Posts

Showing posts from October, 2023

Mvua yaleta maafa nyumba 30 zaezuliwa 150 wakosa makazi

Image
Na Israel Mwaisaka, Kalambo JUMLA ya watu 150 wamebaki bila makazi baada ya nyumba 30 kuezuliwa paa na nyingine zimebomoka kufuatia mvua kubwa iliyonyesha juzi katika Kijiji cha Kaluko kata ya Chitete wilayani Kalambo mkoani Rukwa. Akizungumza na mwandishi wa habari hizi jana Mwenyekiti wa serikali ya kijiji hicho, Edwin Kasama alisema kuwa mvua hiyo ilianza kunyesha Siku ya Octoba 26 majira ya saa 10 jioni zikiwa zimeambatana na upepo mkali. Alisema kuwa ulianza upepo mkali Kisha ikafuatia mvua kubwa ambapo ilisababisha kubomoka baadhi ya nyumba kijijini hapo huku nyumba nyingine zikiezuliwa mapaa na kuziacha baadhi ya familia bila nyumba za kuishi. "Baadhi ya wanakijiji nyumba zao zimebomoka kabisa hawana hata sehemu ya kulala tena wana watoto hivyo tunaiomba serikali iwasaidie kwakua wanapitia wakati mgumu kwakua vitu vyao vimeharibika kabisa" alisema Kasama. Mmoja wa wakazi wa Kijiji hicho Paskalia Katata alisema kuwa tukio hilo limewaacha katika hali mbaya kwani hawana f...

Kijana adaiwa kutekwa ndugu wahaha kumtafuta

Na Mwandishi wetu,Sumbawanga WATU wasiojulikana wanadaiwa kumteka kijana anayefahamika kwa jina la Friday Mbalwa (33) mkazi wa kitongoji cha Chanji Manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa na Kisha kutokomea naye kusikojulikana. Kwamujibu wa mke wa kijana huyo Cecilia Saki, alisema kuwa tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia Oktoba 19 akiwa amelala chumbani na mume wake ndipo watu wapatao watano walivunja mlango wa nyumba wanayoishi na kuingia chumbani huku wakiwa na bunduki na mapanga. Alisema kuwa watu hao baada ya kuingia chumbani walimuamuru mwanamke huyo kujifunika shuka hadi usoni na kumuonya asipige kelele, kisha kumtaka Mbalwa ainuke kitandani na kuanza kumpiga. Inaidawa kuwa wakati wakimpiga Mwanamke huyo alisikia moja wa watu hao akimweleza mume wake kwamba......"tunafanya kazi pamoja za fundi kujenga lakini wewe unatudhulumu hatuwezi kukubali lazima tumalizane" alisema. Alisema kuwa baada ya watu hao kutembeza kichapo kwa Mbalwa waliondoka naye na kuelekea kusikojulikana...

CCM Rukwa watimuana kwa usaliti

Image
Na Israel Mwaisaka Sumbawanga CHAMA cha Mapinduzi (CCM) mkoani Rukwa kimewasimamisha uongozi viongozi wa chama hicho wanao tuhumiwa kukihujumu kwa kuwauzia kadi za Kieletroniki viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ili wazitumie katika mikakati yao ya kisiasa. Akitoa taarifa hiyo mwishoni mwa wiki Jana, Katibu wa Itikadi na uenezi wa chama hicho, Godfrey Mwanisawa alisema viongozi hao walikua wakichukua kadi za wanachama na kumuuzia Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Rukwa, Sadrick Malila, maarufu kwa jina la Ikuwo ili atangaze kuwa wanachama hao wamehamia Chadema na wamerudisha kadi za CCM. Alisema kuwa baadhi ya kadi hizo ni ya aliyekuwa mwana CCM mkongwe marehemu Chrisant Mzindakaya pia marehemu Zuberi Kauzeni ambaye alikua mwenyekiti wa Jumuia ya wazazi tawi la King'ombe Kata ya Majengo pamoja na kadi za Wanachama wengine ambao wamehama mkoani Rukwa. Katibu Mwenezi huyo alisema kuwa baadhi ya viongozi hao wa CCM waliokuwa wakiuza kadi hizo ni Chriss Mwalwanda ambay...

Viongozo CCM Rukwa watimuana kwa usaliti

Image
Na Israel Mwaisaka Sumbawanga CHAMA cha Mapinduzi (CCM) mkoani Rukwa kimewasimamisha uongozi viongozi wa chama hicho wanao tuhumiwa kukihujumu kwa kuwauzia kadi za Kieletroniki viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ili wazitumie katika mikakati yao ya kisiasa. Akitoa taarifa hiyo mwishoni mwa wiki Jana, Katibu wa Itikadi na uenezi wa chama hicho, Godfrey Mwanisawa alisema viongozi hao walikua wakichukua kadi za wanachama na kumuuzia Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Rukwa, Sadrick Malila, maarufu kwa jina la Ikuwo ili atangaze kuwa wanachama hao wamehamia Chadema na wamerudisha kadi za CCM. Amesema kuwa baadhi ya kadi hizo ni ya aliyekuwa mwana CCM mkongwe marehemu Chrisant Mzindakaya pia marehemu Zuberi Kauzeni ambaye alikua mwenyekiti wa Jumuia ya wazazi tawi la King'ombe Kata ya Majengo pamoja na kadi za Wanachama wengine ambao wamehama mkoani Rukwa. Katibu Mwenezi huyo amesema kuwa baadhi ya viongozi hao wa CCM waliokuwa wakiuza kadi hizo ni Chriss Mwalwanda ambay...

Watatu mbaroni kwa mauaji ya mfanyabiashara na kumpora mali

Image
Na Israel Mwaisaka, Sumbawanga JESHI la Polisi mkoani Rukwa linawashikilia wanaume watatu wakazi wa Kijiji cha Katazi wilayani Kalambo mkoani humo kwa tuhuma za kumpiga rungu kisha kumzika akiwa hai mfanyabiashara wa mazao Baraka Nyangala(30) lengo likiwa ni kupora fedha alizo kua ameenda kununulia mazao. Akitoa taarifa ya tukio hilo Kamanda wa Polisi mkoa wa Rukwa, Kamishina msaidizi wa Polisi (ACP) Shadrack Masija alisema kuwa tukio hilo lilitokea juzi Oktoba 16 ambako alikwenda kununua Maharagwe akiwa na watu walio muua. Inaidawa kuwa mfanyabiashara huyo ambaye ni mkazi wa mtaa wa Kasisiwe Manispaa ya Sumbawangaa alipigiwa simu na watuhumiwa ambao ni Frank Simsokwe (33), Edfonsi Simsokwe (28) ambao ni mkubwa na mdogo pamoja na Nikas Lunguya (38) kuwa wanamaharage hivyo walimuita ili aende akanunue. Baada ya marehemu kufika kijijini hapo wakatumia usafiri wa usafiri wa pikipiki wakidai kuwa wanampelekea sehemu yalipo maharage hayo na walipofika maeneo ya porini walimtaka mfanyabi...

Serikali kuwalipa wakulima wa mahindi fedha zao Oktoba 30

Image
Na Israel Mwaisaka,Rukwa KATIBU mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) taifa Daniel Chongolo amewataka Wakulima waliouzia mahindi serikali kupitia NFRA wawe na subira kwani mchakato unaendelea na malipo yanaweza kufanyika Oktoba 30 ya mwaka huu. Ameitoa ahadi hiyo jana katika kijiji cha Ntalamila kata ya Myula wilayani Nkasi alipokuwa akizungumza kwenye mkutano wa hadhara baada ya mbunge wa jimbo la Nkasi kusini Vicent Mbogo kumweleza Chongolo kuwa kilio cha watu wengi katika eneo hilo ni malipo ya mahindi waliyoiuzia serikali. Mbunge katika maelezo yake alisema kuwa wakazi wa wilaya Nkasi ni Wakulima na maisha yao kwa asilimia kubwa yanategemea kilimo na kuwa kitendo cha wao kutolipwa fedha zao kwa wakati kinawaumiza na kushindwa kufanya maandalizi ya kilimo katika msimu ujao wa kilimo kwa kununua pembejeo kwa wakati. Kufuatia hari hiyo katibu mkuu wa CCM taifa Daniel Chongolo alitoa ahadi kuwa ifikapo Oktoba 30 ya mwaka huu wakulima watakua wamelipwa fedha zao na kuwa hiyo ni kero ku...

Vikundi 200 Vya Wanufaika Wa TASAF Kuanzishwa Wilayani Kalambo

Image
Wanufaka wa mradi wa TASAF wilayani Kalambo mkoani Rukwa wametakiwa kujiunga kwenye vikundi vitakavyo wawezesha kukuza uchumi wa kaya kwa kuanzisha miradi ya pamoja na kupata mikopo itakayo wawezesha kuweka akiba na kujikwamua kiuchumi. Hayo yamebainishwa na mratibu wa TASAF wilayani humo Mariam Kimashi wakati wa kampeni ya uundwaji wa vikundi kwenye vijiji vya kata za Matai na Lyowa. amesema kwa kutambua umuhimu wa uwepo wa vikundi, Halmashauri imeanzisha mpango wa kuwaunganisha wanufaika kwenye vikundi na kwamba wanatarajia kuunda vikundi 200 ambapo kila kikundi kitakuwa na wanufaika 15. lengo la serikali ni kuwaweka pamoja wanakikundi ili kuongeza uchumi wa kaya na kwamba endapo kikundi kitafanya vizuri na kuwa na uwezo basi TASAF itakipatia ruzuku ya uzalishaji ili kuifanya kaya kujikwamua kiuchumi’’alisema KimashiHata hivyo baadhi ya wanufaika wa TASAF wilayani humo wameipongeza serikali kwa kuwawezesha kifedha na kwamba kuanzishwa kwa vikundi hivyo kutaenda kuwaondolea adha ya ku...