Posts

Showing posts from October, 2024

WACHUNGAJI NA VIONGOZI WA DINI WATAKIWA KUFANYA KAZI KUEPUKA KUWA OMBAOMBA.

Image
Na Abraham Mwaitenda, Songwe IMEELEZWA kuwa viongozi wa dini wakiwemo wachungaji wa makanisa wametakiwa kufanya kazi za kujiingizia kipato ili kujikwamua kiuchumi kuondokana na uombaomba. Kauli hiyo imetolewa jana .na mmoja wa wadhamini wa kanisa la Marafiki Duniani Mch.,Erick Roy .raia wa Marekani wakati akizungumza na viongozi wa kanisa la.Friend Church mjini Tunduma. Mch. Roy amesema kufanya kazi ni Ibada hivyo wachungaji na viongozi wengine wametakiwa kufanya kazi na kuwawezesha waumini wao mbinu za kutafuta mali ili wajikwamue kiuchumi. Amesema Mungu mwenyewe alifanya kazi siku 6 lakini alipumzika siku ya 7 na akasisitiza kuwa asiyefanya kazi na asile ,hivyo ni wajibu watumishi wa mungu kufanya kazi ili kujiingizia kipato. Amesema wachungaji wakiwa na uchumi mzuri wataendesha ibada vizuri, waumini  wakiwa.na  uchumi watahudhuria ibada na kutoa sadaka na fungu la kumi vizuri na kanisa litaemdelea. " wachungaji wengi wamekuwa wakiendesha maisha kwa kutegemea sadaka za waumini ...

Serikali wilayani Songwe yaweka mkakati kuboresha uzalisha wa zao la tumbaku

Image
Na Ibrahim Yassin,Songwe. Mkuu wa Wilaya ya Songwe, Mhe. Solomon Itunda amekutana na kufanya mazungumzo na wadau wa kilimo cha Tumbaku kujadili mikakati ya kuboresha uzalishaji wa zao hilo kwa msimu wa 2024/2025. Mazungumzo hayo yalifanyika jana kwenye ofisi ya mkuu wa wilaya iliyopo Mkwajuni ambapo walikubaliana kufanya utafiti kubaini mbolea inayoendana na udongo kwenye eneo hilo. Mbali na hilo pia walijadili mambo mengi ikiwemo kupeana elimu ya kilimo na matumizi ya pembejeo za kilimo kwa wakulima. Akizungumza mara baada ya kikao hicho, Mhe. Itunda amesema kuwa Wilaya hiyo inatarajia kupata zaidi ya kilo 3.6 milioni kwa msimu wa kilimo wa 2024/2025. Amewataka maafisa ugani kuhakikisha wanawafikia wakulima ili wawape elimu na ushauri wa kitaalamu utakaoleta matokeo yenye tija kwa wakulima wa zao hilo. Hata hivyo, Mhe. Itunda amemshukuru Rais wa JMT, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuingiza zao la tumbaku kwenye pambejeo za mbolea za ruzuku na kutoa vitendea kazi kwa maafis...

Afisa Mtendaji Ahukumiwa Kifungo cha Miaka 60 kwa Ubadhirifu wa Fedha

Image
Na,Israel Mwaisaka,Nkasi Mahakama ya Wilaya ya Nkasi, mkoani Rukwa, imemhukumu kifungo cha miaka 60 jela afisa mtendaji wa kijiji cha Paramawe, Richard Kiwela (45), kwa makosa matatu, ikiwemo kuibia Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi kiasi cha shilingi 2,881,000 (Mil.2.8) alizokusanya kupitia mashine ya POS. Mtuhumiwa alikabiliwa na mashitaka ya matumizi mabaya ya madaraka, ubadhirifu na kuisababishia hasara mamlaka, kinyume na sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa namba 11/2007 pamoja na sheria ya uhujumu uchumi. Mashitaka yalitolewa na mwendesha mashitaka wa TAKUKURU, Mzalendo Widege. Mahakama ilipokea vielelezo 12 vilivyowasilishwa na upande wa mashitaka, ambavyo mtuhumiwa alikubali, hivyo kuimarisha kesi dhidi yake. Mwendesha mashitaka alieleza kuwa Kiwela alikabidhiwa mashine hiyo mnamo Novemba 11, 2018, na alikusanya jumla ya shilingi 55,825,600,  (Mil.55.8) lakini alishindwa kuwasilisha kiasi cha shilingi 2,881,000(Mil.2.8) Hakimu mkazi mfawidhi, Denis Luwungo, alikubaliana na mas...

CHMT SONGWE NA MKAKATI WA KUZUIA MAGONJWA YA MLIPUKO

Image
Na.Ibrahim Yassin. Songwe Mkuu wa Wilaya ya Songwe,Mhe. Solomon Itunda amefanya kikao na Timu ya Usimamizi wa Huduma za Afya (CHMT) Wilayani humo kujadili masuala ya kiafya ikiwemo namna ya kuzuia magonjwa ya mlipuko katika Wilaya hiyo. Mhe. Itunda amekutana na timu hiyo mwanzoni mwa wiki hii katika ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Songwe iliyopo Mkwajuni huku akiiagiza timu hiyo kuhakikisha wanasimamia usafi wa mazingira na kila kaya kuwa na vyoo bora. Amesema kuwa kaya na maeneo yanayotoa huduma ambayo hayana vyoo bora wanaohusika wachukukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria zilizopo. "kumekuwa na kawaida kwa baadhi ya kaya kuwa na vyoo hatarishi kwa afya , tunataka ujenzi wa vyoo bora vyenye maji tiririka ili kuepuka magonjwa ya milipuko"amesema Dc Itunda. Mganga mkuu wilayani humo Dkt.Carvin Mwasha amesema wamejipanga vizuri kutimiza agizo la mkuu wa wilaya kwani timu yake ya wataalamu itahakikisha kila kilichopangwa kinafanyika kiufasaha. "Afya za wananchi ni muhimu kwani shu...

MADIWANI WAPITISHA AZIMIO KUZIITA SHULE MAJINA YA DC NA DED WA SONGWE.

Image
LENGO NI  KUTAMBUA MCHANGO WAO KATIKA KUIMARISHA MAHUSIANO NA USIMAMIZI MZURI WA MIRADI. Na Ibrahim Yassin,Songwe.  Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Songwe mkoani hapa,limepitisha azimio la kuzipa majina ya Solomon Itunda (Mkuu wa Wilaya ya Songwe) na CPA. Cecilia Kavishe (Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songwe) shule mbili mpya ambazo ujenzi wake umeanza. Lengo la madiwani kupitisha azimio hilo  ni kutambua mchango wa viongozi hao wa kuimarisha ma husiano katika wilaya hiyo pamoja na usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo. Azimio hilo limepitishwa jana Jumanne Oktoba 22, 2024 wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani cha robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2024/20 25 kilichofanyika katika ukumbi wa Sambila uliopo katika ofisi za Halmashauri. Azimio hilo limepitishwa baada ya madiwani kupata nafasi kila mmoja kujadili sababu za kuzipa shule hizo majina ya viongozi hao, wakieleza kuwa wamekuwa wakiimarisha mahusiano na kusababisha Wilaya kuwa na utulivu. Mbali na wi...

UONGOZI WA JUU BONDE LA MTO SONGWE WATOLEA UFAFANUZI MIKAKATI ILIYOPO KUDHIBITI KUHAMA HAMA KWA MPAKA TANZANIA NA MALAWI.

Image
Na Ibrahim Yassin,yassin.ibrahimu@yahoo.com  0718382817 Imeelezwa kuwa uharibifu wa mazingira unaofanywa na wananchi hadi kwenye kingo za mto imetajwa kuwa chanzo mto Songwe kugawa upya mpaka wa Tanzania na Malawi. DiraKamilifu ilifika kijijini humo kuzungumza na wananchi wakiwemo viongozi wa pande zote mbili kujua sababu ya uharibifu huo na mipango iliyopo ya kunusuru hali hiyo. Umoja wa waendesha mitumbwi wanaovusha watu na mizigo kwenda upande wa pili wa nchi ,wakiongozwa na mjumbe wa kijiji cha Mpung uti,Ambele Mwaikeneke,anasema uharibifu wa mazingira hasa watu kulima hadi kwenye kingo za mito ndiyo sababu kubwa, Nae Harodi Mwakatundu mwenyekiti wa CCM kata ya Katumba Songwe alilieleza gazeti hili kuwa wakazi wa pande zote mbili wamekuwa wakiharibu mazingira kwa kulima na kufanya shughuri za kibinadamu hadi kwenye kingo za mto huo. Hata hivyo anasema wanafanya kila linalowezekana kuongeza katazo na kudhibiti uharibifu huo ili kurejesha njia ya asili ya mto huo jambo ambalo linahit...

WANANCHI KYELA WANG'AKA KWA MAMLAKA YA MJI MDOGO KUTAKA KUVUNJWA

Image
                                             MAKALA Na Ibrahim Yassin, yassin,ibrahimu@yahoo.com 0718382817 IMEELEZWA kuwa siasa za hila,maji taka,chuki binafsi uelewa mdogo kwa baadhi ya viongozi wilayani Kyela mkoani Mbeya zatajwa kuwa ni chanzo cha kutaka mamlaka ya mji mdogo wa Kyela uvunjwe Dira kamilifu limebaini. Mwandishi wa Dirakamilifu aliweka kambi ya siku 20 wilayani humo kuzungumza na wananchi pamoja na viongozi wa pande zote kutaka kujua mamlaka ilianzishwa kwa sababu ipi na nini sababu ya kutaka kuvunjwa. Chief Kennedy Koroso Mwananchi na kiongozi mstaafu wa CCM anasema kwa upande wake haoni sababu ya uwepo wa mamlaka ya mji mdogo kwani imekaa zaidi ya miaka 10 imeshindwa kupata hadhi kuwa halmashauri ya mji kama ilivyo Tunduma. Anasema wakati tunduma iliyopo mkoani Songwe imepaishwa kuwa mamlaka ya mji mwaka huo huo Kyela nayo ilipaishwa ,lakini Tunduma imepaishwa kuwa halmashauri ya mji katika kipindi cha miaka 3 pekee lakini Kyela ni zaidi ya miaka 10 haijapata hadh...

Uongozi wa Rais Samia waing'arisha Kyela kwa maendeleo lukuki

Image
Na Ibrahim Yassin. Kyela IMEELEZWA kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan ameweka historia ya kimaendeleo Wilayani Kyela Mkoani Mbeya. Hayo yamebainika baada ya Dirakamilifu kuongea na madiwani pamoja na wadau wa Maendeleo Wilayani humo ambapo wamesema Wilaya ya Kyela imekumbana na mabadiliko makubwa ya Kimaendeleo kutoka kwa Rais Samia Suluhu Hassan. Elia Mwaipetania Diwani wa Kata ya Ipinda ameeleza kuwa tangu aingie madarakani kama Diwani amekuwa akifanya kazi zake kirahisi kutokana na uwepo wa Rais Samia kwa kuwapiga tafu kila wanapoomba msaada wa kimaendeleo. Mwaipetania amesema Rais samia amekuwa akitoa fedha kwa kila Sekta jambo ambalo limepelekea uwepo wa maendeleo ya haraka Wilayani Kyela na kusema kuwa huenda ndiye Rais aliyevunja rekodi ya mageuzi ya kimaendeleo katika wilaya ya Kyela. Amesema licha ya wilaya hiyo kukumbwa na changamoto za kisiasa kwa miaka mingi kutokana na uwepo wa makundi lakini kwa miaka ya hivi kalibuni kumekuwepo na utuli...

Mfumo wa stakabadhi gharani ulivyonufaisha Wakulima wa zao la ufuta mkoani Songwe

Image
                 MAKALA Wakulima wapelekwa Morogoro kujifunza mbinu mkoani Morogoro huku wakiibuka na zao la Mbaazi Na Ibrahim Yassn, yassin.ibrahimu@yahoo.com 0718382817. WANANCHI ambao ni wakulima katika halmashauri ya wilaya ya Songwe mkoani Songwe wameeleza jinsi wanavyonufaika na kilimo cha mazao mbalimbali l ikiwemo zao la ufuta kupitia mfumo stakabadhi gharani,huku mpango uliopo ni kuanza kilimo cha mbaazi. Asilimia 75 ya wakazi wa Songwe ni wakulima,wafugaji,wavuvi na wachimbaji ambao wanaendesha maisha yao kupitia mazao hayo huku zao la ufuta likiwatajirisha zaidi. Licha ya wilaya hiyo kuwa ni ya uchimbaji wa madini ya dhahabu,lakini wakazi wa eneo hilo wameanza kujiingiza katika kilimo huku halmashauri ikiwashika mkono kuwezesha kilimo chenye tija. Halmashauri hiyo ilianza kuzalisha zao la ufuta kabla ya kuanzishwa kwa wilaya hiyo wakati huo ikiwa chini ya wilaya ya Chunya, ikijulikana kama Tarafa ya Kwimba na Songwe. Kwa kuwa hawakuwa na stakabadhi gharani, wakulima k...

Mkuu wa wilaya Nkasi awaongoza Wananchi kujiandikisha kwenye daftari la mpiga kura

Image
Na Israel Mwaisaka,Nkasi MKUU wa wilaya Nkasi mkoani Rukwa Peter Lijualikali ameongoza wakazi wa wilaya Nkasi Kwa kujiandikisha kwenye daftari la wakazi Kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika Novemba 27,mwaka Huu. Mkuu huyo wa wilaya amejiandikisha kwenye kitongoji chake Cha juhudi kilichopo kata ya Nkomolo wilayani Nkasi. Akizungumza mara baada ya kujiandikisha amesema kujiandikisha kwenye daftari Hilo litawafanya Wananchi kutumia haki yao ya kikatiba ya kuwachagua viongozi wanaowataka kwenye vitongoji na vijiji vyao. Alidai kuwa licha ya kujiandikisha Kwa ajili ya kupiga kura kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa Bali pia litatumika kama orodha ya wakazi kwenye kitongoji husika na kuwa hiyo Sasa ni fursa Kwa Kila mmoja kujiandikisha. Hivyo aliwataka Wananchi waliojitokeza kujiandikisha katika kitongoji hicho Cha Juhudi kuendelea kuwahamasisha wenzao Kwa kuhakikisha Kila mmoja anajitokeza na kwenda kujiandikisha kwenye kitongoji Ili aweze kupata haki ya kupiga kura ik...

Waandikishaji wa Wapiga kura waonywa dhidi ya Rushwa

Image
Na Baraka Lusajo,Kalambo Kamati ya ulinzi na usalama Wilayani Kalambo Mkoani Rukwa imetoa tahadhari kwa waandikishaji wa Wapiga kura kujiepusha na vitendo vya rushwa ikiwa ni pamoja na kutowaandikisha watu kutoka Nchi za jirani na kusisitiza kuchukua hatua kali za kisheria dhidi ya wandikishaji ambao watabainika kukiuka kwa makusudi kanuni za uchaguzi. Mapema akiongea kupitia mafunzo ya wandikishaji Wapiga kura Wilayani humo, Mkuu wa TAKUKURU Wilayani Kalambo Lupakisyo Mwakyolile akawataka wandikishaji kujiepusha na vitendo vya rushwa wakati wa zoezi hilo na kusema mtu au watu ambao watabainika kujihusiha na vitendo hivyo watachukulia hatua kali za kisheria ikiwemo kifungo cha miaka 20 jela Mkuu wa idara ya uhamiaji Wilayani humo Bw. Kumbo Shaban Mbwana amesema watu watakao takiwa kujiandikisha kwenye zoezi hilo ni wale ambao ni raia wa Tanzania na kusisitiza wandikishaji kufanya kazi hiyo kwa weledi na kwa kuzingatia miongozo iliyotolewa na Serikali. Katibu tawala Wilayani humo Bw. Se...

Waandikishaji wa Wapiga kura waonywa dhidi ya Rushwa

Image
Na Baraka Lusajo,Kalambo Kamati ya ulinzi na usalama Wilayani Kalambo Mkoani Rukwa imetoa tahadhari kwa waandikishaji wa Wapiga kura kujiepusha na vitendo vya rushwa ikiwa ni pamoja na kutowaandikisha watu kutoka Nchi za jirani na kusisitiza kuchukua hatua kali za kisheria dhidi ya wandikishaji ambao watabainika kukiuka kwa makusudi kanuni za uchaguzi. Mapema akiongea kupitia mafunzo ya wandikishaji Wapiga kura Wilayani humo, Mkuu wa TAKUKURU Wilayani Kalambo Lupakisyo Mwakyolile akawataka wandikishaji kujiepusha na vitendo vya rushwa wakati wa zoezi hilo na kusema mtu au watu ambao watabainika kujihusiha na vitendo hivyo watachukulia hatua kali za kisheria ikiwemo kifungo cha miaka 20 jela Mkuu wa idara ya uhamiaji Wilayani humo Bw. Kumbo Shaban Mbwana amesema watu watakao takiwa kujiandikisha kwenye zoezi hilo ni wale ambao ni raia wa Tanzania na kusisitiza wandikishaji kufanya kazi hiyo kwa weledi na kwa kuzingatia miongozo iliyotolewa na Serikali. Katibu tawala Wilayani humo Bw. Se...