Posts

Showing posts from August, 2023

MWENGE WA UHURU 2023 WAZINDUA MIRADI YENYE THAMANI YA SHILINGI BILIONI 2.4 WILAYANI NKASI

Image
Mwenge wa Uhuru mwaka 2023 ukiongozwa na Ndugu Abdalla Shaib Kaim Leo Agosti 29 2023 umezindua miradi 03, umeweka jiwe la msingi Mradi 01na umekagua mradi 01 katika Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi yenye thamani ya Shilingi Bilioni 2.4 Miradi iliyozindundiliwa ni miradi wa Maji- Lyazumbi wenye thamani ya Shilingi Milioni 331,Mradi endelevu wa maji na usafi wa mazingirana maboresho ya wodi ya wazazi katika Zahanati ya Paramawe wenye thamani ya Shilingi Milioni 65 , mradi wa ujenzi wa vyumba vya madarasa 10 shule ya Sekondari Kirando yenye thamani ya shilingi Milioni 201, umeweka jiwe la msingi daraja la Kivunja lenye Thamani ya Shilingi Milioni Bilioni 1.6 na kukagua na kutembelea shuguli za vijana. Akiongea na hadhara ya wananchi Wilayani Nkasi katika Kata ya Kirando katika viwanja vya Polisi, Ndugu Abdala Shaibu Kaim ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi, RUWASA na TARURA kwa kuwa na miradi mizuri ambayo inazingatia ubora pamoja na thamani ya fedha huku akisisitiza kuhakikis...

Serikali yachanja mbuga, uwekezaji bandari Jumatatu, Agosti 28, 2023

Image
Dar es Salaam. Serikali imesema inaandaa nyaraka kwa ajili ya utekelezaji wa makubaliano ya uwekezaji wa bandari kati yake na Dubai. Hatua hiyo inakuja wakati bado kukiwa na ukinzani wa maoni, kuhusu makubaliano hayo kutoka kwa makundi mbalimbali nchini. Akijibu maswali ya waandishi wa habari katika mkutano Jumamosi Agosti 26, 2023, Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa alieleza hatua hiyo inafuata baada ya Serikali kushinda kesi hivi karibuni. “Hakuna ukimya, Serikali ilishasema kwamba inapokea maoni ya Watanzania, baada ya kukamilisha michakato yote. Bunge limeridhia, hatua inayofuata sasa ni kuandaa nyaraka. Zikikamilika ndiyo tunakwenda kuandaa miradi ya utekelezaji,” alisema Msigwa alipojibu swali la John Marwa wa Jambo TV. “Kinachofanyika ni hivi; baada ya makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Dubai ni mikataba ya utekelezaji. Hii mikataba ndiyo itakayosema sasa mradi wetu utakuwa namna gani, tunashirikiana kwenye eneo gani na mikataba hii itakuwa ming...

Mtumishi Halmashauri Ya Kalambo Mbaroni Kwa Kukutwa Na Mashine Bandia Ya Ukusanyaji Mapato.

Image
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Kalambo Shafii Mpenda Na Israel Mwaisaka,Rukwa Je shi la polisi Mkoani Rukwa linamshikilia Timoth Ngambeki ambae ni mtumishi wa Halmashauri ya Kalambo kwa tuhuma za kutumia mashine bandia na kutoa risiti feki kwa wananchi na kuisababishia serikali hasara ya shilling million thelathini na tisa na laki tano. Mapema leo akizungumza ofisini kwake mkurugenzi mtendaji Halmashauri ya Kalambo Shafi Mpenda alisema mtumishi huyo aligundulika kufanya kitendo hicho baada ya kushindwa kuwasilisha fedha Benk na kwamba baada ya ufuatiliaji zaidi kwenye mageti ya ukusanyaji mapato aligundua uwepo wa udanganyifu kwenye utoaji wa risiti. ‘’baada ya kugundua uwepo wa udanganyifu kwenye swala la ukusanyaji mapato nilianzisha utaratibu wa kuweka madaftari ya kusaini kwenye mageti yote yanayo unganisha halmanshauri za jirani na kuweka watu ambao walikuwa wakifanya kazi ya kupiga picha risiti za ushuru kisha kunitumia na wakati mwingine nilikuwa nikiamka usiku ...

Mtumishi Halmashauri Ya Kalambo Mbaroni Kwa Kukutwa Na Mashine Bandia Ya Ukusanyaji Mapato.

Image
Mkurugenzi mtendaji halmashauri ya wilaya Kalambo mkoani Rukwa Shafii Mpenda Na Israel Mwaisaka,Rukwa Jeshi la polisi Mkoani Rukwa linamshikilia Timoth Ngambeki ambae ni mtumishi wa Halmashauri ya Kalambo kwa tuhuma za kutumia mashine bandia na kutoa risiti feki kwa wananchi na kuisababishia serikali hasara ya shilling million thelathini na tisa na laki tano. Mapema leo akizungumza ofisini kwake mkurugenzi mtendaji Halmashauri ya Kalambo Shafi Mpenda alisema mtumishi huyo aligundulika kufanya kitendo hicho baada ya kushindwa kuwasilisha fedha Benk na kwamba baada ya ufuatiliaji zaidi kwenye mageti ya ukusanyaji mapato aligundua uwepo wa udanganyifu kwenye utoaji wa risiti. ‘’baada ya kugundua uwepo wa udanganyifu kwenye swala la ukusanyaji mapato nilianzisha utaratibu wa kuweka madaftari ya kusaini kwenye mageti yote yanayo unganisha halmanshauri za jirani na kuweka watu ambao walikuwa wakifanya kazi ya kupiga picha risiti za ushuru kisha kunitumia na wakati mwingine nilikuwa nikiamka ...

KAYOGOLO MAKAMU MWENYEKITI MPYA HALMASHAURIYA WILAYA NKASI

Image
Na Israel Mwaisaka,Nkasi BARAZA la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa limemchagua Stephen Kayogolo kuwa Makamu Mwenyekiti wa halmashauri hiyo ambaye ataongoza kwa kipindi cha mwaka mmoja. Akitangaza matokeo hayo leo Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya Nkasi Pankrasi Maliyatabu amesema kuwa kwa mujibu sheria Makamu Mwenyekiti huchaguliwa kila baada ya mwaka mmoja. Amesema kuwa jumla ya kura 34 zimepigwa kati ya hizo kura za ndiyo ni ni 31 zilizoharibika ni 3 na nyingine zote ni za ndiyo . Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti huyo wa Halmashauri hiyo aliyechaguliwa,Diwani wa Kata ya Isale , Stephen Kayogolo amesema kwa nafasi aliyopewa na kuaminiwa ameomba waendelee kumshauri na kumtumia kwa maslahi mapana ya halmashauri na kuwa sehemu nzuri ya kumshauri Mwenyekiti wao Pankras Maliyatabu. “Nitaendelea kujenga mshikamano na umoja baina yetu Madiwani, ofisi ya Mkuu wa Wilaya pamoja na viongozi wote ngazi ya halmashauri, mimi ni binadamu kwa nafasi ambayo mmeniamini nao...

TBS YAWAONYA WANAOFOJI NEMBO YAO

Image
Israel Mwaisaka,Rukwa Shirika la viwango Tanzania TBS limesema halitasita kuwachukulia hatua kali za kisheria ikiwemo kuwapiga faini ya shilling million 20 wajasiliamali na wasindikaji watakao bainika kufoji nembo ya TBS pamoja na kuingiza sokoni bidhaa zisizokuwa na ubora. Hayo yamebainishwa na kaimu meneja wa shirika la viwango Tanzania Tbs kanda ya Magharibi Rodney Alananga wakati akitoa elimu kwa wajasiliamali, wasindikaji na wamiliki wa viwanda na kufanyika katika ofisi za kata ya Matai wilayani Kalambo mkoani Rukwa,Ambapo aliwataka waandaji wa bidhaa kuzingatia weledi na viwango na ubora wakati wa uandaaji wa bidhaa kabla ya kuingizwa sokoni. ‘’Tbs inazo skimu mbalimbali za udhibiti ubora ikiwemo skimu ya alama ya ubora,mzalishaji ambaye bidhaa yake imethibitishwa ubora kwa kuzingatia kiwango cha kitaifa cha bidhaa husika hupewa leseni ya kutumia alama ya TBS katika bidhaa hiyo hivyo kwa mwaka 2024 mzalishaji yeyote ambaye atashindwa kuwa na alama hiyo kwenye bidhaa yake atazuili...

WATUMISHI WA HALMASHAURI YA MPIMBWE WAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA TUHUMA ZA WIZI WA BILIONI 1.2

Image
Na Walter Mguluchuma,Katavi Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na  Rushwa  Mkoa wa Katavi imewafikisha   Mahakamani watumishi  saba wa Halmashauri ya  Wilaya ya  Mpimbwe  Mkoani  Katavi  akiwemo  mtunza  hazina wa Halmashauri hiyo kwa kutuma za wizi wa zaidi ya  shilingi Bilioni 1.2 walizokuwa wakiziingiza kwenye  akaunti za watu binafsi . Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na  Rushwa  Mkoa wa Katavi imewafikisha   Mahakamani watumishi  saba wa Halmashauri ya  Wilaya ya  Mpibwe Mkoani  Katavi  akiwemo  mtunza  hazina wa Halmashauri hiyo kwa kutuma za wizi wa zaidi ya  shilingi Bilioni 1.2 walizokuwa wakiziingiza kwenye  akaunti za watu binafsi . Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Katavi  Faustine  Maijo  amewataja watuhumiwa hao waliofikishwa  Kizimbani na  Takukuru Mkoa wa Katavi kuwa ni  Canuthe Matsindiko, Michael Katanga(Big),Masami  Mashauri ambae  ni mweka   hazina wa  Halmashauri hiyo(DT) Tumaini  Misese,Maila  Oluomba , Emanuel  Salanga  na  Laurent  Sunga. Maijo  alisema  watuhumiwa hao wamefik...

UWT NKASI WAZINDUA MFUKO WA UWEZESHAJI WANSWAKE KIUCHUMI

Image
Na Israel Mwaisaka,Nkasi JUMUIA ya Wanawake (UWT) ya CCM wilaya Nkasi mkoani Rukwa kupitia kikundi cha TUPENDANE umezindua mfuko wa pamoja utakaowawezesha wajasiliamali wadogo wenye lengo la kujikwamua kiuchumi kukopa na kupata mitaji ya kuendesha shughuli zao za kiuchumi. Uzinduzi wa mfuko huo ni kwenda sambamba na kauli ya Mwenyekiti wa CCM taifa na Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dkt,Samia Suluhu Hassan ya "siasa ni uchumi na uchumi ni siasa" katika mpango mathubuti wa Wanawake kujikomboa kiuchumi na kisiasa Akizindua mfuko huo mwenyekiti wa CCM wilaya ya Nkasi Keissy Aljabri Sudi aliwapongeza Wanawake hao kuubuni mfuko huo na kuwa lengo la CCM na serikali yake ni kutaka makundi mbalimbali ya kijamii yanajikwamua kiuchumi ikiwemo kundi kubwa la Wanawake. Amesema kuwa maendeleo ni mchakato na wengi ukosa mitaji kujiendeleza na kuwataka sasa kuutumia mfuko huo kukopa na kujiendeleza kiuchumi ikiwa ni pamoja na kujakikisha kuwa unakua endelevu hasa kwa kurejesha miko...

Kisangai achaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti Mbarali

Image
BARAZA la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya limemchagua Jeremiah Kisangai kuwa Makamu Mwenyekiti wa halmashauri hiyo ambaye ataongoza kwa kipindi cha mwaka mmoja. Akitangaza matokeo hayo leo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali, Raphael Shitindi amesema kuwa kwa mujibu sheria Makamu Mwenyekiti huchaguliwa kila baada ya mwaka mmoja. Diwani wa Kata ya Miyomboni,Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali, Jeremiah Kisangai Amesema kuwa jumla ya kura 21 zimepingwa kati ya hizo kura za ndiyo ni 19 iliyoharibika ni moja na hapana moja kwa maana hiyo Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali ni Jeremiah Kisangai ambaye ataongoza halmashauri hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja. Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti huyo wa Halmashauri hiyo aliyechaguliwa,Diwani wa Kata ya Miyomboni , Jeremiah Kisangai amesema l kwa nafasi aliyopewa na kuaminiwa ameomba waendelee kumshauri na kumtumia kwa maslahi mapana ya halmashauri na kuwa sehemu ...
Image
Na Israel Mwaisaka,Nkasi JUMUIA ya Wanawake (UWT) ya CCM wilaya Nkasi mkoani Rukwa kupitia kikundi cha TUPENDANE umezindua mfuko wa pamoja utakaowawezesha wajasiliamali wadogo wenye lengo la kujikwamua kiuchumi kukopa na kupata mitaji ya kuendesha shughuli zao za kiuchumi. Uzinduzi wa mfuko huo ni kwenda sambamba na kauli ya Mwenyekiti wa CCM taifa na Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dkt,Samia Suluhu Hassan ya "siasa ni uchumi na uchumi ni siasa" katika mpango mathubuti wa Wanawake kujikomboa kiuchumi na kisiasa Akizindua mfuko huo mwenyekiti wa CCM wilaya ya Nkasi Keissy Aljabri Sudi aliwapongeza Wanawake hao kuubuni mfuko huo na kuwa lengo la CCM na serikali yake ni kutaka makundi mbalimbali ya kijamii yanajikwamua kiuchumi ikiwemo kundi kubwa la Wanawake. Amesema kuwa maendeleo ni mchakato na wengi ukosa mitaji kujiendeleza na kuwataka sasa kuutumia mfuko huo kukopa na kujiendeleza kiuchumi ikiwa ni pamoja na kujakikisha kuwa unakua endelevu hasa kwa kurejesha miko...

BARAZA LA MAASKOFU ( TEC)

BARAZA LA MAASKOFU (TEC): Tunasisitiza kwamba SAUTI YA WATU NI SAUTI YA MUNGU, hivyo basi kuwasikiliza Wananchi na kufanya Maamuzi kadiri wanavyotaka kutailetea Serikali Heshima kubwa ya kuwa sikivu kwa Watu Kinyume cha haya, Mwenyezi Mungu anatuonya kupitia Nabii Yeremia anaposema: "Kama kapu lililojaa Ndege walionaswa, ndivyo Nyumba zao zilivyojaa Maili za udanganyifu. Ndio maana wamekuwa Watu wakubwa na Matajiri, wamenenepa na kunawiri katika kutenda maovu hawana kikomo hawahukumu yatima kwa Haki, wapate kufanikiwa, wala hawatetei Haki za Masikini" (Yeremia 5:27-28) #JamiiForums #Governance #FreeSpeech #DPWorldSaga #TamkolaTEC
Image
Wananchi Katavi Kunufaika na Elimu ya Ujasiriamali 16 August 2023, 7:16 am Wananchi Mkoani Katavi waanza kunufaika na mafunzo ya Ujasiriamali yanayoendeshwa na Mpanda Radio FM kwa kushirikiana na Mkwawa Vocational Training Center, Mafunzo hayo yatatolewa Kwa siku tatu kuanzia August 15 Hadi August 17.

DKT. KIRUSWA AITAKA KAMPUNI YA UCHIMBAJI MAKAA YA MAWE KUCHANGIA HUDUMA KWA JAMII RUKWA

Image
Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa ameitaka Kampuni ya uchimbaji wa Kati wa Makaa ya Mawe ya Edenville Tanzania Limited kuchangia huduma kwa jamii inayozunguka eneo la shughuli za uchimbaji wa madini hayo kama Kanuni chini ya Kifungu namba 129 cha Sheria ya Madini kinavyoelekeza. Hayo, ameyasema wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Pande Kijiji cha Komolo wilayani Nkasi mkoa wa Rukwa kwenye mkutano wa hadhara ambapo amesisitiza kampuni hiyo kuwasilisha Mpango wa Wajibu wa Mmiliki wa Leseni ya Madini kwa Jamii inayozunguka Mgodi. "Naomba mkutane na Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi ili kupata vipaumbele vya eneo husika ili mjue mnatakiwa kuchangia katika maeneo gani, uchangiaji huo sio ombi bali ni takwa la kisheria kwa mmiliki wa leseni kuchangia huduma za kijamii inayozunguka mgodi", amesema Dkt. Kiruswa. Aidha, Dkt. Kiruswa ameliagiza Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kuitembelea Kampuni ya Edenville Tanzania Limited ili kuona namna bora ya kushirikiana nayo kw...

Masomo yaongezeka mtaala mpya msingi

Image
TAASISI ya Elimu Tanzania imetoa mtaala wa elimu ya msingi kuanzia darasa la kwanza hadi la saba 2023. Muundo wa mtaala huo umebadilika na sasa elimu hiyo itakuwa ni ya miaka sita badala ya saba kama ulivyokuwa Mtaala wa Elimu ya Msingi wa mwaka 2016. Mtaala huo umezingatia nadharia za ukuaji na ujifunzaji na falsafa ya elimu ya kujitegemea inayosisitiza elimu inayomwezesha Mtanzania ajitegemee na amudu maisha yake ya kila siku. Muundo wa mtaala unaonesha elimu ya msingi itatolewa kwa miaka sita katika hatua mbili ambazo ni darasa la kwanza na la pili ili kujenga umahiri katika stadi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK). Katika hatua ya pili inaonesha mtaala huo utaanzia darasa la tatu hadi la sita na italenga kuimarisha stadi za KKK na stadi nyingine za maisha. Mwanafunzi wa shule ya msingi anatakiwa aanze darasa la kwanza akiwa na umri wa miaka sita na kumaliza darasa la sita akiwa na umri wa miaka 11. Kwa mujibu wa mtaala huo mwaka wa masomo utakuwa na siku 194 sawa na wiki 39 na u...

Mbaroni kwa kuua mke, shemeji

Image
TANGA; JESHİ la Polisi Mkoa wa Tanga limefanikiwa kumkamata Swalehe Miraji Ally, mwenye umri wa miaka 38 aliyekuwa kakimbilia mkoani Tabora baada ya kufanya mauaji ya mkewe na shemeji yake kwa kuwakata na mapanga mara mbili kichwani wakati wakiwa shambani. Kamanda wa  Polisi Mkoa wa Tanga, Almachius Mchunguzi amesema kuwa mtuhumiwa huyo ambaye ni fundi ujenzi mkazi wa Mkanyageni wilayani Muheza, alimuua mkewe Mwanahawa Hassan (24) na Sauda Sufian (20) kisha kukimbilia Tabora, ambapo jitihada za Polisi zilifanikiwa kumkamata. Katika tukio linguine polisi imemkamata mkazi wa Handeni, Rajab Athuman mwenye umri wa miaka 32 akituhumiwa kumuua kwa kumkata kichwa kwa kutumia kamba ya katani Helena Sila.

‘Kuweni na subira ripoti takwimu hali ya ulemavu ‘

Image
OFISI ya Taifa ya Takwimu imewataka wadau wanaohitaji ripoti za takwimu za hali ya ulemavu nchini  baada ya matokeo ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 kuwa na uvumilivu kwani bado taarifa zake zinaandaliwa. Hayo yamesemwa na Meneja wa Takwimu Mkoa wa Tanga Toni Mwanjota kwa niaba ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali  Albina Chuwa, wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya matokeo ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 Kwa viongozi,watendaji na watu wa makundi maalum mkoani Tanga. Amesema kuwa matokeo ya ripoti hiyo yamekuwa yakisubiriwa kwa hamu kubwa na wadau mbalimbali ,Ili kujua hali halisi ya kundi hilo kwa sasa hapa nchini. “Taarifa za watu wenye ulemavu ni ripoti ambayo inaandaliwa hivyo tunaomba subira kutoka kwa wadau wote wa takwimu za hali za watu wenye ulemavu,”amesema Mwanjota. Amesema kuwa  ofisi ya takwimu inaelewa umuhimu wa ripoti hiyo ndio maana imo katika orodha ya taarifa ambazo zinaandaliwa kama ambavyo zilizotangulia hapo awali.

Wabunge Uganda waja kujifunza sheria ya ndoa

Image
WABUNGE kutoka nchini Uganda wapo nchini kwa ajili ya kujifunza namna sheria ya ndoa inavyotekelezwa hapa nchini, changamoto zilizopo kwa sasa na namna wanavyojipanga kuzitatua. Mwenyekiti wa Chama cha Wabunge Wanawake nchini Uganda, Sara Opendi amesema hayo baada ya kukutana na Menejimenti ya Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzamia ( LRCT). Opendi amesema wamekuja kujifunza eneo hilo kwa sababu kwa serikali ya Uganda ipo kwenye mchakato wa kuandaa muswada wa sheria ya ndoa, hivyo wapo Tanzania kwa ajili ya kupata uzoefu kutoka nchi mbalimbali zinazotekeleza sheria hiyo ikiwemo Tanzania na Zimbabwe. “Uganda kuna ndoa za aina nyingi ambapo muswada huo unategemewa kugusa jamii yote huku kama ambavyo Tanzania ilivyofanya kwa kuzingatia ndoa za kidini, ndoa za kimila na ndoa za serikali,” amesema. Akielezea uzoefu kuhusu sheria ya ndoa, Katibu Mtendaji Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania. Griffin Mwakapeje amesema tume inatambua ndoa kama taasisi ambayo haina budi kulindwa kwa lengo la kuwa na...

Wananchi Dar kupimwa magonjwa ya moyo

Image
TAASISI ya Moyo ya Jakaya Kikwete na Hospitali ya Dar Group wanatarajia kufanya kambi maalum ya upimaji na matibabu ya magonjwa ya moyo kwa wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam na mikoa ya jirani – Taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano, Anna Nkinda imesema upimaji huo utafanyika kwa watoto na watu wazima kuanzia Septemba 02, 2023 hadi Septemba 03,2023 kuanznia saa mbili asubuhi  hadi saa 10 alasiri jioni katika Hospitali ya Dar group iliyopo Temeke . “Aidha katika kambi hii kutakuwa na wataalamu wa lishe ambao watatoa elimu ya lishe bora, ambayo itawapa wananchi uelewa na kufuata mtindo bora wa maisha na kuepukana na magonjwa yasiyoambukizwa yakiwemo ya moyo, ambayo yanaweza kuepukika kwa kufuata ushauri wa kitaalamu,”ameeleza Nkinda. Amewaomba wananchi kujitokeza kwa wingi kupima afya zao kujua kama wana matatizo ya moyo, ili kuanza matibabu mapema kwa atakayegundulika kuwa na magonjwa na kusisitiza kuwa huduma hiyo itakuwa ya kuchangia gharama ya matibabu. “...

TASAC yaboresha kanuni kuongeza ufanisi

Image
SHIRIKA la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), limesikia kilio cha wadau wa sekta ya usafiri kwa njia ya maji kwa kuboresha kanuni mbalimbali ambazo zimekuwa ni kikwazo katika utendaji wao wa kila siku. Akizungumza kwa niaba ya wadau hao wa sekta ya usafiri kwa njia ya maji, Rais wa Chama cha Mawakala wa Forodha Tanzania (TAFFA), Edward Urio amesema maboresho yaliyofanyika yamegusa maeneo yaliyokuwa na utata mwingi katika utendaji wao. Amesema upande wa mawakala wa forodha walikuwa na utata katika ule muda wa kontena linaposhuka bandarini na linapofika kwenye bandari kavu, ambako kulikuwa na upotevu wa siku mbili au tatu kwa kuhoji jambo hilo lilipaswa kubebwa na nani jambo ambalo kanuni hizo zimekuja na majibu yake. “Lakini kuna suala moja kubwa kama unaagiza mzigo kwa kupitia bandari hasa mzigo wa makasha, kuna utaratibu ambao unatakiwa uweke dhamana ya kuweza kuaminiwa na wale mawakala wa meli uweze kulichukua lile kisha ukapakue mzigo wako. “Kama ni hapa Dar es Salaam, kama ni Morogo...

WATUMISHI MADINI WATEMBELEA MGODI WA BULYANHULU

Image
  #Katibu Mkuu Madini aanza Utekelezaji Maazimio Timu ya Watumishi wapatao 13 kutoka kada mbalimbali za Wizara ya Madini ikihusisha Makatibu Mahususi, Watunza Kumbukumbu na Wahudumu wametembelea Mgodi wa Barrick - Bulyanhulu uliopo Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga. Ziara hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa maazimio na ahadi alizotoa Katibu Mkuu Wizara ya Madini Kheri Mahimbali wakati wa kikao cha Baraza la Wafanyakazi la Wizara hiyo lililofanyika mwezi Mei, 2023, jijini Dodoma. Aidha, ziara hiyo inalenga kuwajengea uelewa wa pamoja watumishi wote wa Wizara kuhusu shughuli zinazofanywa katika Sekta ya Madini hususan shughuli za uchimbaji wa madini katika migodi mikubwa, ya kati na midogo ili kuwezesha malengo mahususi ya wizara kutekelezwa kwa pamoja kama familia moja ya Madini. Watumishi hao wamepata fursa ya kutembelea maeneo mbalimbali katika mgodi huo ikiwemo mgodi wa chini ( underground mining), sehemu ya uchenjuaji (processing plant) bwawa la huifadhi tope sumu ( TSF) , sehemu ya up...

Ugonjwa wa Kipindupindu Watokea Nkasi Mkoani Rukwa

Image
  UGONJWA wa Kipindupindu umeibuka wilayani Nkasi mkoani Rukwa ambapo wagonjwa 37 wameripotiwa katika kijiji cha forodhani kata ya Korongwe. Akitoa taarifa kwenye kikao cha dharura cha kamati ya afya ya msingi mganga mkuu wa wilaya Nkasi Benjamini Chota alisema kuwa taarifa za kwanza za kuwepo kwa wagonjwa wa kipindupindu zililipotiwa Desemba 2 mwaka huu ambapo wagonjwa watatu walilipotiwa kuwapo katika zahanati ya Korongwe. Alisema kuwa baada ya taarifa hiyo timu afya ya wilaya kwa kushirikiana na timu ya mkoa walielekeza nguvu katika kijiji hicho na baada ya kuchukua sampuli na kuzipima ilibainika kuwa ni ugonjwa wa kipindupindu ndipo walipoanza kuchukua hatua mara moja za kukabiliana na ugonjwa huo. Alidai kuwa waliweka kambi kwa ajili ya wagonjwa wa kipindupindu na kuwa hadi sasa wagonjwa waliolipotiwa na kupata matibabu ni 37 ambapo walioruhusiwa kurudi nyumbani ni 25 na waliopo hodini wakiendelea kupata matibabu ni 12 lakini hadi sasa hakuna kifo kilichoripotiwa kutokana na ugonj...