ZAIDI YA BILIONI 4.8 ZATOLEWA KWA WAKAZI 494 KUPISHA MRADI WA KISASA.
Na Ibrahim Yassin,Songwe WANANCHI zaidi ya 494 wilayani Mbozi mkoani Songwe wameanza kupokea fedha kwa ajili ya malipo ya fidia ya kupisha mradi wa kitaifa wa kituo cha ukaguzi wa pamoja (Iboya). Asilimia 70 ya bidhaa zinazovushwa bandari ya Dar es salaam zinapita kwenye mpaka wa Tunduma,ujenzi wa ikiwemo njia nne zitahepusha msongamano wa magari naajari na kuongeza tija za kiuchumi. Akizungumza leo Agost 31/ 2025 Meneja wa wakala wa barabara mijini na vijijini (Tanroads) mkoani Songwe Mhandisi Suleiman Bishanga amesema wapo kuwapatia cheki za malipo wananchi kupisha mradi. Anasema kabla ya kuwapatia malipo hayo serikali ilifanya tathimini kwa kuwashirikisha wenyeji wa maeneo hayo ambapo kila mlengwa analipwa kutokana na ukubwa wa eneo husika. Amesema eneo hilo la Iboya patajengwa mradi mkubwa wa kitaifa cha kisasa cha ukaguzi wa magari yaendayo katika nchi za kusini mwa afrika (Sadc) itakaoendana na njia nne inayotarajiwa kujengwa. ''Lengo la serikali ni kujenga barabara ya ...