Posts

Showing posts from January, 2024

TANGAZO LA SHULE YA AWALI NA MSINGI

Image
Shule ya Awali na msingi ya ANSADE MEMORIAL PRE & PRIMARY SCHOOL -imeanza kutoa huduma na sasa imeanza kupokea Wanafunzi. -Shule hiyo inafundisha kwa lugha ya Kiingereza -Shule ina mandhari mazuri na ada yake ni nafuu sana. -Shule ipo mjini Namanyere wilayani Nkasi mkoani Rukwa karibu kabisa na uwanja wa Sabasaba -kwa mawasiliano zaidi .0683294360,0786825145 na 0762860415 Shule hiyo pia ina eneo zuri la mapumziko kwa Watoto nyakati za mchana ikiwemo hata kulala Mpeleke mwanao kwa elimu bora zaidi

Ajeruhiwa na Tembo akienda shambani

Image
Na Israel Mwaisaka,Nkasi KIJANA mmoja aliyefahamika kwa jina la Shija Machenga (19) mkazi wa kijiji cha Itete kata ya Itete wilayani Nkasi mkoani Rukwa amejeruhiwa vibaya baada ya kukanyagwa na Tembo. Akizungumzia tukio hilo afisa mtendaji wa kata ya Itete Justin Mangazini amesema kuwa tukio hilo limetokea jana majira ya saa 2 za asubuhi wakati kijana huyo alipokuwa akielekea shambani. Amesema kuwa kijana huyo alikua ameongozana na Mbwa wake watatu alipokuwa akielekea shambani na wakiwa njiani katika eneo la kitongoji cha Sokonso Mbwa walinusa harusu ya Tembo na kuanza kumfuata alipokuwa na ndipo alipoanza kuwafukuza Mbwa hao . Katika jitihada za kujiokoa Mbwa hao dhidi ya Tembo walikimbilia alipokuwepo mwenye Mbwa pasipo yeye kujua na alipomuona Tembo akiwa karibu na yeye aliamua kuanza kukimbia ili kujiokoa lakini alianguka na ndipo Tembo huyo alipomkanyaga na kumjeruhi vibaya katika mguu wake ambapo nyama za mguuni zilinyofoka na kumsababishia maumivu makali. Diwani wa kata ya ...

Madeni ya Manispaa yamuumiza kichwa DED

Image
Na Musa Mwangoka,Rukwa Uongozi wa halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa, unaumiza kichwa kutatua changamoto ya mlundikano wa madeni yanayoikabili halmashauri hiyo. Mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga, Catherine Mashalla alisema hayo jana katika hafla fupi ya kukabidhi gari aina ya Coaster yenye thamani ya Sh milioni 65.8 kwa viongozi wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Manispaa ya Sumbawanga, hafla iliyofanyika katika ofisi za CWT mkoani Rukwa. Alisema kwamba madeni halali yaliyohakikiwa ambayo halmashauri hiyo inadaiwa na watumishi wake na wazabuni ni zaidi ya Sh 2.9 bilioni fedha ambazo wanapambana kuzilipa kadri wanavyokusanya kutoka katika vyanzo mbalimbali vya mapato yao. "Watumishi kwa ujumla wakiwemo walimu wanadai Sh 1.5 bilioni 1.5 fedha zilizotokana na likizo, uhamisho madeni ya wastaafu......huku Sh 1.4 bilioni zikiwa ni madeni ya wazabuni" alisisitiza Alisema wameiomba serikali kuu iwasaidie kulipa baadhi ya madeni kwa kuwa kwa halmashauri pekee ni m...

Benki ya NMB imekabidhi vitanda 40 kwa shule ya sekondari ya Wasichana Kalambo

Image
Na Israel Mwaisaka,Rukwa BENKI ya NMB kanda ya nyanda za juu jana imekabidhi msaada wa vitanda 40 vyenye thamani ya shilingi Milioni kumi na laki nne kwa shule ya sekondari ya wasichana kalambo kama sehemu ya utatuzi wa changamoto hiyo katika shule hiyo. Akikabidhi vitanda hivyo 40 vitakavyokuwa na uwezo wa kutumiwa na Wanafunzi 80 kwa katibu tawala wa wilaya Kalambo Selivily Ndumbaro meneja wa NMB kanda ya nyanda za juu Straton Chilongola amesema msaada huo ni sehemu ya faida wanazozipata na kuweza kuirudisha kwa jamii. Amesema kuwa Benki hiyo ilipata ombi kutoka kwa viongozi wa serikali wilayani Kalambo juu ya uhitaji wa vitanda kwa shule hiyo ya wasichana ambayo ni mpya na kuona umuhimu wa jambo hilo na wao kulipa uzito mkubwa na kuamua kutoa vitanda 40 vitakavyokwenda kutatua tatizo la ukosefu wa vitanda lililopelekea baadhi yao kulala chini Katibu tawala wa wilaya Selivil Ndumbalo kwa upande wake aliishukuru benki hiyo kwa msaada huo mkubwa na kuahidi kuvitunza vyema vitanda hi...

Wavuvi ziwa Tanganyika waomba kupewa elimu ya utotoleshaji vifaranga vya Samaki

Image
Na Israel Mwaisaka,Rukwa Siku chache baada ya serikali kutoa tangazo la kusitishwa kwa shughuli za uvuvi kwa muda wa miezi mitatu katika ziwa tanganyika ,wavuvi kutoka wilaya za Nkasi na Kalambo mkoani Rukwa wameiomba serikali kuwachimbia mabwawa sambasamba na kuwapatia elimu ya utotoleshaji vifaranga vya samaki ili kujikimu kimaisha. Wameyasema hayo kupitia mkutano wa hadhara uliofanyika katika soko kuu la kimataifa la samaki Kasanga wilayani Kalambo mkoani Rukwa na kuiomba serikali kuwapatia vizimba na kuwajengea mabwawa ya samaki . mapema akizungumza na wavuvi kutoka katika vijiji 16 vya mwambao wa ziwa Tanganyika wilayani kalambo mkoni Ruwa naibu waziri wa mifugo na uvuvi Alexanda Mnyeti amelezea mikakati ya sekali katika kuwawezesha wavuvi. Naibu waziri wa mifugo na uvuvi Alexander pastory mnyeti ametangaza mpango wa serikali wa kupumzisha shughuli za uvuvi katika ziwa Tanganyika kwa miezi mitatu ili kuwezesha samaki kuzaliana na kuongeza tija kwa wavuvi wanaofanya shughuli za...

UWT watakiwa kujipanga na uchaguzi serikali za mitaa

Image
Na Israel Mwaisaka,Nkasi MBUNGE wa viti maalumu mkoa Rukwa Bupe Mwakang'ata (CCM) amewataka Wananchi kujitokeza kujiandikisha kwenye daftari la wakazi ambalo litatumika kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa. akizungumza kwenye kikao cha baraza la Wanawake (UWT) jana amesema kuwa zoezi la uandikishaji wakazi litaanza hivi karibuni hivyo litakapoanza ni vyema wakajitokeza kujiorodhesha kwani daftaro hilo ndilo litakalotumika kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa. amesema kuwa ili uweze kupata haki ya kushiriki kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa na kuweza kuwachagua viongozi wawatakao ni lazima wajiorodheshe katika daftari hilo. "Wanawake kama mnataka chama chetu kishinde kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa ni lazima sisi wenyewe tujitokeze kujiandikisha kwenye daftari hilo na tuwahamasishe na wenzetu kujitokeza kujiandikisha pindi zoezi litakapoanza" alisema Na aliwataka Wajumbe wa baraza hilo la UWT kuendelea kupendana na kuepuka migawanyiko ndani ya chama na wasikubali k...

JESHI LA POLISI LAKOSHWA NA USHIRIKIANO ULIOPO NA WANANANCHI

Image
Na Ibrahim Yassin,Songwe JESHI la polisi nchini limewapongeza wananchi wa mikoa mbalimbali nchini hasa ile iliyopo kwenye mipaka na nchi jirani ikiwemo mkoa wa Songwe kwa kuvuka mwaka kwa amani ukilinganisha na miaka ya nyuma. Mkoa wa Songwe una wilaya mbili zinazopakana na nchi jirani ambazo ni Ileje inayopakana na nchi ya Malawi na halmashauti ya mji Tunduma inayopakana na nchi ya Zambia. Akizungumza Januari 2 /2024 kwenye ukumbi wa jeshi hilo mkoani Songwe msemaji wa Jeshi la polisi nchini David Misime, alisema elimu inayoendelea kutolewa na jeshi la polisi kwa wananchi kupitia makundi mbalimbali kuhusu kuacha masuala ya uhatifu umesaidi kupunguza vutugu. Alisema katika sherehe za mkesha wa kuvuka mwaka 2023 na kuukatibisha mwaka 2024 hakuna matukio ya uharifu,wizi,ubakaji na unyang’anyi wala watu kuumizana na kwamba hii inatokana na watu kuelewa madhata ya kufanya uhatifu. ‘’Ndugu wanahabari watu wamesherehekea sikuku ya mwaka mpya kwa amani,tunataka amani hii iendelee kuwa hivyo n...

Rukwa Press Club yapitisha mabadiliko madogo ya katiba

Image
Na Israel Mwaisaka,Rukwa CLUB ya Waandishi WA HABARI Mkoani Rukwa imefanya mabadiliko madogo katika katiba Yao kwa kuongeza baadhi vipengele ambavyo havikuwemo katika katiba Yao ilikuendana na mazingira ya sasa kiutendaji. Mkutano mkuu WA dharura uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita uliweza kukubaliana kufanya marekebisho katika vipengele vitatu ambapo kamati ya nidhamu,maadili na usuluhishi lmebaki kuwa kamati ya nidhamu na maadili na kuongeza kipengele Cha kamati ya utatuzi WA migogoro. Pia katika mkutano mkuu huo waliweza kupitisha azimio la uanzishwaji WA Kikoba ambacho kitaanza mapema January,2024 katika kukabiliana na changamoto za umasikini katika tasnia hiyo ya Habari. Akitoa ufafanuzi katika mkutano mkuu huo mwenyekiti WA Club ya Waandishi WA HABARI mkoa Rukwa Nswima Ernest alidai kuwa marekebisho hayo ya katiba yametokana na mkutano mkuu WA UTPC ambao ulipendekeza Vilabu vya Waandishi WA HABARI kufanya mabadiliko hayo ya katiba Ili kuendana na mabadiliko ya kiutendaji kat...