Kituo cha afya Kapele chaleta furaha kwa Wananchi,Rais Dkt,Samia atajwa kwenye mafanikio hayo
‘’Nilishuhudia mwaka 2018 dada yangu Aide Simkamba,akipoteza maisha akiwa njiani akikokotwa na baiskeli kwenda kujifungua kata ya Ikana kilometa 56, Rais Dkt,Samia ametufuta machozi’’
Na Ibrahim Yassin,Momba
Wananchi wa vijiji vilivyopo kata ya Kapele wilayani Momba mkoani Songw e wamemtaja Rais wa Tanzania Dkt,Samia Suluhu kuwa amewafuta macho zi baada ya kuwajengea kituo cha afya kinachotajwa kuwa mkombozi kwao baada ya ndugu zao kupoteza maisha wakitembea umbali mrefu kusaka tiba.
Kituo hicho cha afya kipo katika Tarafa ya Ndalambo ikiwa na vijiji 8 vyenye idadi ya watu25,442 kati ya hao wanaume ni 12,391 wanawake wakiwa 13,051 huku ikiwa na kaya 5,287.
Kutokana na idadi hiyo kuwa kubwa ,wakazi hao walianzisha ujenzi wa kituo hicho baada ya kuchoshwa kutembea umbali wa kilometa zaidi ya 50 hadi kituo cha afya Ikana hali iliyosababisha wanawake kuzalia njiani na wengine kufariki.
Baada ya kuanza ujenzi huo,halmashauri ya wilaya ya Momba iliomba fedha serikali kuu na mwaka 2018 walipokea Tsh,Milioni 400 na kuanza ujenzi kwa mfumo wa Force Akaunt wakijenga majengo matano.
Akitoa ushuhuda wa kufiwa na nduguye,Abia Simkamba ambaye pia ni mwenyekiti wa kijiji cha Kapele alisema mwaka 2018 dada yake Aide Simkamba alifariki dunia wakati anakokotwa na baiskeli kwenda kujifungua kata ya Ikana kilometa 56.
Alisema kukamilika kwa kituo hicho kutaondoa wanawake kuzalia njiani,wazee kushindwa kumudu kutembea kilometa 50 hadi 54 kutoka vitongoji vilivyo pembezoni mwa kijiji kwenda kata jirani ya Ikana.
Aliongeza kuwa kituo hicho kitawakomboa wao na hata wnaoishi maeneo jirani ambao ni wakazi wa kutoka vijiji jirani vya mkoa wa Rukwa na wan chi jirani ya Zambia ambao wamepakana nao.
Akizungumza jana na mwandishi wa habari hizi,Mganga mfawidhi wa kituo hicho,Violeth Nyaulin go,alisema bada ya kupokea fedha hizo walianza kujenga jingo la wagonjwa wan je (OPD) Maabara (Labaratory) ,jengo la upasuaji (Theater),afya ya uzazi (Maternity), Jengo la kulaza wagonjwa (IPD).
Alisema mbali na fedha hizo,pia halmashauri imetumia Tsh,Milioni 85 za mapato ya ndani kukamilisha jengo la wagonjwa wa nje (OPD) ambalo tayari limekamilika huku jingo la Maabara likiwa hatua za mwisho.
Hata hivyo mwishoni mwa wiki katibu tawala mkoani Songwe Happiness Seneda,akiwa katika ziara yake ya kikazi,alikagua kituo hicho na kuridhika hatua ya ujenzi huku akimwagiza msimamizi wa ujenzi kuongeza kasi ya umaliziaji majengo yaliyosalia.
‘’Tunafahamu jinsi wananchi walivyoteseka kufuata huduma ya matibabu kilometa nyingi,serikali ya Rais Samia ilitoa kiasi hicho cha fedha ili kuwaso gezea karibu wananchu huduma ya matibabu,nahitaji kuona changamoto z ujenzi zinamalizwa wananchi waanze kupata huduma’’alisema Seneda.
Wilaya ya Momba ni moja ya wilaya Mpya mkoani Songwe iliyomegwa kutoka wilaya mama ya Mbozi ikikabiriwa na changamoto nyingi zikiwemo za matibabu,lakini katika kipindi hiki cha Rais Dkt,Samia karibu kata zote zimejengewa vituo vya afya.




Comments
Post a Comment