SERIKALI YATENGA BILL, 6 KUJENGA DARAJA LA MSANGANO MTO NKANA KUKUZA RURSA ZA KIUCHUMI.



Na Ibrahim Yassin,Momba

WANANCHI wa vijiji vilivyopo katika bonde la Msangano wilayani Momba mkoani Songwe,wameanza kupata manufaa ya kukuza uchumi wao kutokana na serikali ya Rais Dr, Samia Suluhu kujenga daraja katika mto Nkana kuunganisha wakazi wa Momba –Tunduma hadi makao makuu ya mkoa.

Wananchi wa Bonde la Msangano asilimia 75 wanategemea kilimo,ufuga ji na uvuvi kuendesha maisha yao ya kila siku ambapo kwa miaka mingi walikumbwa na kadhia ya kusafirisha bidhaa zao kupitia njia ya Sumbaw anga mkoani Rukwa hadi kufika Tunduma –Mbozi na mkoawa Mbeya k utokana na ukosefu wa daraja.
Baada ya kero hiyo ya Muda mrefu,serikali ya Rais Dr,Samia ilisikia kilio cha wananchi na kutoa kiasi hicho cha fedha kujenga daraja hili kuwaon dolea wananchi kero iliyodumu zaidi ya miaka 20.



Wakizungumza jana wakati wa ziara ya katibu tawala wa mkoa wa Songwe,wakazi hao walisema Rais Dr,Samia ameingia katika kitabu cha kumbukumbu kwa kuwezesha ujenzi huo ambapo wakati wakandarasi wanaanza walidhani ni ndoto.

Safia Sinkala mkazi wa Msangano,alisema ni kama ndoto daraja kujeng wa kwani awamu nyingi za Marais zimepita pasipo kujengwa hivyo wana kila sababu kumpongeza Rais Dr,Samia kwa kuona umuhimu wa kuwajengea daraja hilo,

Michael Silumbwe mkazi wa Msangano alisema daraja litakapo kamilika wataweza kusafiri kwa muda mfupi kwenda Tunduma na Mbozi ambapo awali walipita njia ya mzunguko wakitumia fedha nyingi na hata kulazimik a kushindwa kusafirisha mazao yao kwenda kuuza kwenye masoko ya uhakika.

Alisema wanatarajia kuwa na uchumi mkubwa kutokana na daraja hili kusafirisha mazao yao pamoja na samaki wanaotoka ziwa Rukwa hadi  Tunduma ,Songwe na Mbeya huku wakitarajiwa kufikiwa na wawekezaji wakubwa kutokana na uwepo wa darada hilo.

Akizungumzia hali hiyo,Meneja wa wakala wa barabara vijijini na mijini (Tarura) Mhandisi,Yusuph Shaban kufuatia uhitaji mkubwa wa daraja kwa wakazi wa Momba hasa Tarafa ya Msangano na Kamsamba,serikali iliidhinisha fedha kwa ajili ya ujenzi.

Alisema Serikali ilisikia kilio cha wananchi na kuidhinisha kiasi cha Tsh,Bilioni 2 katika bajeti ya mwaka 2022-2023 fedha za tozo za mafuta (FUEL LEVY) katika ujenzi wa daraja la Msangano –Chindi baada ya kufanyika usanifu wa daraja hilo,ilibainika kuwa gharama ya ujenzi ni zaidi ya Bilioni 3.

Alisema Mwaka wa Fedha wa 2023-2024 yalitokea mabadiliko ya matumizi ya efdha za barabara Bilioni 1 ambazo zilipelekwa kwenye ujenzi wa daraja hilo,kufuatia makubaliano ya kikao cha baraza la madiwani ambao waliidhinisha ongezeko hilo.



Alisema mradi huo unatekelezwa na mkandarasi M/S LUKOLO COMPA NY ya Dar es Salaam  kwa Tsh,2,999,811,125.00 na utakamilika Mwezi Septemba 14/2025 mradi ukiwa wa miezi 24 ambapo hadi sasa upo asilimia 65.

Katibu tawala mkoani Songwe Happines Seneda,baada ya kuukagua mradi huo na kuridhika na hatua iliyopo alimtaka mkandarasi kuongeza kasi kwani ananchi wanauhitaji mkubwa wa daraja hilo ambalo walilihitaji kwa miaka mingi ili waongeze fursa za kiuchumi.

Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa