Posts

Showing posts from March, 2025

Mvua yenye upepo mkali yasababisha maafa nyumba zabomoka, familia zakosa makazi

Image
Na Israel Mwaisaka, Nkasi Nyumba 29 zimebomoka na nyingine kuezuliwa para kufuatia mvua yenye upepo mkali katika vijiji vya Mabatini na Mkangale kata ya Namanyere huku familia kadhaa zikiachwa bila ya makazi. Diwani wa kata ya Namanyere Nestory Kaloto akitoa taarifa mbele ya kamati ya maafa ya wilaya ikiongozwa na mkuu wa wilaya Nkasi Peter Lijualikali amesema kuwa tukio Hilo limetokea juzi jioni baada ya mvua iliyokuwa imeambatana na upepo mkali kunyesha na kusababisha maafa hayo. Amesema kuwa wengi wao wanahifadhiwa na majirani zao na kuwa wengi wanahitaji msaada mkubwa na wa haraka Ili kuweza kurudia katika hari Yao ya kawaida. Mkuu wa wilaya ambaye pia ndiye mwenyekiti wa kamati ya maafa ya wilaya Peter Lijualikali kwa upande wake amewataka wakazi wa eneo Hilo kupanda miti ya kutosha Ili kukabiliana na changamoto hiyo Na kuwa ameagiza halmashauri kupeleka mara Moja Miche ya miti mbalimbali Ili waanze kuipanda miti hiyo. Pia amewataka kufuata kanuni za ujenzi pale wanapoanza kujen...

Walimu watakiwa kuutumia muda wa ziada kufanya shughuli zao za kiuchumi kujiongezea kipato

Image
Na Israel Mwaisaka,Rukwa MKUU wa wilaya ya Nkasi Peter Lijualikali amewataka Walimu kuutumia vizuri muda wao baada ya kazi kujishughulisha na shughuli nyingine za kiuchumi kama kilimo na ufugaji ili kuweza kujiongezea kipato. Rai hiyo ameitoa jana kwenye ufunguzi wa mkutano mkuu wa uchaguzi wa Chama Cha Walimu Tanzania (CWT) wilaya Nkasi ambapo alidai kuwa kimsingi mishahara haiwezi kutosheleza mahitaji yote ya kijamii na hivyo kujishirikisha katika shughuli nyingine za kiuchumi ili kukuza kipato chao. Alisema kuwa wilaya Nkasi ni moja ya eneo zuri sana kwa kilimo na ufugaji na kuwa kama watajikita katika sekta hiyo ya kilimo na ufugaji ni rahisi san asana kuweza kujikwamua kiuchumi na kuweza kuifanya vyema kazi yao ya Ualimu na kuweza kuleta tija mahala pao pa pazi. Pia aliwasihi Walimu kuendelea kulinda maadili ya kazi yao na kuwa kwa kufanya hivyo kutaifanya kazi yao kuheshimika na wao kuwa kioo katika jamii badala ya wao kuwa watu wa hovyo na kuwa kitu hicho hakikubaliki. Awali k...

MAMA NA WATOTO WAKE WAWILI WATEKETEA KWA MOTO BABA MAHUTUTI BAADA YA NYUMBA YAO KUUNGUA MOTO

Image
Na Israel Mwaisaka, Rukwa Watu watatu wa familia Moja wakazi wa Kijiji cha Lyapinda kitongoji cha Lupata  kata ya Kizumbi wilayani Nkasi  mkoani Rukwa wamefariki kwa moto baada ya nyumba Yao waliyokuwa wakiishi Kushika moto kufuatia mafuta ya Petrol waliyokuwa wameyahifadhi ndani ya nyumba  kushika moto. Akitoa taarifa mbele ya mkuu wa wilaya Nkasi Peter Lijualikali diwani wa kata ya Kizumbi Mashaka Kamsipi alisema kuwa waliofariki katika moto huo ni Mama na Watoto wake wawili huku Baba akijeruhiwa vibaya kwa moto alipokuwa kwenye jitihada za kuiokoa familia yake kutoka kwenye moto. Alisema kuwa Baba wa familia hiyo  Timothy Katumbo (31) ambaye alikua ni dereva wa boda boda alikua akihifadhi mafuta ya pikipiki ndani ya nyumba Yao waliyokuwa wakiishi na siku ya tukio dereva huyo asubuhi mnamo majira ya saa Moja asubuhi aliweka mafuta aliyokua ameyahifadhi nyumbani kwake na kuwa baada ya kuweka mafuta kulikua na mafuta yaliyokuwa yakidondoka chini na baada ya mke kuwasha kiberiti Ili awa...

Mtandao wa Polisi Wanawake TPF-Net Nkasi wafanya matendo ya huruma kuelekea siku ya Wanawake duniani

Image
Na Israel Mwaisaka,Nkasi MTANDAO wa Polisi Wanawake wilayani Nkasi mkoani Rukwa TPF-NET limeafanya matendo ya huruma kwa kuwatembelea wagonjwa katika hospitali ya wilaya Nkasi na kuwapatia zawadi mbalimbali kama sehemu ya maadhimisho ya siku ya Wanawake duniani. Akizungumza wakati wa kukabidhi misaada hiyo kwa wagonjwa mwenyekiti wa mtandao wa Polisi wilayani Nkasi Ivona Mwanga amesema kuwa katika kuelekea kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya Wanawake duniani March 8 wao wameonelea kufanya matendo hayo ya huruma kwa kuwapatia zawadi mbalimbali huku wakitoa ujumbe mahususi juu ya siku ya Wanawake duniani. Amesema kuwa TPF-Net kama mtandao wa Polisi Wanawake umeundwa kwa ajili ya kuisaidia jamii katika kukabiliana na vitendo mbalimbali vya ukatili katika jamii na kuwataka Wananchi kutokaa kimya pale wanapoona wanaonewa bali wakimbilie Polisi ambako lipo dawati la jinsia na Watoto ambako wanaweza kupata haki zao za kimsingi Katibu wa mtandao huo Anna kisimba kwa upande wake amei...

DC_DED WAWAASA VIJANA KUTOKAA VIJIWENI KUPIGA SOGA. WAKITENGA BIL.1.39 ZA MIKOPO.

Image
Na Ibrahim Yassin,Songwe VIJANA waaswa kuto kukaa vijiweni kupiga soga na kujadili mambo ya umbea na badala yake wametakiwa waunde vikundi wapate mikopo wajiingize kwenye ujasiliamali. Kauli hiyo ilitolewa siku za hivi karibuni na mkuu wa wilaya ya Songwe  Solomon Itunda akiwa kwenye ziara zake ngazi za vijiji na kata wilayani humo. Katika ziara hizo Itunda mbali na kukagua miradi ya maendeleo pia aliitisha mikutano ya hadhara kuwaeleza wananchi kuchangamkia fursa za mikopo ya asilimia 10. Alisema serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt.Samia Suluhu awali ilisitisha utoaji wa mikopo kwa sababu ya changamoto kadhaa lakini tayari imeruhusu mikopo hiyo inayotolewa bila riba. Alisema wananchi walio kwenye vikundi waendelee kujiimarisha na wasio na vikundi wajiunge watapatiwa elimu na maafisa maendeleo ya  jamii kisha wasajiliwe kwa ajili ya kupatiwa mikopo. " Fedha za mikopo kwa vijana, wanawake na wenye ulemavu zipo na tayari baadhi ya vikundi vimeoatiwa, wale wasio na vikundi ji...

KIJIJI CHA KANAZI KUNUFAIKA NA MAJI YA KISIMA,

Image
Naibu waziri wa Maji Kundo Andrew Mathew jana tarehe Machi,03,2025 amefanya ziara ya kikazi katika halmashauri ya wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa katika ziara hiyo Naibu Waziri wa maji pia ameweka jiwe la msingi katika mradi wa maji Mkangale na amekagua mradi wa maji mtaa wa Isunta akiridhishwa na utekelezaji wake. Kutokana na mradi wa maji uliopo kijiji cha Kanazi kutoanza kutoa huduma ikamlazimu Naibu Waziri wa maji Kundo Mathew kutoa maelekezo ya serikali kuwa siku tano RUWASA mkoa wa Rukwa iwe imekamilisha matengenezo madomadogo ili wananchi wanufaike na matunda ya mradi huo. Mhadisi BRUNO ISAKWISA Mratibu wa Programu ya visima 900 mkoa wa Rukwa akieleza taarifa ya Mradi huo akisema visima saba (07) vinavyochimbwa katika halmashauri ya wilaya ya Nkasi ni pamoja na Lyele,kanazi,kipundu,kakoma, Ng*udwe,china na Mnyula na visima hivyo vilivyopata maji vimefikia asilimia 78 huku visima viwili (02) vimekosa maji Kalundi na lunyala . Kwa upande wao Wakazi hao wa kijiji cha Kanazi wamempokea...