BARABARA ILIYOAHIDIWA NA HAYATI DR,MAGUFULI YAANZA KUJENGWA KUING’ARISHA WILAYA YA SONGWE.
Na Ibrahim Yassin,Songwe
WANANCHI wilayani Songwe mkoani hapa wameanza kutabasamu baada ya wakala wa barabara za vijijini na mijini (Tarura) wilayani humo,kuanza ujenzi wa barabara ya kiwango cha Lami yenye urefu wa kilometa 4.0 itakayoiweka katika sura nzuri mji wa Mkwajuni.
Ujenzi wa barabara za Lami mkwajuni mjini ni utekelezaji wa ahadi ya aliyekuwa Rais wa awamu ya tano Hayati Dr,John Magufuli wakati wa kampeni za uchaguzi mwezi Octoba 2025 akiwa wilayani humo alitoa ahadi hiyo.
Akizungumza jana wakati wa ziara ya katibu tawala mkoani humo, meneja wa wakala wa barabara mijini na vijijini (TARURA) Mhandisi Emmanuel Nkwera alisema mpaka sasa wamefanikiwa kujenga kilometa 2.87 kwa kiwango cha Lami na kuwa kukamilika kwa barabara hiyo itapelekea kuwa na barabara zenye urefu wa Kilometa 4.87.
Alisema ujenzi huo wa barabara za Mkwajuni zenye kilometa 2.0.Barabara ya Pangani Mita 320,Mdula Mita 410,Moravian 1 mita 240,Moravian 11 mita 320 unatekelezwa kwa fedha za tozo ya mafuta kwenye Tarafa ya Kwimba kata ya Mkwajuni.
Alisema mradi huo ulianza mwezi Agosti 28/2024 na unatarajiwa kukamilika Juni 12/2025 ukitekelezwa na mkandalasi Comt Enterpreneurs ya Iringa kwa gharama ya Tsh,Milioni 760.
Alisema kazi zinazofanyika ni kuandaa kitako cha barabara kwa kukata,kuchonga na kujaza changarawe katika baadhi ya maeneo,kuweka changarawe kwa ajili ya ‘’Sub Base’’,kuweka changarawe iliyochanganywa na saruji,(C1) kwa ajili ya ‘base course,
Aliongeza kuwa baada ya hapo itawekwa Lami matabaka mawili (DSD) Ikiwemo ujenzi wa mifereji na makalavati ambapo hadi sasa mkandalasi bado hajamjamlipa.
Aliongeza kuwa katika bajeti ya mwaka 2024-2025 Tarura wilaya ya Songwe kwa fedha za tozo ya mafuta imetengewa Tsh,1,000,000,000.00 ambapo hadi sasa wamepokea Tsh,37,500,000.00 sawa na asilimia 3.75.
Katibu tawala wa mkoa wa Songwe Happines Seneda,mbali na kuukubali mradi huo,alimtaka mkandalasi kuongeza kasi ya ujenzi ili wananchi waanze kupata fursa za kibiashara kwani eneo hilo litafungwa taa ili wananchi waweze kufanya biashara nyakati za usiku.
Ezekiel Mwashilindi mkazi wa Mkwajuni aliipongeza serikali kwa kuona umuhimu wa kujenga barabara hiyo makao makuu ya wilaya na kuondoa vumbi kwa wananchi nyakati za usiku kwa wananchi wanaoishi pembezoni mwa barabara.




Comments
Post a Comment