Posts

Showing posts from March, 2026

FIFA, TFF waanza utambuzi wa vipaji Rukwa.

Image
Na Israel Mwaisaka, Nkasi. Zoezi la utambuzi wa vipaji vya soka kwa watoto wa kike na kiume wenye umri wa miaka 12-16 limeanza mkoani Rukwa, likilenga kuandaa wachezaji wa baadaye wa timu za taifa. Zoezi hilo linaendeshwa chini ya wataalam kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA), ambapo mchakato wa awali wa ulianza rasmi ngazi ya halmashauri katika wilaya nne za mkoa wa Rukwa kuanzia Machi 12, 2026. Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa zoezi hilo, Mkuu wa Idara ya Utambuzi wa Vipaji kutoka TFF, Gidion Ngereza, alisema kuwa jumla ya watoto 180 walichaguliwa kuendelea kwenye hatua ya mkoa, iliyoanza Machi 16, 2026 na kuendelea kwa siku tano mkoani humo. Ngereza alisema kuwa lengo kuu la zoezi hili ni kutafuta wachezaji wa kike na kiume wenye vipaji ambao wanaweza kuingia kwenye timu ya taifa ya vijana. Aliongeza kuwa zoezi hili linafanyika katika mikoa 32 na halmashauri 184 kote nchini. Aidha, Ngereza aliwahimiza wazazi na...

SERIKALI KUWEKA UZIO WA UMEME KUTHIBITI TEMBO HIFADHI YA LWAFI. ‎

Image
‎ Na Israel Mwaisaka, Nkasi  ‎ ‎Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Nkasi Mkoani Rukwa Ndugu Afraha Hassan amesema Serikali inakusudia kuweka uzio wa umeme wenye thamani ya shilingi Billioni 7 katika kata tano (5) zinazozunguka maeneo ya hifadhi ya Lwafi ambao utasadia kudhibiti Wanyama waharifu aina ya Tembo kuharibu mazao ya wananchi. ‎ ‎Aliyasema hayo wakati wa mkutano wa hadhara uliokuwa na lengo la kusikiliza na kutatua kero za wananchi katika maeneo hayo na kusema uwepo wa uzio huo utakuwa suluhisho la kudumu katika kuwadhibti Wanyama hao na kuwataka wananchi kuendelea kuwa na subra wakati swala hilo likiendelea kufanyiwa kazi. ‎ ‎‘’suluhisho la kudumu litapatikana baada ya kuwekwa uzio wa umeme ni waya mfupi unaopitishwa kwenye vigingi, unakuwa mmoja au miwili, tembo akifika unampiga shoti,hivyo anakuwa anashindwa kuvuka Gharama yake ni kubwa ni takribani Billion saba hivi’’alisema Hassan. ‎ ‎Kwa upande wake Afisa Wanyama Poli Wilayani humo  Anod Shadrack Ngagashi,al...

WAZIRI MKUU KUANZA ZIARA MKOANI RUKWA KUANZIA MARCHI 8 HADI 10 AMBAPO ATAKAGUA MIRADI YA MAENDELEO NA KUZUNGUMZA NA WANANCHI

Image
‎ ‎Na Israel Mwaisaka,Rukwa ‎ ‎Waziri Mkuu, Dkt,Mwigulu Lameck Nchemba, anatarajia kufanya ziara ya kikazi Mkoani Rukwa kuanzia Machi 8 hadi 10, 2026. ‎ ‎Akitoa taarifa ya ziara hiyo mbele ya waandishi wa habari leo Machi 7, 2026, Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Charles Makongoro Nyerere, amesema ziara ya Mheshimiwa Waziri Mkuu inalenga kukagua maendeleo ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo, kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi na kusikiliza wananchi kupitia mikutano ya hadhara. ‎ ‎Katika taarifa yake, RC Makongoro ameeleza kuwa tarehe 8 Machi Waziri Mkuu atatembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Sumbawanga na Soko la Kimataifa la mazao Kanondo, na kisha kufanya mkutano wa hadhara katika Mji Mdogo wa Laela, Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga. ‎ ‎Tarehe 9 Machi Waziri Mkuu anatarajia kutembelea Wilaya ya Nkasi, kuweka jiwe la msingi la Shule ya Amali ya Mkoa iliyoko Namanyere na kufanya mkutano wa hadhara ambapo Pia atakagua Bandari ya Kasanga na kuzungumza na wa...

TAKUKURU Rukwa yazuia vitendo vya rushwa kwenye miradi ya Bil. 1.7

Image
Na Israel Mwaisaka, Rukwa ‎ ‎Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, TAKUKURU mkoani Rukwa, imefanikiwa kudhibiti vitendo vya rushwa katika miradi ya maendeleo yenye thamani ya shilingi bilioni 1.7 kwa kipindi cha Oktoba hadi Disemba mwaka 2025. ‎ ‎Akitoa taarifa kwa umma leo Februari 3,2026, Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Rukwa Mzalendo Widege alisema taasisi hiyo ilifanya ufuatiliaji wa miradi saba ya maendeleo na kubaini mapungufu mbalimbali yaliyotolewa ushauri na kufanyiwa kazi. ‎ ‎ Katika hatua nyingine, TAKUKURU ilifanikiwa kumrejesha mkandarasi aliyekuwa ameacha ujenzi wa bweni na madarasa katika Shule ya Sekondari Mzindakaya. ‎ ‎ Mradi huo wenye thamani ya shilingi milioni 380 ulisimama kwa miezi miwili kuanzia Oktoba hadi Novemba 2025 kutokana na mkandarasi kuwa na zabuni nyingi. ‎ ‎Baada ya mazungumzo yaliyohusisha pia Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga, mkandarasi huyo alirejea kazini mwezi Disemba 2025 na mradi unatarajiwa kukamilika hivi karibuni. ‎ ‎Katika kuboresha uteke...

Mafundi Rukwa wachaguana

Image
Na Israel Mwaisaka, Rukwa ‎ ‎UMOJA wa mafundi mkoa Rukwa kupitia Magic Builders Foundation umepata viongozi wapya watakaouongoza umoja huo kwa kipindi Cha miaka mitatu ijayo. ‎ ‎Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo uliofanyika kwenye ukumbi wa Libori mjini Sumbawanga Jana March Mosi 2026,Mwenyekiti wa uchaguzi Evarist Futakamba Mohammed alimtangaza Moses Simtowe kuwa Mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti ,Makamo Mwenyekiti Jerry Mwaijwanga, Katibu Mkuu Avary Gregory. ‎ ‎Wengine ni Katibu msaidizi Shambani Nyangindu,Katibu mkuu,Mtunza hazina Jabir Sanga, Mwenyekiti wa nidhamu Linus Kalikwenda na Musa Mzapora alichaguliwa kuwa Afisa habari. ‎ ‎Akizungumza mara baada ya kutangazwa rasmi kuwa Mwenyekiti Moses Simtowe aliwataka mafundi kuwa wamoja na kushirikiana kwa Kila jambo lakini kubwa ni kuhakikisha mafundi wanakua na mikataba halisi ya kikazi na wateja wao ili kuondoa changamoto za kulaumiana kati Yao na wateja wao na kutengeneza uhasama ‎ ‎Alidai kuwa umoja huo ukiimarishwa una nafasi hat...