DIWANI MWASHITETE AYATAJA MABILIONI YA RAIS DKT,SAMIA YALIVYOING’ARISHA KATA YAKE
‘’Wanaomsema vibaya Rais Dkt,Samia wakapimwe akili,amegusa kila sekta kujenga miradi,imeturahisishia kupunguza hoja kwa wananchi wakati wa kuomba kura’’.
Na Ibrahim Yassin,Songwe
DIWANI wa kata ya Harungu wilayani Mbozi mkoani Songwe Maarifa Mwashitete,amemsifu Rais Dkt,Samia Suluhu kwa kujenga miradi iliyogusa jamii katika idara zote huku akiwaponda wanaomsema vibaya Rais akidai kuwa wakapimwe akili.
Mwashitete aliyedumu nafasi hiyo kwa mihura miwili ambapo miaka mitano iliyopita alikuwa diwani kupitia chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) ambapo pia alikuwa mwenyekiti wa vijana mkoani humo,alipohamia CCM aliukwaa tena udiwani.
Alisema kata yake ina vijiji 6,vitongoji 31 ikiwa na wakazi zaidi ya 30,000 ambao awamu zilizopita walikuwa wakikabiliwa na changamoto nyingi zilizopatiwa majibu katika awamu ya sita,kwa kujengewa miradi sekta zote.
Alisema katika utawala wake wa miaka mitano chini ya Rais Samia kata yake imenufaika zaidi kwa kuletewa mabilioni ya fedha kujenga miradi ambapo kwenye miradi yake alipokea Bilioni 3.91katika kipindi cha miaka 5.
Alisema mbali na fedha hizo,pia katika sekta ya umeme kata hiyo ilipatiwa Bilioni 1.340 ambapo vijiji vyote vimepatiwa umeme na wananchi wameanza kukuza uchumi wao kwa kuweka vitega uchumi mbalimbali zikiwemo mashine za kusaga nafaka.
Mbali na fedha hizo pia katika sekta ya miundombinu,kata hiyo ilipokea Tsh,Milioni 500 zilizopelekea barabara zote kujengwa kwa kiwango cha vumbi na changarawe na kuifanya kata hiyo kufunguka na wakulima kupitisha mazao yao kiurahisi.
Alisema barabara ya Harungu kwenda Hambangala yenye kilometa 9.2 ilikuwa haipitiki,lakini awamu ya sita imejengwa na inapitika masaa yote wananchi,hasa wakulima na wagonjwa waliokuwa wakitaabika sasa watembea kifua mbele.
Aliongeza kuwa katika fedha Bilioni 3.91 zilisaidia kujenga miradi ya elimu afya,Maji na kuboresha miundombinu chakavu ikiwemo kujenga kituo cha afya cha kisasa kinachotoa huduma masaa 24 kilichowapunguzia watu kutembea umbali wa kilometa 20 kwenda Vwawa.
Alisema mbali na kujengewa kituo hicho pia kata yake vijiji vyote vimejengewa zahanati hali ilifuwarahisishia wananchi kupata tiba ambapo awali wengi walikuwa wakienda kwa waganga wa tiba za jadi kutibiwa.
Mchungaji Mwashitete,alisema katika sekta ya elimu kila kijiji kimejengewa shule za msingi na katika kata hiyo wameweza kujenga shule za sekondari 3 wakivuka lengo la serikali la kuwa na sekondari moja kila kata.
Aliongeza kuwa Katika sekondari ya Harungu iliyoanzishwa mwaka 1975 awamu zilizopita ilikuwa hoi lakini awamu hii ya sita imeboreshwa na kujengewa madarasa mapya likiwemo darasa la Maabara likiwa na vifaa vyote.
‘’Nina kila sababu ya kujipongeza mimi,kuwapongeza viongozi wangu wa wilaya na mkoa akiwemo Rais Dkt,Samia kwa kazi kubwa iliyofanyika kwenye kata yangu,kitendo cha kila kijiji kuwa na shule na kata kuwa na shule 3 za sekondari sio kitu kidogo,’’alisema.
Hata hivyo Mwashitete,aliwajia juu baadhi ya watu wanaowasema vibaya viongozi wakuu wan chi hii,akisema wakapimwe akili,kwani katika awamu zote toka nchi ianzishwe hakuna awamu iliyofanya kazi kubwa kama awamu ya sita.
Katibu kata wa ccm Jummanne Mwafywefwe alisema ilani ya chama chake imetekelezwa kwa vitendo,hivyo aliwaomba wananchi waendelee kuiamini ccm kutokana na kazi kubwa ya ujenzi wa miradi iliyoifanya.
Affect Panja katibu wa siasa na malezi wa kata hiyo,ataendelea kuwale vizuri viongozi wake wa kata hiyo ili waendelee kuwatumikia wananchi kwani wamepunguza hoja za kujieleza kwa wananchi,Rais Samia amewabeba wanatembea kifua mbele.
Jumamosi Mwaenga mwenyekiti wa wazazi wa kata hiyo,alisema mwaka 2020 sekta zote zilikuwa na changamoto,lakini 2025 kila sekta imejengwa na kuboreshwa.
Alisema mwaka huu kituo cha afya cha kisasa kimejengwa,kila kijiji kina zahanati na shule wamefikia hatua ya kuvuka lengo kwa kujenga sekondari 3 katika kata moja huku vyoo vya kisasa na miundombinu ikiboreshwa.




Comments
Post a Comment