RAS -SENEDA ARIDHISHWA NA UJENZI JENGO LA UTAWALA HOSPITALI YA WILAYA YA SONGWE.
Na Ibrahim Yassin,Songwe
KATIBU Tawala mkoani Songwe Happines Seneda,ameridhishwa na ujenzi wa miundombinu ikiwemo jengo la utawala katika hospitali ya wilaya ya Songwe baada ya kufanya ukaguzi akiwa na wataalam kutoka mkoani.
Hospitali ya wilaya ya Songwe ni miungoni mwa hospitali 67 za awali katika mpango wa maboresho ya miundombinu ya kutolea huduma za Afya nchini na utekelezaji wake ulianza Mwezi Machi 25/2019 ambapo fedha zilitolewa kwa awamu 7.
Jumla ya Tsh,Bilioni 3.785 za Uviko zilitolewa na serikali kuu na zilitolewa kwa awamu 7 zikijenga majengo 17 kwa mtindo wa Force Accaunt na majengo yote muhimu yalijengwa kilichosalia ni ukamilishaji wa baadhi ya miundombinu na jengo la utawala likiwa asilimia 99.
Akizungumza jana na mwandishi wa Habari hizi,Mganga mkuu wa hospitali ya wilaya hiyo.Dkt,Kalvin Mwasha alisema Pmoja na ukamilishaji wa majen go hayo,pia walipokea fedha Tsh,Milioni 400 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba kwa awamu mbili.
Alisema mwaka 2024-25 hospitali ilipokea Tsh,Milioni 235 kwa ajili ya umaliziaji na ukamilishaji wa majengo manne wodi mbili za upasuaji,ufung aji wa mirango,mfumo wa umeme,kuweka madirisha ya alminiam,jengo la kuhifadhia maiti,Jokofu na mfumo wa maji safi na taka.
Alisema Jengo la utawala ni kati ya majengo 7 ya awamu ya kwanza ambayo ujenzi wake ulianza 2018/2019 na baada yah apo ujenzi wake ulisimama ili Kutoa kipaumbele kukamilisha majengo 6 ya kutolea huduma kutokana na bajeti.
Dkt,Mosha alitaja manufaa ya mradi huo kuwa ni kuongeza wigo wa huduma kwa wateja kwani baadhiya ofisi za utawala zilikuwepo ndani ya jengo la wagonjwa wa nje ikiwemo ofisi ya mganga mkuu ,afisa ustawi na mhasibu wa hospitali.
Akizungumza kwaniaba ya wenzake Doroth Mwashilindi mkazi wa Mkwaju ni,alisema Rais Dkt,Samia amewaheshimisha hasa wanawake,kwani kabla ya mradi walitibiwa hospitali ya Misheni wakipanga foleni kutokana na uwingi wao.
Alisema kukamilika kwa hospitali hiyo kumewafanya waende kutibiwa kwa wakati na kurejea kwenye sehemu zao za kazi kuendelea na shughuri,kwa ni hakuna foleni na wanatibiwa haraka na kwa nidhamu ya hali ya juu.





Comments
Post a Comment