Wananchi wafurahishwa kukamilika kwa mradi wa maji huku wakihitaji umeme kukuza uchumi
‘’Baada ya mradi huu kukamilika hakuna tena shida ya maji,ila tunaomba umeme,program ya serikali ya kila kijiji kuwa na umeme sisi hatujafikiw a,tunashindwa kuwa na kasi ya kiuchumi’’
Na Ibrahim Yassin,Songwe
WAKAZI wa kijiji cha Songambele kata ya Magamba wilayani Songwe mkoani hapa, wameanza kunufaika na mradi wa maji wa program ya serikali ya kujenga visima 900 nchi nzima ambao kwa kila jimbo kuchi mbiwa visima vitano na wao wakiwa ni wanufaika lakini wameomba wawekewe umeme kuongeza tija.
Kijiji cha Songambele kipo mpakani na vijiji viliyopo wilaya ya Mbozi,amba cho tayari kimeondokewa na uhaba wa maji ambapo kwa sasa hitaji lao kubwa ni umeme ili waweze kujenga miradi ya kibiashara kuongeza tija za kiuchumi.
Wakizungumza mwishoni mwa wiki,wakazi hao walisema awali walipata hadha kubwa ya maji na kulazimika kugombaniana na Ng’ombe maji ya kwnye madimbwi ambayo hata hivyo si safi na salama hali iliyosababisha waugue homa za matumbo.
Jesto Mgaza mkazi wa kijiji cha Songambele,alisema kwa kuwa mradi wa maji umeanza kufanya kazi,wanaomba wawekewe umeme ili waweze kufungua saloon na kuweka mashine za kusaga nafaka yakiwemo maduka ya vinywaji na vibanda umiza vya kuoneshea mpira kukuza uchumi.
Mwishoni mwa wiki katibu tawala mkoani Songwe Happiness Seneda alifa nya ziara kutembelea mradi huo wa maji,ambapo alikutana na wanan chi wakimueleza ukosefu wa umeme ambapo alimuinua meneja wa shirika la umeme (Tanesco ) wilayani Songwe kutoa maelezo.
Michael Kidoto meneja wa shirika la umeme Tanesco wilayani humo,alisem a ni kweli kijiji hicho hakina umeme,lakini kipo kwenye mpango wa bajeti ya mwaka 2025—2026 ambpo vitongoji 20 pekee ambavyo havina umeme vitawekewa.
Alisema mpango wa kuweka umeme kila kijiji umekamilika kwa kipindi kijacho wanaendelea kukamilisha kwenye vitongoji kwani vitongoji vyenye umeme ni 141,vilivyokosa ni vitongoji 20 pekee ambavyo tayari vipo kwenye mpango katika bajeti ijayo.
Baada ya kauli hiyo ya meneja,wananchi wakaridhika huku wakionesha wazi kuwa na uhitaji wa umeme,ndipo katibu Seneda alipo toa wasia kwa wananchi hasa wanaume kuheshimu ndoa zao kwa kuacha kuuza mazao na kukimbilia mijini kuanzisha maisha mapya na wanawake wengine.
‘’Kumekuwa na kawaida ya wanaume wakivuna mazao wanauza na kuzitelekeza familia zao na kuanzisha maisha mapya na wanawake wengine,aliwataka wanaume kuheshimu ndoa zao ili wapate Baraka kwa mungu.




Comments
Post a Comment