KASI YA KATAZO LA UHARIBIFU WA MAZINGIRA KWENYE VYANZO VYA MAJI UONGEZEKE.


MAKALA



---TUTUNZE MAZINGIRA NA KUACHA KUKATA MITI YA ASILI KWENYE VYANZO VYA MAJI KULINDA UOTO WA ASILI NA KUSABABISHA UKAME---

Na Ibrahim Yassin,Songwe

‘’Lengo ni kufikia asilimia 90 kutoka 83 iliyopo,kuna mradi wa Bilioni 119 uliosainiwa na Waziri wa fedha na waziri wa maji chanzi ni mto Momba,wakazi wa majimbo ya Tunduma,Momba,Mbozi na Mlowo watanufaika’’

 UKAME na uhaba wa mazi unatokana na uwepo wa uharibifu wa mazingira kwenye vyanzo vya maji vinavyofanywa na baadhi ya watu kufanya shughuri za kibinadamu kwenye vyanzo hivyo kwa kulima,kukata miti ama kuingiza mifugo.



Maji ni muhimu kwa viumbe vyote duniani, bila maji hakuna uhai,aidha maji ni muhimu kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii, Kiwango cha maendeleo ya jamii yoyote kinategemea kuwepo kwa maji ya kutosha na yenye ubora unaotakiwa.

 Katika hali yake ya asili, maji ni sehemu ya mazingira ambapo wingi na ubora wake ndio unaosaidia katika kuamua jinsi maji yatakavyotumika. Upatikanaji wa maji safi na salama kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na usafi wa mazingira ni muhimu katika kulinda afya za wananchi.


Utumiaji wa maji ambayo sio salama na uhaba wa maji huchangia katika kusababisha milipuko na kuenea kwa magonjwa kama kuhara na kipindupindu. Japokuwa maji ni muhimu kwa uhai wa viumbe, na maendeleo ya kijamii na kiuchumi, hakuna uwiano wa mgawanyo wa maji ulio sawa kati ya sehemu moja na nyingine na katika majira mbalimbali ya mwaka. 

Aidha, wingi wa maji yanayofaa kwa matumizi mbalimbali ya kijamii na kiuchumi una kikomo, na maji hayo pia yanaweza kuathirika kirahisi
Ipo kauli isemayo maji ni uhai,na ni kweli bila maji hakuna uhai,ili kauli hiyo itimizwe ni lazima ongezeko la katazo la uharibifu wa mazingira kwenye vyanzo vya maji iongezwe ili fedha za serikali zisipotee na watu wanufaike na miradi.



Kutokana na umuhimu huo wa maji,serikali mbali na Kutoa fedha nyingi kujenga miradi ya maji inayogusa jamii lakini bado baadhi ya maeneo kuna uhaba wa maji,kwa kuliona hilo serikali iliamua kutenga fedha kujenga visima 900 nchi nzima.

Lengo la Kutoa fedha hizo za kujenga visima 900 kila jimbo limejengewa visima vitano katika maeneo yenye uhitaji ili kupunguza kasi ya uhaba wa maji licha ya kuwa baadhi ya maeneo kumekuwa na uharibifu mkubwa kwenye vyanzo.

Mkoa wa Songwe ni moja ya wanufaika wa vizsima hivyo ambapo kila jimbo tayari wananchi wake wameanza kunufaika na siku za hivi karibuni meneja wa Ruwasa mkoa alitoa katazo kwa watu kuilinda miundombinu kwa kulinda mazingira kwenye vyanzo.

Akizungumzia hali hiyo mwishoni mwa wiki,Meneja wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira (RUWASA) mkoani Songwe Mhandisi Charles Pambe,anasema mkaoa wa Songwe ni mnufaika wa program hiyo ya visima na kila kisima kinagharimu Tsh,Milioni 60.

Anasema serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt,Samia Suluhu,imefanya kazi kubwa ya kumtua mwanamke ndoo kichwani,kwa kujenga miradi mikubwa inayogusa jamii karibu kila kata na kujenga miradi mikubwa ya fedha nyingi kuhakikisha tatizo la maji Songwe linabaki historia.

‘’Licha ya ujenzi wa visima vitano kila jimbo,pia kuna mradi mkubwa wa maji wa Msangano,Naming’ng’o wa Bilioni 6.132 unaendelea ,mradi utakalohudumia wakazi wa kata nne na maeneo Jirani,ombi langu ni wananchi wawe walinzi kukemea wanaoharibu vyanzo na miundombinu ya maji’’anasema Pambe.



Anasema lengo la mkoa ni kufikia asilimia 90 za upatikanaji wa maji ambapo kwa sasa wapo asilimia 83 ambapo kabla ya Rais Dkt,Samia kuingia madarakani kulikuwa na asilimia 56 na sasa baada ya kuwa madarakani amepandisha na kuwa asilimia 83.

Mhandisi Pambe anasema ukuondoa mikakati hiyo ya kufikisha asilimia 90 kuna mradi mkubwa wa maji unajengwa utakaogharimu Tsh,Bilioni 119 ambapo Waziri wa fedha na Waziri wa maji walisaini mkataba huo,utakaonufaisha wakazi wa majimbo ya Tunduma,Momba,Vwawa na Mlowo chanzo ni mto Momba.

Anasema mbali na mradi huo mkubwa,pia kuna mradi wa Itumba -Isongole kule wilayani Ileje wa Tsh,Bilion 4.6 ambao upo asilimia 85,na upo pia mradi wa Milioni 800 unajengwa kata ya Nanyara wilayani Mbozi miradi itakayowakomboa wananchi na taasisi zilizopo.

Anasema ili kufikia malengo haya na kuilinda fedha kubwa inayotolewa na serikali isipotee nguvu kubwa ya katazo la kulinda mazingira hasa kwenye vyanzo vya maji kulinda uoto wa asili,watu waache kulima na kuchungia mifugo kwenye vyanzo vya maji.

Hata hivyo mwishoni mwa wiki katibu tawala mkoani Songwe Happiness Seneda,alifanya ziara ya kutembelea na kukagua ujenzi wa miradi iliyokamilika na inayoendelea katika majimbo yote Matano ambapo alisifu utekelezaji wa miradi yam aji jinsi ilivyojengwa vizuri.



Katika taarifa zake Ras Seneda alimsifu Rais Dkt,Samia Suluhu kwa kuuheshimisha mkoa huku meneja wa mamlaka ya Maji Mhandisi Charles Pambe na timu yake wakitajwa kuisimamia vyema miradi hiyo iliyojengwa kwa ubora wa hari ya juu na nidhamu ya matumizi.

Pia Ras Seneda alipigilia msumali kwa kuwataka wananchi kuilinda miradi hiyo,ili iendelee kuwepo waitumie wao na vizaji vijavyo na kusisitiza kulipia bili za maji ili fedha hizo ziweze kukarabati miundombinu pindi itakapo haribika.

‘’Ndoo moja ya lita 20 nimeambiwa mnalipia Tsh,40,fedha hizo zinakusanywa na jumuiya ya watumia maji mliowachagua wenyewe na zinatunzwa benki,hakikisheni fedha hizo haziliwi kazi yake ni kuikarabati miundombinu pindi itakapo haribika’’Alinukuliwa Seneda.

Aidha katibu huyo tawala aliyeongozana na timu ya wataalam na wakuu wa idara kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa,alisisitiza wananchi kuendelea kuitunza miundombinu na vyanzo vya maji akichukizwa na tukio la moja ya kata wilayani Mbozi ambapo baadhi ya watu wamekata bomba maji wameelekeza kwenye mashamba ya Kahawa.

Chukizo hilo la Katibu tawala lilitiliwa mkazo akitaka mtu atakayepatikana anaharibu miundombinu mbali na kutozwa faini apelekwe pia mahakamani ili afungwe iwe fundisho kwa wengine,kwani seriikali inaumiza kichwa kutafuta fedha ni lazima miradi ilindwe.

Ipo haja wananchi kuziishi kauli hizi za viongozi kuilinda miundombinu ya miradi iliyopo hasa yam aji kwa kutolima ama kufanya shughuri zozote kwenye vyanzo vya maji kwa kufanya hivyo miradi itakuwa endelevu.

Mwisho……Mwandishi wa Habari hizi anapatikana kwa simu,,,0718382817—0766936392 barua pepe yassin.ibrahimu@yahoo.com

picha ,,1 ,Katibu tawala mkoani songwe Happines Seneda akizungumza na watendaji wake katika hitimisho la ziara yake akiisfu Ruwasa kwa kazi nzuri ya usimamizi wa miradi ya maji.



Picha namna 2 na zinazeonekana,katibu tawala mkoani Songwe Hapiness Seneda akizungumza mara ya kukagua moja ya miradi ya maji,aliyevaa kofia ni meneja wa Ruwasa mkoa Charles Pambe akizikiliza kwa makini maelekezo ya bosi wake..pichazote na Ibrahim Yassin,

Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa