Uwazi wa mapato na matumizi ya kijiji chawa kichocheo kwa Wananchi kushiriki shughuli za maendeleo



Mwenyekiti wa kijiji cha Swahila Legius Choma

Na Israel Mwaisaka, Rukwa

Wananchi wa Kijiji cha Swahila kata ya Mkwamba wilayani Nkasi wameridhishwa na uwazi unaofanya na viongozi wao wa Kijiji katika kuweka wazi mapato na matumizi kitu kinachowafanya wao kujitokeza katika shughuli mbalimbali za maendeleo ya kijiji.

Wakizungumza na Majira Wananchi hao walisesema kuwa hivi sasa wanajenga shule mpya ya msingi shikizi kwa njia ya kujitolea ikiwa ni pamoja na kuongeza ukubwa wa jengo la zahanati ya kijiji hicho na kuwa tayari kutoa michango mbalimbali ya kufanikisha shughuli hizo na kuwa michango yote wanayoitoa matokeo yake wanayaona na uwazi uliopo unawafanya kuendelea kujitolea kufanya kazi za maendeleo.

Sophia Kambaulaya,Edigar Minazi na Judithi Kipeta kwa niaba ya Wananchi hao wamedai kuwa katika siku za hivi karibuni wameguswa na utaratibu wa kujitolea kwenye shughuli za maendeleo kutokana na uwazi uliopo wa viongozi wao na kuwa hivi sasa uongozi wa Kijiji umekuwa ukiwasomea mapato na matumizi Kila wakati na kazi inayofanyika inaonekana.

Walisema kuwa kwa utaratibu huu ambao haukuwepo hapo nyuma umewatia nguvu kubwa ya kushiriki katika shughuliza maendeleo na kuwa hari hiyo utasaidia wao kujiletea maendeleo kwa haraka.

Mwenyekiti wa kijiji hicho Legius Choma amekiri kuwepo kwa Kasi ya Wananchi kujitokeza kwenye shughuli za maendeleo imekua kubwa na kuwa Siri kubwa ni uwazi tu wa michango wanayoitoa ikiwa ni pamoja na kazi inayofanyika kuonekana.

Alisema kuwa wao kama viongozi wa Kijiji waligundua kuwa kutokuwepo kwa uwazi wa michango umekuwa kikwazo kwa muda mrefu kwa Wananchi kujitokeza kwenye shughuli za maendeleo na kuwa sasa Kila kitu kinachofanyika kinafanyika kwa uwazi na shirikishi kwa Kila jambo na kuwa Hilo limeleta mvuto mkubwa wa Wananchi kujitokeza kwenye shughuli za maendeleo bila ya kusukumwa.

Pia amempongeza Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa namna alivyopeleka fedha za maendeleo katika maeneo mbalimbali na kuwa Hilo nalo limeamsha hari ya Watu kushikamana na kuamua kujitoa kushiriki shughuli za maendeleo

Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa