Posts

Showing posts from December, 2025

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa

Image
Na Israel Mwaisaka,Nkasi ‎ ‎Mwanamke aliyefahamika kwa jina la Joyce Baton Mwasumbi mkazi wa Kijiji Cha Kanazi wilayani Nkasi amefariki dunia baada ya kujinyonga kwa kutumia kanga chumbani kwake. ‎ ‎Akizungumzia tukio hilo Mwenyekiti wa Kijiji Cha Kanazi Rudis Ulaya amesema kuwa tukio la Mwanamke huyo ambaye ni mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT kujinyonga limetokea leo Jumatano Disemba 24,2025 majira ya saa 2 asubuhi baada ya Mumewe ambaye ni mchungaji kwenda kanisani kupalilia pembeni mwa jengo la kanisa hilo. ‎ ‎Amesema kuwa wakati Mumewe ambaye ni Mchungaji akiendelea na jukumu lake kanisani mkewe aliutumia mwanya huo kujitundika kwa kutumia kitenge na muda mfupi Mumewe aliingia chumbani huko na kumkuta Mkewe akiwa amejitundika juu huku akitapatapa kufa ndipo alipochukua kisu na kukikata kitenge hicho kwa lengo la kuokoa uhai wake lakini muda mfupi alipoteza maisha ‎ ‎Mwenyekiti huyo wa Kijiji amefafanua kuwa baada ya yeye kumhoji Mume wa marehemu Mchungaji Ibrahimu Mwaipopo alid...

Serikali kuanzisha kitengo maalumu cha kusikiliza kero za Wananchi na makundi mengine ya kijamii

Image
Na. Israel Mwaisaka, Rukwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano Mhe. Deus Sangu amesema Serikali itaanzisha kitengo maalum cha huduma kitakachofanya kazi kwa saa 24 chenye jukumu la kupokea, kusikiliza na kufanyia kazi maoni, mapendekezo pamoja na kero za wananchi. Kitengo hicho kitawezesha wananchi kuwasilisha changamoto zao moja kwa moja bila vikwazo vya kiurasimu na kusaidia Serikali kupata mrejesho wa haraka kwa ajili ya kuboresha sera na huduma. Sangu amebainisha hayo jana, Disemba 23, 2025 Sumbawanga Mkoani Rukwa alipofanya kikao na wadau wa Mahusiano kutoka makundi ya Kijamii, Kisiasa, Kiuchumi na wawakilishi wa kundi la Vijana. Aidha, amesisitiza umuhimu wa mawasiliano na uwajibikaji kati ya Serikali na wananchi kwa ajili ya kuimarisha imani, mshikamano wa kitaifa na maendeleo jumuishi. ‎Aidha, amesema lengo la kikao ni kutambulisha shughuli za Ofisi yake na kutekekeza mkakati wa kuwafikia wadau wa mahusiano ili kujenga uelewa wa pamoja kwa maendeleo ...

MADEREVA WA VYOMBO VYA MOTO NA WAMILIKI WAPEWA SOMO UTII WA SHERIA NA KANUNI KWENYE VYOMBO VYA MOTO

Image
WATAKIWA KUTOPANDISHA NAULI KUZIDISHA ABIRIA NYAKATI ZA SIKUKUU, WENYEWE WATAKA  SHERIA SHIRIKISHI. Na Ibrahim Yassin,Songwe IMEELEZWA kuwa vitendo vya kupandisha bei za nauli na kujaza abiria kupita kiasi katika magari yanayosafiri umbali mrefu umetajwa kuhatarisha usalama wa abiria uneopelekea uwepo wa ajali za mara kwa mara imebainika. Imekuwa ni kawaida kwa madereva wa vyombo vya moto siku za sikukuu wakizitumia kama fursa za kujipatia kipato kikubwa kwa kuvunja sheria kwa kupandisha nauli na kujaza abiria kupita kiasi bila kujari kuwa wanaweza kusababisha maafa. Miaka yote inapofika mwisho mwa mwaka katika sikukuu za Chrismas na mwaka mpya tumeshuhudia uwepo wa ajali za mara kwa mara zinazosababishwa na uzembe na tamaa ya madereva na makondakta. Maeneo mengi ya stendi za mabasi yaendayo mikoani hujumazimekuwa zikifanyika baada ya wakatisha tiketi kupandisha nauli baada ya uwepo wa abiria wengi wanaoenga mapumzikoni na hata shule zinapo funga. Mbali na hilo pia kumekuwa na uzembe w...

MADEREVA NA WAMILIKI WA PIKIPIKI NA BAJAJI WAHOJI SABABU YA WALIPISHA LESENI KUKAMATA NA KUTOZA FAINI VYOMBO VYAO.

Image
Na Ibrahim Yassin,Songwe MARUFUKU yatangazwa kwa wanaochukua tenda za kulipisha Leseni za bajaji na pikipiki kufanya msako wa kuwakamata wasiolipa Leseni na kuwatoza fedha zinazodaiwa kuwa ni Rushwa ikidaiwa hakuna sharia inayowaruhusu kufanya hivyo. Marufuku hiyo imetolewa hivi karibuni katika semina elekezi iliyotolewa na maafisa wa sharia wa Mamlaka ya udhibiti wa usafiri ardhini (LATRA) katika ukumbi wa jeshi la polisi uliopo mkoani Songwe ukihudhuriwa na wamiliki wa vyombo vya moto, madereva.makondakta na jeshi la polisi usalama barabarani. Katika kikao hicho mwenyekiti wa waendesha bodaboda mkoani Songwe Omary Mbuba ,amesema wanapongeza elimu iliyotolewa ya usalama barabarani lakini wanataka kujua sababu ya waliopewa tenda za kukamata pikipiki zisizo na Leseni na kusababisha ajali. Amesema waliopewa tenda za uwakala wa kukatisha Leseni wamekuwa wakivaa sale zenye nembo za LATRA na kukimbizana na waendesha pikipiki na bajali kufanya ukaguzi na kusababisha ajali hali ya kuwa sharia...

MADEREVA NA WAMILIKI WA VYOMBO VYA MOTO WATAJA CHANGAMOTO ZA FAINI WAKIPIGWA MSASA NA LATRA

Image
Na Ibrahim Yassin,Songwe Madereva wa vyombo vya moto wametakiwa kuheshimu sheria za barabarani kwa kutozidisha abiria ikiwemo utoaji wa tiketi kwa abiria ili kuepuka kulipishwa faini zisizokuwa na tija na kuhatarisha usalama wa abiria. Imekuwa ni kawaida kwa madereva na makondakta hasa nyakati za sikukuu kuvunja sheria kwa tamaa ya kupata fedha nyingi kwa kujaza abiria kupita kiasi licha ya kuwa sharia inawataka wapakie kulingana na idadi ya viti. Kauli hiyo imetolewa leo Disemba 19/ 2025 na mkaguzi wa polisi ofisi ya mkuu wa usalama barabarani wilayani Mbozi mkoani Songwe Anthony Sabasaba katika mafunzo siku moja yaliyofanyika kwenye ukumbi wa jeshi la polisi mkoani Songwe chini ya maafisa sharia kutola Latra makao makuu. Amsema wamekuwa wakifanya ukaguzi wa mara kwa mara na kukuta makosa yanayojirudia ikiwemo makondakta kuto toa tiketi,kujaza abiria kupita kiasi na baadhi ya madereva wakibainika Leseni zao kuisha muda wake. Amesema maafisa wa Mamlaka ya udhibiti wa usafiri aridhini (...

Wananchi watakiwa kushiriki miradi ya maendeleo

Image
Na Asha Hassan,Nkasi ‎ ‎Vongozi wa kata ya Isale Halmashauri ya wilaya ya Nkasi Mkoani Rukwa akiwemo Diwani wametakiwa kwenda kuwahamasisha wakazi wa kijiji cha Mtapenda kata ya Isale kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa mradi wa vyoo wa SWASH unaotekelezwa katika Shule ya Msingi Kitete. ‎ ‎Wito huo umetolewa na Afisa Elimu Ufundi Optunatus Mussi kwa niaba ya Afisa Elimu Msingi katika kikao cha maendeleo ya kata kilichofanyika katika Ofisi ya Kata ya Isale mara baada ya kusomewa taarifa ya maendeleo ya mradi huo ambao utagharimu kiasi Cha Shilingi Milioni thelathini na nne sitini elfu miatisa na hamsini na moja na senti kumi na tatu. ‎ Aidha Mussi amewasisitiza kuwa wao kama viongozi wanatakiwa kutumia utashi na kukubalika kwao kwa wananchi kuendelea kuwasawishi wakazi hao kushiriki ujenzi wa mradi huo kwa nguvu zao kama Sheria ya mradi inavyosema, kwani serikali ina dhamira ya dhati ya kusogeza huduma ya Elimu kwa wananchi. Kwa upande wake Afisa Mipango kutoka Ofisi ya Mkurugenzi ...

SONGWE YA DKT.SAMIA YAJIVUNIA KUPAA SEKTA YA ELIMU,AFYA NA MAJI WATAKA MAFANIKIO ZAIDI AWAMU HII

Image
                                  MAKALA Na Ibrahim Yassin,Songwe RIPOTI MAALUM. WAKATI wananchi wa wilaya nne zilizopo mkoani Songwe wakijivunia mafanikio ya awamu ya 6 iliyopita katika sekta ya Elimu,Afya na Maji,wananchi hao wamejenga Imani ya kupata mafanikio zaidi katika awamu hii. Mkoa wa Songwe ulioanzishwa mwaka 2016 ukimegwa kutoka mkoa wa Mbeya na jina la mkoa limetokana na mto Songwe huku makao makuu yake yakiwa Vwawa wilayani Mbozi. Mkoa huu ukiwa nae neo lake la Kilometa 27,656 linapakana na nchi za Zambia na Malawi kwa upande wa kusini,Mji wa Tunduma ndiyo lango kuu la kuingilia nchini Zambia na Isongole Ileje ndiyo lango kuu la kuingilia nchini Malawi. Mikoa jirani na mkoa wa Songwe ni Rukwa na Katavi upande wa Magharibi,Tabora upande wa Kaskazini, na Mbeya upande wa Mashariki,Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi waliohesabiwa ni 1,035,214,na asilimia 80 ya wananchi wa mkoa huu hutegemea kilimo na ufugaji. MAFANIKIO SEKTA YA ELIMU. Wakati Rais Dkt,Samia anaingia madarakani ...

Wazee wamtwisha zigo la migogoro ya ardhi diwani wa Nkomolo

Image
Na Israel Mwaisaka,Nkasi ‎ ‎Wazee wa kata ya Nkomolo wilayani Nkasi wamemtaka diwani wa kata hiyo Sitivine Tontololo kuahakikisha analiangazia tatizo la migogoro ya ardhi ambalo limeendelea kuwa tatizo kubwa katika eneo Hilo. ‎ ‎Wamesema kuwa licha ya serikali na wadau wengine kufanya jitihada mbalimbali za kuondoa tatizo Hilo lakini bado tatizo la migogoro ya ardhi halijatafutiwa ufumbuzi. ‎ ‎Hayo yamezungumzwa leo na Wazee baada ya diwani huyo kuwakutanisha Wazee wa kata ya Nkomolo na kutaka wamueleze changamoto zilizopo kata ya Nkomolo ikiwa ni pamoja na kutizama vipaumbele atakavyoanza navyo kama diwani baada ya kuchaguliwa hivi karibuni ‎ ‎Mwenyekiti wa Wazee wa (CCM) wilaya Nkasi Permin Matumizi amemuomba diwani huyo kuanza na jambo hilo la migogoro ya ardhi ikiwa ni pamoja na kufuatilia fidia serikalini kwa watu ambao mazao Yao yameharibiwa na Wanyama waharibifu wakiwemo Tembo baada ya kata hiyo kupakana na hifadhi ‎ ‎Diwani Tontololo amewashukuru Wazee hao kwa kumueleza changam...