipoomba ajengewe chuo cha ufundi lakini pia hawakuchoka wakatoa na ufadhili bure wa masomo katika shule hiyo lakini amesikitishwa baada ya kuona baadhi ya vijana waliofadhiliwa kukimbia masomo na kwenda kuzurura mitaani. Alisema kuwa katika mpango huo wa ufadhili wa masomo waliandikisha Wanafunzi 57 lakini cha ajabu katika mwaka wa kwanza tu vijana 30 walikimbia masomo na kubaki 27 ambao mpaka jana walihitimu masomo yao huku wakiwa na ujuzi katika...

Wachungaji waaswa kuitangaza injli ya kweli na kuepuka injili potofu za mafuta na maji

Image
MAKAMO mkuu wa chuo cha Bibilia cha AMO (African Ministries Outreach Bible College) Mhandisi Nelson Makoti amewataka wahitimu wa kozi ya uchungaji katika chuo hicho kwenda kuitangaza injili ya kweli na kuachana na injili potofu zilizoenea sasa za maji na mafuta zilizolenga kuwaibia Wananchi. amesema kuwa hivi sasa kumeibuka injili za kitapeli na kwa kuwa wengi hawaifahamu Biblia kiundani ujikuta wakitapeliwa na kujikuta na wao wakieneza injili ambazo ni kinyume na mwenyezi Mungu. Hivyo aliwataka wahitimu wa kozi hiyo ya uchungaji kuwa mstari mbele kuitumia elimu ya Biblia waliyoipata kwa kuitangaza injili iliyo ya kweli na kuondokana na injli za mazoea kama walivyokuwa wakihubiri huko nyuma kabla ya kupata elimu hiyo ya Biblia. Makoti alisema kuwa Wachungaji wengi uendesha makanisa bila ya kuwa na elimu ya Biblia wakidai kuwa wamepata upako wa kiroho kutoka kwa Mungu huku wakiwadanganya waumini wao kuwa mbona Yesu hakusoma lakini alifanya kazi ya Mungu sawa sawa na kuwa hayo ni manen...

Paroko ataka vijana kuchangamkia elimu ya ufundi

Image
Na Israel Mwaisaka,Nkasi MKURUGENZI wa chuo cha ufundi cha St Anselim Vocational training Centre kilichopo Chala ambaye pia ni Paroko wa Parokia ya Chala wilayani Nkasi mkoani Rukwa Anselim Kashatila amesikitishwa na kitendo cha vijana waliokuwa wakisoma chuo hicho kuacha masomo na kwenda kuzurura mtaani licha ya masomo yao kutolewa bure chini ya wafadhili kutoka nchini Ujerumani. Akizungumza jana kwenye mahafali ya kwanza ya chuo hicho amesema kuwa yeye katika urafiki na wenzake walioko Ujerumani walimwambia wamusaidie nini ndipo yeye alipoomba ajengewe chuo cha ufundi lakini pia hawakuchoka wakatoa na ufadhili bure wa masomo katika shule hiyo lakini amesikitishwa baada ya kuona baadhi ya vijana waliofadhiliwa kukimbia masomo na kwenda kuzurura mitaani. Alisema kuwa katika mpango huo wa ufadhili wa masomo waliandikisha Wanafunzi 57 lakini cha ajabu katika mwaka wa kwanza tu vijana 30 walikimbia masomo na kubaki 27 ambao mpaka jana walihitimu masomo yao huku wakiwa na ujuzi katika f...

Radi yaua mtu mmoja na Ng'ombe 27

Image
Na Israel Mwaisaka,Sumbawanga MKAZI wa kijiji cha Muze kilichopo katika Bonde la Ziwa Rukwa wilayani Sumbawanga Edward Silungu (32) amekufa papo hapo baada ya kupigwa radi iliyoambatana na mvua kubwa. Edward alifikwa na umauti akiwa amjikinga na mvua chini ya mti akiwa na baba yake mzazi Ibrahim Silungu (75) ambaye hakujeruhiwa. Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Nyakia Ally Chirukie amethibitisha tukio hilo ambalo lilitokea Jumatatu asubuhi. Kufuatia mkasa huo amewataadharisha wananchi kuchukua tahadhari katika msimu huu wa Masika kwa kutokimbilia kukaa chini ya miti. Katika tukio lingine lilitokea Jumatatu asubuhi , Mkuu wa Wilaya Chirukie amethibitisha kuwa ng'ombe 27 wamekufa baada ya kupigwa na radi huku wengine wawili wakiwa wamejeruhiwa . Akizungumza na wanahabari jana jioni Chirukie amesema vifo vya ng'ombe vilitokea katika maeneo mawili tofauti katika Manispaa ya Sumbawanga katika kijiji cha Tamasenga ambapo walikufa ng'ombe 25 huku wawili wamejeruhiwa. Huku katika ki...

Jela maisha kwa ubakaji

Image
Na Gurian Adolf, Sumbawanga MAHAKAMA ya hakimu mkazi wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa imemuhukumu kifungo cha Maisha jela, Joseph Nyansio (40) mkazi wa Kijiji cha Kasekela wilayani Sumbawanga baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kuwabaka wajukuu wake wawili. Kamanda wa Polisi mkoa wa Rukwa, Shadrack Masija ametoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari Jana na kusema kuwa watoto hao (majina yamehifadhiwa) walikua na umri wa miaka 7 na mwingine miaka 8. Alisema kuwa siku ya June 29 mwaka huu majira ya mchana, mtuhumiwa huyo aliwalaghai watoto hao kuwa anawapeleka shambani ili akawachumie matunda ndipo alipo wafanyia kitendo hicho. Kamanda huyo alisema kuwa baada ya mtuhumiwa kukamatwa na upelelezi kufanyika ndipo alipofikishwa mahakamani mbele ya hakimu Thomas Bigambo na baada ya ushahidi kukamilika, siku ya Octoba 30 alihukumiwa kifungo cha Maisha jela. Aidha Kamanda Masija akitoa wito kwa wanaume mkoani humo kuacha kuendekeza tamaa za kimwili ndiyo imekua sababu ya kuwafanyia matukio ya ...