BIL,7 KUJENGA DARAJA KUUNGANISHA MOMBA NA MBEYA,WAKULIMA WACHEKELEA.



Na Ibrahim Yassin,Songwe

WANANCHI wa vijiji vilivyopo bonde bonde la Kamsamba wilayani Momba mkoani Songwe,wameiponge za serikali kwa kusikia kilio chao kwa kuwajengea daraja kubwa linalounganisha vijiji vya bonde la Kamsa mba hadi Mlowo kuelekea Mbeya.              

Bonde la Kamsamba linatumika kwa kilimo cha mazao mbalimbali ambapo wakulima watarahisishiwa kusafirisha mazao ya nafaka na samamki ambapo awali walitumia njia ya mzunguko kusafirisha bidhaa hizo kwa bei kubwa.

Wakizungumza jana wakati wa ziara ya kikazi ya katibu tawala mkoani Songwe wakazi hao walisema kukamilika kwa daraja hilo kutaongeza fursa za kiuchumi na hata kuipa wilaya yao sura mpya kutokana na kutokuwa na barabara ya Lami.



Isack Mkumbwa mkazi wa Kamsamba alisema walilazimika kusafirisha mazao kupitia njia ya Sumbaw anga Tunduma hadi Mbeya wakitumia fedha nyingi kutokana na ukosefu daraja katika barabara hiyo na kwamba mradi ukikamilika fursa za kiuchumi zitaongezeka.

Samwel Sinkala mkazi na mkulima wa Msangano, alisema daraja hilo litaongeza thamani ya mazao yao,kwani walilazimika kuuza kwa bei ya hasara baara ya kushindwa kusafirisha kwenye masoko ya uhakika kutokana na ubovu wa barabara na ukosefu wa daraja hivyo walanguzi waliwafuata masha mbani.

 Mhandisi Suleiman Bishanga Meneja wa Tanroads alisema mradi huo,umefadhiriwa na Benki ya Dunia unatekelezwa na mkandalasi,M/s Abemulo Contractors kwa Tshs,7,365.251 na mkataba ulisainiwa Novemba 1/202 4,ujenzi ulianza Novemba 21/2024 na utakuwa wa miezi 12.

Bishanga alisema hadi sasa mkandarasi amelipwa malipo ya awali Tsh,2,209,575,386.4 sawa na asilimia 30 ya gharama ya mradi,na kuwa ujenzi wa daraja hilo utaenda smbamba na makaravati na miundombin u ya maji kwani mvua za El-nino pamoja na kimbunga Hidaya ziliharibu miundombinu.


Alisema katika eneo hilo panajengwa Daraja la Mpapa lenye urefu wa mita 60 na barabara unganishi katika barabara kuu ya kimkoa ya Kamsamba –Mlowo hadi mkoa wa Songwe,ambapo kukamilika kwa barabara hiyo kutaongeza fursa za kiuchumi.

Akiwa katika ziara ya kikazi wilayani humo,katibu tawala mkoani Songwe Happiness Seneda,alipongeza hatua za mradi huku akishauri kasi iongezeke kwa kuzingatia ubora ili mradi uendane na thamani ya fedha ili fursa za kiuchumi ziongezeke.

Mwisho.

 

Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa