Posts

Showing posts from March, 2024

Huduma bora za afya zapunguza vifo vya Mama na Mtoto

Image
Na Baraka Lusajo,Kalambo Hospitali ya wilaya ya kalambo mkoani Rukwa kwa kipindi cha miezi sita imewezesha wanawake 860 kujifungua kati yao wanawake 741wakijifungua kwa njia ya kawaida na 119 wakijifungua kwa njia ya upasuaji huku vifo vya mama na mtoto vikipungua kutoka 11-8 kwa mwaka 2023. Hayo yamebainishwa na mratibu wa huduma za mama na mtoto wilayani humo Bakari Ndarusi wakati wa utoaji elimu kwa wanawake wanao jifungua katika hosptali hiyo,ambapo amesema licha ya hilo hospitali hiyo inahudumia wastani wa watoto 180 hadi 200 na watoto njiti 6 kwa kila mwezi. Aidha amesema hospitali hiyo inahudumia wanawake wanaojifungua wapatao 8-9 kwa siku na kubainisha kuwa hadi kufikia march 2024 wanawake 2218 wamepatiwa huduma za Mama na mtoto na kwamba kila mwezi Wanawake 164 wamekuwa wakihudhuria huduma hizo . Kwa upande muuguzi mkuu wa hospitali hiyo , Diana Didi amesema licha ya hilo hospitali hiyo imekuwa ikihudumia wanawake 30 kwa siku na kuwataka wanawake kujenga mazoea ya kuwahi ...

Mbaroni kwa ubakaji na mauaji ya Mwanamke

Image
Na Israel Mwaisaka,Rukwa Polisi mkoani Rukwa inamshikilia Daudi Mwanalinze (25) akituhumiwa kumbaka na kumsababishia kifo Martha Zacharia (32) . Mtuhumiwa huyo wa mauaji na marehemu ni wakazi wa eneo la Makutano lililopo nje kidogo ya Mji wa Sumbawanga. Kamanda wa Polisi mkoa wa Rukwa,Shadrack Masija amethibithisha kutokea ka tukio hilo wakati akizungumza na wanahabari jana ofisini kwake mjini Sumbawanga. Akizungumzia hilo alisema mwili wa Martha ulikutwa Februari, 02mwaka huu asubuhi katika eneo la Makutano nje kidogo ya Mji wa Sumbawanga. " Mwili wa marehemu ulifanyiwa ukaguzi wa kitabibu katika Hospitali ya Rufaa mkoa wa Rukwa mjini Sumbawanga na matokeo yake yalionesha kuwa alibakwa au kuingiliwa kimwili" alieleza. Aliongeza kuwa Polisi kwa kushirikiana na wananchi walifanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo wa mauaji Machi 06, mwaka huu mkoani Kigoma alikokuwa amejificha. " Tumemkamata mtuhumiwa wa mauaji (Daud) Machi,06 mwaka huu huko mkoani Kigoma alikokuwa amekimbili...

JINSI VIJANA WALIVYOENDELEZA MAISHA YAO KUPITIA KAMPUNI YA LIMA KWANZA WAKIWAASA MACHANGUDOA.

Image
                  MAKALA WANAWAKE WANAOJIUZA WAPEWA MCHINGO KUINUA VIPATO VYAO. Na Ibrahim Yassin,Songwe Imeelezwa kuwa vijana wakiwemo wanawake nchini wametakiwa kutojiingiza kwenye kazi za hatari zikiwemo za wizi,Uharifu na ukahaba na badala yake wametakiwa kujiingiza kufanya kazi za viwandani ili wajipatie kipato hahali. Mkoa wa Songwe ni moja ya mikoa iliyojaliwa kuwa na Viwanda vingi vikiwemo vya uchakataji wa mazao ambapo kiwanda kilichopo kwenye kampuni ya Lima Kwanza pekee kikiajiri vijana zaidi ya 300 wanaofanya kazi mbalimbali na kujiingizia kipato. Uwepo wa viwanda ni moja sababu ya kupunguza uzururaji na ukahaba ikiwemo uharifu,kwani vijana wengi wakiingizwa kufanya kazi viwandani matukio ya kiharifu yatapungua na hata kutokomezwa kabisa. Kumekuwa na kawaida kwa akina dada wengi hasa wenye umri mdogo kujiingiza kwenye kufanya kazi Baa na wengine wakiingia kwenye mkumbo wa kuuza miili yao kwa wanaume kwa ajili ya kupata fedha zinazotajwa ni haramu. Kwa upande wa vijana wengi...

WANAWAKE WATAKIWA KUTOJIINGIZA KWENYE KAZI ZA KUJIUZA,WAOMBE KAZI VIWANDANI.

Image
Na Ibrahim Yassin,Songwe WANAWAKE wa wilaya mbalimbali zilizopo mkoani Songwe,wametakiwa kuacha tabia ya kujiuza miili yao kwa wanaume kama ni njia ya kujipatia kipato na badala yake waombe kazi kwenye kampuni mbalimbali zitakazowatoa kwenye lindi la umasikini. Kauli hiyo imetolewa  Machi 14/2024 na  Vicent Samwel,Meneja wa kampuni ya Lima Kwa nza Limited inayojishughulisha na uchakataji na usindikaji mazao ya kahawa na Parachichi kwe nye kijiji na kata ya Nyimbili wilayani Mbozi mkoani humo. Samwel amesema mkoa wa Songwe unajiwanda vingi ambapo vijana wengi wakiwemo wana wake wanafanya kazi za mikataba na kujiinua kiuchumi hivyo wanawake wanaotegemea kuuza miili yao (Kudanga) ili wapate fedha waache na waombe kazi viwandani. Alisema kampuni ya Lima Kwanza inayoongozwa na Mkurugenzi mtendaji Tinson Nzunda imetoa ajira kwa vijana na wanawake zaidi ya 300 wanaofanya kazi ya kuchambua kahawa na parachichi huku wengine wakiwa mashambani wamevuka hatua kubwa kutokana na mishahara waipatayo....

Watakiwa kujitokeza kupiga kura uchaguzi mdogo ili kutimiza haki yao ya kikatiba

Image
Na Israel Mwaisaka,Sumbawanga MWENYEKITI wa tume ya taifa ya Uchaguzi taifa ,jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele amewataka wananchi wa kata ya Kabwe wilayani Nkasi mkoani Rukwa kujitokeza kupiga kura kwenye uchaguzi mdogo wa udiwani katika kata hiyo ili kuweza kutimiza haki yao ya kidemokrasia. Akizungumza jana katika ofisi ya mkurugenzi mtendaji wa wilaya amesema kuwa uchaguzi huo unatarajia kufanyika Marchi 20 na uchaguzi huo utafanyika katika kata 23 za Tanzania bara. Amesema kuwa kwa kata ya Kabwe vyama sita vya siasa vimejitokeza kusimamisha Wagombea ambavyo ni NCCR-Mageuzi,ADA Tadea,CCM,ACT-Wazalendo,CHAUMA na chama cha UDP Jaji Mwambegele amedai kuwa karibia maeneo yote kutakakofanyika uchaguzi huo mdogo kila kitu kinaenda vizuri na kuwa kwa sasa vyama vyote vya siasa vinaendelea na kampeni ya kunadi sera zao. Hivyo amevitaka vyama vya siasa kuendelea na mchakato wa kampeni za kisiasa vizuri kwa kufuata kanuni na sheria huku akiwatoa wasiwasi wananchi ya kuwa atakayes...

Mzazi awamotisha Walimu baada ya shule kufanya vizuri kwenye matokeo ya darasa la saba

Image
Na Israel Mwaisaka,Rukwa MMOJA ya Wazazi wa watoto wanaosoma shule ya msingi Kipundukala kata ya Namanyere wilayani Nkasi mkoani Rukwa ametoa motisha kwa Walimu wa shule hiyo kwa kuwanunulia vitenge doti 8 baada ya shule hiyo kufanya vizuri kwenye mtihani wa darasa la saba baada ya kushika nafasi ya saba kiwilaya na tisa kimkoa. Akizungumza kwenye hafla fupi ya kukabidhiwa zawadi hiyo ya vitenge leo mwalimku mkuu wa shule hiyo Josephat Labani aliwaeleza walimu wa shule hiyo kuwa mmoja wa wazazi wa Watoto wanaosoma katika shule hiyo Issa Kabuje ametoa zawadi ya vitenge kwa walimu wa shule hiyo kama Motisha kwao kutokana na maendeleo mazuri kwa shule hjiyo kuendelea kupandisha ufaulu kwa kila mwaka. Alidai kuwa vitenge hivyo vimekabidhiwa ofisini kwake siku chache zilizopita na kuwa leo ni siku muhimu ya kukabidhiwa kila mwalimu zawadi yake ya kitenge iliyotolewa na mzazi huyo baada ya kuitambua kazi nzuri inayofanywa na walimu. Mwenyekiti wa kamati ya shule hiyo Angelina Mwampashi ame...

Mtandao wa Polisi Wanawake TPF-NET Nkasi watoa msaada kwa Wazee kuelekea maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani

Image
Na Israel Mwaisaka,Nkasi KATIKA kuelekea maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani yatakayofanyika Marchi 8 ya mwaka huu mtandao wa Polisi Wanawake TPF-NET wilayani Nkasi mkoani Rukwa wametoa msaada wa vitu mbalimbali vya matumizi ya nyumbani kwa Wazee vyenye thamani ya zaidi ya laki tano. Akikabidhi vitu hivyo kwa Wazee hao Mwenyekiti wa Mtandao wa Polisi Wanawake wa wilaya Mkaguzi msaidizi wa Polisi Ivona Mwanga amesema wao kama polisi wanawake wanautambua mchango wa Wazee katika taifa hilo na ndiyo maana wameamua kuwaona na kuwapatia baadhi ya vitu kama sehemu ya utambuzi wa mchango wao mkubwa kwa taifa. Alisema kuwa siku ya Wanawake Duniani imelenga kutambua mchango wa Wanawake katika jamii na kubwa ndani ya jeshi la Polisi ni kukabiliana na vitendo vya ukatili kwa kuweka usawa katika mizania ya haki kwani kila mmoja ana haki ya kuishi bila kubughudhiwa bila kujali jinsi yake. Mwanga amedai kuwa Wazee ni moja ya kundi muhimu ambalo limepigania haki mbalimbali ikiwemo na za Wanawa...
Hhhhh
Vhhhhjjvccf

TAG kuadhimisha miaka 85 toka kuanzishwa kwake kwa mafanikio makubwa

Image
Na Israel Mwaisaka,Nkasi KANISA la Assemblies Of God Tanzania (TAG) wilaya Nkasi mkoani Rukwa linatarajia kufanya matendo mbalimbali ya kijamii na ya huruma katika kuelekea maadhimisho ya miaka 85 toka kuanzishwa kwa kanisa hilo hapa Nchini. Akizungumza na Waandishi wa habari jana Makamo mwenyekiti mwangalizi wa kanisa hilo sehemu ya Nkasi na mchunbgaji wa kanisa hilo Nkomolo Efraimu Lyandulu amesema kuwa wao kama kanisa katika kuelekea maadhimisho ya miaka 85 ya kanisa hilo watashiriki katika shughuli mbalimbali za kijamii ikiwa ni pamoja na kufanya matendo mbalimbali ya huruma. Amesema kuwa kwanza wanatarajia kutoa mifuko 10 ya saruji kwa shule ya msingi Nkomolo kama sehemu ya mchango wao kuchangia nguvu za wananchi katika ujenzi wa shule hiyo ikiwa ni pamoja na kwenda kuwatizama Wafungwa katika gereza la Kitete liliopo wilayani Nkasi. Alidai kuwa kanisa kama taasisi ukiachana na mambo ya kiroho ambayo yamekuwa yakifanyika kwa asilimia kubwa lakini pia linalo jukumu la kuhakikisha ...

DC Nkasi awataka Wananchi wa Kabwe kulinda amani kipindi hiki cha uchaguzi mdogo

Image
Na Israel Mwaisaka,Rukwa MKUU wa wilaya Nkasi mkoani Rukwa Peter Lijualikali amewataka wakazi wa kata ya Kabwe wilayani Nkasi kuwa watulivu katika wakati huu wanapoelekea kufanya uchaguzi mdogo wa udiwani kata hiyo. Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara jana katika kijiji cha Kabwe amesema kuwa wao kama serikali watahakikisha kuona kwamba uchaguzi huo unafanyika katika mazingira mazuri na ya uwazi na kuwa atakayeshinda katika uchaguzi huo ndiye atakayetangazwa. Alisema kuwa hakuna sababu ya kuwa na wasiwasi juu ya hilo na kuwa sasa washikamane katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye kampeni za vyama vya siasa na kuwa amani ikitawala kutakua na utulivu utakaowasaidia wao kufanya maamuzi sahihi ya kuchagua kiongozi mzuri. ‘’kata hii ina historia ya kuwa na vurugu hasa katika nyakati kama hizi za uchaguzi hivyo nawasihi sana muachane na vurugu na atakayejihusisha kwa namna yoyote na vurugu atachukuliwa hatua kali za kisheria’’alisema Kata ya Kabwe inafanya uchaguzi mdogo baada ya aliyek...