WANANCHI WAIPA 5 SERIKALI YA AWAMU YA 6 KUFANIKISHA KUSAMBAZA UMEME VIJIJI VYOTE.




Na Ibrahim Yassin,Songwe

MPANGO wa serikali kuhakikisha vijiji vyote vinapatiwa umeme umetimizwa baada ya wananchi kumueleza katibu tawala mkoani Songwe alipokuwa wilayani Songwe.

Awamu za nyumba hali ya upatikanaji wa umeme ulikuwa ni ndoto lakini mkakati ulianzia awamu ya 5 chini ya Hayati John Magufuli na ilipofika awamu 6 chini ya Rais Samia Suluhu tayari vijiji vyote vimepatiwa umeme.



Wananchi hao walimueleza Katibu tawala alipotembelea miradi wilayani Songwe kuwa awapelekee salam kwa Rais Samia kutatua kero ya umeme wakisema watamlipa kura za ndiyo katika uchaguzi mkuu ujao.

Mariet Mwashilindi mkazi wa Songwe alisema ana kila sababu kuipongeza serikali kwa kutimiza ahadi yake ya kila kijiji kuwa na umeme hivyo aliomba ahadi hiyo itimizwe ngazi ya vitongoji ili wananchi wajiinue kiuchumi.



Sharif Mtambo mkazi wa kata ya magamba,alisema alisema kuna vitongoji kadhaa havina umeme aliomba watimiziwe ili waanze kufunga mashine za kusaga nafaka na salooni ili waingize kipato na kuuboresha mji.

''Serikali imefanya kazi kubwa mno,niwapongeze pia Tanesco wakiongoz wa na meneja Michaek Kidoto,walikuwa hawalali walipita vijiji vyote kusimamia ufungwaji wa umeme na sasa tumeanza kupata manufaa.
Meneja wa shirika la umeme (Tanesco ) wilayani Songwe Michael Kidoto,alisema ni kweli serikali iliahidi kila kijiji nchini kuwa na umeme na tayari imetimiza ,katika wilaya ya Songwe vijiji vyote vina umeme.



Alisema katika wilaya yote vijiji vimewekewa umeme ila Songwe kuna vitongoji 161 kati ya hivyo vitongoji 20 havina umeme ila vipo kwenye mpango wa bajeti ya 2025/26 hivyo wananchi wawe na utulivu kwani serikali yao sikivu itatimiza ahadi hiyo.

Sekta ya umeme ni moja ya sekta muhimu kwa mustakabari wa maisha ya watu,kwani endapo wanavitongoji watawashiwa umeme watakuza vipato vyao kwa kufungua viwanda vidogo,saloon,mashinde za kunyoa na za kusaga.




Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa