UWANKA yapata viongozi wa muda kwa kipindi cha miezi sita




Na Israel Mwaisaka, Nkasi

Umoja wa Watumishi Nkasi UWANKA umepata viongozi wa mpito watakaouongoza Umoja huo kwa kipindi cha miezi sita.

Viongozi hao Moja ya jukumu kubwa walilonalo ni kujenga umoja huo na kuweka misingi itakayotumika ikiwa ni pamoja na kuandaa uchaguzi mkuu kwa mujibu wa katiba ya umoja huo na kupata viongozi wa kudumu.



Waliochaguliwa ni Mwenyekiti Didas Saadan,Makamo mwenyekiti Beatrice Mlay,Katibu mkuu Victor Makoba na mweka hazina Abbas Kiloge.

Kwa mujibu Afisa utumishi wa halmashauri ya wilaya Nkasi Rainel Mwenda kwa niaba ya mkurugenzi Mtendaji Afraha Hassan ni kuwa umoja huo dhumuni lake kubwa ni kusaidiana wakati wa shida ikiwa ni pamoja na kuleta ushirikiano na umoja mahala pa kazi.


Ili mtumishi aweze kuwa mwanachama wa umoja huo atalazimika kujiunga kwa kiingilio cha Tshs,20,000 na zoezi Hilo limeanza sasa Hadi Juni 25,2025.

Mwenda amedai kuwa umoja huo kama utakwenda sawa na malengo waliyoyaweka huenda wakaenda mbali Zaidi kwa kutengeneza ushirika wenye nguvu utakaokuwa wa mfano katika wilaya Nkasi na mkoa kwa ujumla.




Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa