Posts

Showing posts from April, 2025

WAANDIKISHAJI WAPIGA KURA WATAKIWA KUFANYA KAZI YAO KWA UWELEDI ILI KUFANIKISHA JUKUMU HILO LA KITAIFA

Image
Na Israel Mwaisaka,Nkasi WASHIRIKI wa mafunzo ya uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura awamu ya pili wametakiwa kufanya kazi yao kwa ueledi mkubwa ili kuweza kufanikisha jukumu hilo la msingi la kitaifa na kuhakikisha wale wote wenye sifa wanajiandikisha katika daftari hilo. Wito huo umetolewa jana na afisa mwandikishaji  wa wilaya Nkasi  Ladislaus Mzelela  alipokuwa akifunga mafunzo ya  siku moja  kwa maafisa Waandikishaji wasaidizi na waendesha vifaa  ambapo amedai kuwa jukumu lao ni kubwa hivyo uweledi pekee utapelekea kufanikisha kazi hiyo kwa ufanisi. Alisema kuwa mafunzo hayo  waliyoyapata kwa njia ya nadharia na vitendo yalijikita katika ujazaji fomu mbalimbali zitakazotumika vituoni  fomu za kiapo cha kutunza siri na kujitoa uanachama katika chama cha siasa ikiwa ni pamoja na namna ya kuandikisha wapiga kura wapya,wanaorekebisha au kuboresha taarifa zao ikiwa ni pamoja na wale wanaoondolewa au kufutwa kwenye daftari la kudumu la mpiga kura. Hivyo amewataka kutambua  uz...

JAMII YAASWA KUPANDA MITI YA ASILI KWENYE VYANZO VYA MAJI NA KINGO ZA MITO KULINDA UOTO WA ASILI

Image
JAMII YAASWA KUPANDA MITI YA ASILI KWENYE VYANZO VYA MAJI NA KINGO ZA MITO KULINDA UOTO WA ASILI ''Mimi ni mkulima wa mazao mseto.pia naotesha michw ya miti ya asili, kutokana na uzoefu nilioupata,nahitaji kuwafundisha vijana ili nikifa vizazi vijavyo viweze kufanya kama anavyofanya kuhepuka majanga na kuendeleza kilimo''.. Na Ibrahim Yassin,Songwe JAMII nchini imetakiwa kulinda vyanzo vya maji na kingo zake kwa kupanda miti ya asili kulinda na kutunza mazingira ili uoto wa asili usipotee na kusababisha majanga yanayoweza kuzuilika. Imekuwa ni kawaida kwa baadhi ya jamii kuharibu mazingira kwa kuendesha kilimo hadi kwenye kingo za maji ikiwemo kukata miti ovyo na kuchoma mikaa hali inayosababisha kuzuka kwa ukame wa mvua na mazingira kuharibika. Kauli hiyo imetolewa jana na  mkulima bora wa khawa anayelima kilimo mseto Benard Haonga kutoka kijiji cha Mbozi kata ya Igamba wilayani Mbozi mkoani hapa wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye bustani za kuoteshea Mic...

CCM Songwe wazungumzia mikakati ya uchaguzi,yawapoga pini wanaopitapita majimboni

Image
‘’wabunge waliopo madarakani waache woga,hata wao wakati wanasaka ubunge walipita majimboni,kama walishindwa kutimiza ahadi wajiandae kuwa na hoja nyingi za kujibu kwa wananchi’’. Na Ibrahimu Yassin,Songwe CHAMA cha mapinduzi (CCM) mkoani Songwe kimeeleza mikakati iliyojiwekea kufuatia uchaguzi mkuu ujao huku kikiwapiga pini makada wanaodaiwa kupita majimboni na kwenye kata kujitangaza ili kujiwekea mikakati mizuri ya ushindi. Akizungumza jana na waandishi wa habari,Katibu wa Siasa itikadi na mafunzo mkoani Songwe,Mwl, Yusuph Rajabu alisema mkoa umejiandaa vizuri kuhakikisha katika uchaguzi ujao hakuna kata wala jimbo watakalo lipoteza huku akisisitiza wanaccm kufuata sheria zilizopo kuhepuka migogoro. Alisema ikiwa ccm inajipanga ili kuyalinda majimbo na kata zote wamepata taarifa za baadhi ya wagombea kupita pita kwenye majimbo na katakabla ya muda huku wengune wakitoa fedha na wengine wakidiliki kuwapa mabarozi laki 3 ili waachie nafasi zao na kupatikana mabarozi na wajumbe watakaok...

CCM SONGWE YATOLEA UFAFANUZI SAKATA LA MBUNGE CONDESTER KUMPIGA KOFI KIJANA WA UVCCM AMBAO WALIMGOMEA KUINGIA KIKAONI.

Image
Na Ibrahim Yassin,Momba SIKU Chache baada ya umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (CCM) wilayani Momba mkoani Songwe kuingia kwenye mgogoro baada ya mbunge wa Momba Condester Sichalwe kuzuiliwa kuingia kwenye kikao huku akidaiwa kumpiga kofi mmoja mmoja wa vijana hao,hatimaye ccm mkoa wafanikiwa kumaliza mgogoro huo. Umoja wa vijana (UVCCM) wa jimbo la Tunduma na wa jimbo la Momba walikutana tarehe 19/4/2025 kufanya kikao chao kwenye ukumbi wa shule ya Tunduma TC,yaliibuka nadai ya mbunge Sichalwe wa Momba kumpiga kofi mmoja wa vijana kutoka jimbo la Tunduma kwa madai ya kumzuia kuingia ukumbini. Wilaya ya Momba yenye majimbo mawili yaani la Tunduma linaloongozwa na mbunge David Silinde na jimbo la Momba linaloongozwa na Condester Sichalwe,umoja wa vijana wameingia kwenye mgogoro toka mkunge wa Sichalwe kuzuiliwa kuingia kwenye kikao. Baada ya kuzuka kadhia hiyo,Mwenyekiti wa chipukizi tawi la Nkangamo jimbo la Momba Elisha Sosy alizungumza wazi kuwa hawapo tayari kufanya kazi na wen...
Dfghhhhggg

TAcRI yatakiwa kujikita kwenye utafiti wa afya ya udongo ili kuongeza uzalishaji wa kahawa

Image
                         MAKALA .SERIKALI IWAONGEZEE UWEZO WATAFITI WA UDONGO/MBEGU KUONGEZA TIJA KWA WAKULIMA,MADADIRIKO YABIA YA NCHI YATAJWA. .UONGOZI NA WADAU WA KILIMO WAPAMBANA KUREJESHA HESHIMA YA SONGWE KWENYE ZAO LA KAHAWA,MIKAKATI UGAWAJI MBEGU CHOTARA YAFANA. Na Ibrahim Yassin,Songwe WAKULIMA na wadau wa zao la Kahawa mkoani Songwe wameiomba serikali kupitia taasisi ya utafiti wa Mbegu (TAcRI) kuwawezesha wataalam kufanya tafiti za afya ya udongo ili kuongeza tija ya zao hilo.. Mkoa wa Songwe kupitia wilaya ya Mbozi inashika nafasi ya pili kitaifa kwa uzalishaji wa zao la Kahawa licha ya siku za hivi karibuni uzalishaji wake ulisuasua huku wakulima wakiwa na uhaba wa mbegu. DISMAS Pangalas ni meneja wa kanda wa Taasisi ya utafiti wa Mbegu (TAcRI) licha ya kukiri changamoto ya uhaba wa mbegu,lakini anaeleza mikakati waliojiweka kukabiliana na uhaba huo. Anasema licha ya kuzalisha mbegu nyingi lakini haitoshelezi kwani mwaka jana walizalisha miche Milioni 8 kwa kanda nzima na ...

Askari mstaafu (JWTZ) ajikita kwenye kilimo cha kahawa,awa mfano kwa Wakulima Mbozi

Image
VIJANA ZAIDI YA 100 WAPATA AJIRA ZA MKATABA KUOTESHA MBEGU CHOTORA ZA COMPACT. NZUNDA AWATAKA WAKULIMA WADOGO KUJIFUNZA KILIMO MSETO,SHAMBA LAKE LAWA SHAMBA DARASA. Na Ibrahim Yassin,Songwe ‘’Nimeingia mkataba na taasisi ya utafiti (TAcRI) Nazalisha mbegu chotara nimeajiri vijana 100 wawalipa mshahara,shamba darasa la mazao mchanganyiko lipo wakulima waje kujifunza kiklimo mseto’’ ASKARI wa jeshi la wananchi (JWTZ) mstaafu aliyekuwa kwenye kitengo cha mizinga Chriss Nzunda,ajikita kwenye kilimo cha Kahawa na kutoa wito kwa wakulima kulitumia shmba darasa lililopo shambani kwake ili walime kilimo chenye tija, Nzunda ametoa wito kwa wakulma wadogo na walio kwenye ushirika kufika shambani kwake Kijiji cha Masangula kata ya Nyimbili wilayani Mbozi mkoani Songwe ili waone na kujifunza namna ya kulima mazao mchanganyiko katika shqamba moja. Alisema imezoeleka kuwa wakulima wengi wamekuwa wakima zao moja katika kila heka kumbe kulima mazao mchanganyiko inawezekana,hivyo ili kuondokana na kili...

NGULI WA SIASA NCHINI ALIYESHIKA UDIWANI TOKA 1988 HADI SASA AELEZA ALIVYOIPAMBANIA KATA YA BARA.

Image
                                  MAKALA -aeleza mafanikio ikiwemo kujenga shule za msingi kila kijiji wastafu Rais Kikwete na waziri mkuu Sumaye. ‘’miaka 10 iliyopita wagonjwa wa kata hiyo yenye wakazi 30,000 wakiwemo wajawazito walitibiwa kwa waganga wa tiba za jadi kwa kukosa fedha kwenda wilayani umbali wa kilometa 56’’. Na Ibrahim Yassin, Songwe Diwani wa kata ya Bara iliyopo wilayani Mbozi mkoani Songwe aliyeshika nafasi hiyo toka 1988 hadi sasa Chief Aloyce Mdala vuma amewapongeza wananchi wa kata hiyo kwa kuendelea kumuamini na kushirikiana kuleta maendeleo katika kila sekta. Amesema yeye ni familia ya Kichifu ambapo mwaka 1972 alite uliwa kuwa barozi wa nyumba kumi wakati huo waliwajibika kwenye serikali wakilipwa posho,mwaka 1983 akiwa kiongozi wa umoja wa ccm,ilipofika mwaka 1987 alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa kijiji. Anasema baada ya kufanya kazi kwa uaminifu na utiifu alichag uliwa kuwa diwani lakini aliacha udiwani baada ya kuchaguliwa kuwa mjumbe wa chama kikuu cha ushi...

WAKUFUNZI SCOUT WAJENGEWA UWEZO KUENDANA NA MTAALA MPYA WA ELIMU-ELIMU YA AMALI

Image
Na Israel Mwaisaka,Rukwa WAHITIMU wa mafunzo ya Scout wilaya Nkasi wametakiwa kuitumia elimu waliyoipata katika kuwajenga vijana wa Scout mashuleni Ili yaweze kuwanufaisha katika maisha Yao hasa katika kipindi hiki ambacho kina mtaala mpya wa Elimu ya mafunzo ya amali. Hayo yamesemwa na kaimu afisa elimu sekondari wilaya Nkasi Fortunatus Kaguo alipokuwa akifunga Kambi ya siku Nne ya Scout Wakufunzi katika shule ya sekondari. Nkasi ambapo amedai kuwa wao kama wahitimu Wakufunzi wanayo nafasi kubwa ya kuyatumia mafunzo hayo katika kuwajenga vijana wa Scout na kuwa Watu makini na wenye uwezo mkubwa katika kuchakata masuala mbalimbali ya kimaisha. Amesema kuwa Scout inayo nafasi kubwa ya kumtengeneza kijana kuwa mbunifu na hakiri na kuwa katika kipindi hiki ambacho mtaala mpya wa Elimu unakwenda kufanya kazi wa Elimu ya amali mafunzo ya Scout yanayo nafasi kubwa ya kuwatengeneza vijana. Mkufunzi wa mafunzo kitaifa ALT. Edmak Mwamalala kwa upande wake amesema kuwa wahitimu wa mafunzo hayo...

Mwanafunzi wa kidato cha Nne ajifungua na kumtupa Mtoto chooni

Image
Na Israel Mwaisaka, Rukwa Jeshi la Polisi mkoani Rukwa linaendelea kufanya uchunguzi wa kina juu ya binti ambaye ni Mwanafunzi wa kidato cha Nne (18) wa shule ya sekondari Nkasi ambaye amejifungua mtoto na kumtupia chooni . Akizungumzia tukio Hilo Kamanda wa Polisi mkoani Rukwa Shadrack Masija amesema kuwa wiki iliyopita Mwanafunzi huyo akiwa mjamzito bila ya mtu yeyote kufahamu.. alijifungua mtoto Kisha mtoto huyo kumtupia kwenye choo cha shimo na yeye kuelekea shuleni kuendelea na masomo. Amesema kuwa Watu walisikia sauti za mtoto huyo zikitoka ndani ya choo hicho na taarifa hizo ziliwafikia Polisi ambao walifika eneo la tukio na kumuokoa mtoto huyo ambaye yupo hai Hadi sasa. Amesema kuwa baada uokozi huo uliofanyika mtoto huyo alikimbizwa hospitali kwa ajiri ya matibabu huku wakifanya uchunguzi wa aliyefanya kitendo hicho ndipo walipombaini Mwanafunzi huyo. Kamanda Masija amedai kuwa binti huyo baada ya kuhojiwa alikiri kufanya tukio Hilo na kudai kuwa halifanya hivyo bila ya kujit...

SERIKALI YA ANZA UJENZI VITUO VYA ASKARI WANYAMA PORI -RUKWA

Image
Na Baraka Lusajo,Rukwa Serikali kupitia shirika la hifadhi za Taifa Tanzania TANAPA) imeanza mkakati wa kukabilina na kupambana na wanyama wakali na waharibifu wakiwemo tembo ambao wamekuwa wakisababisha vifo,kujeruhi na kuharibu mazao kwa kujenga vituo vyenye askari wenye mafunzo maalumu na silaha za kukabilina na wanyama katika vijiji 16 vinavyozunguka hifadhi ya mazingira asilia Kalambo mkoani Rukwa. Mapema akiongea wakati wa ziara ya kutembelea maeneo ya hifadhi Kamishina msaidizi mwandamizi wa uhifadhi na mkuu wa Kanda ya Nyanda za juu kusini (TANAPA) ndugu Godwell Ole Meing’ataki,amesema vituo hivyo vinajengwa maeneo yenye changamoto ya wanyama wakali na waharibufu,wakiwemo Tembo ambao wamekuwa wakileta migogoro kwa wananchi wanaoishi jirani na hifadhi. -ACC- GODWELL OLE MEING’ATAKI - MKUU WA HIFADHI ZA (TANAPA) KANDA NYANDA ZA JUU KUSINI. Kwa upande mhifadhi mwandamizi wa wakala wa huduma za misitu Tanzania TFS wilayani Kalambo ndugu Brayson Mkiwa, amesema uwepo wa vituo hivyo ...

Watumishi wa Umma wametakiwa kutunza siri za seriikali na uwajibikaji

Image
Na Baraka Lusajo,Rukwa Katibu tawala mkoani Rukwa Msalika Makungu amewataka watumishi wa umma katika Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo kuzingatia sheria na maadili ya utumishi wa umma kwa kuimarisha ushirikiano na uwazi wakati wa utekelezaji wa majukumu yao mahali pakazi ili kuongeza ufanisi wa kiutendaji. Ameyasema hayo wakati akiongea na watumishi wa umma wilayani Kalambo mkoani Rukwa kupitia ziara yake ya kusikiliza na kutatua changamoto za watumishi mahali pa kazi na kuwataka wakurugenzi mkoani humo kufuata miongozo ya serikali wakati wa utekezaji majukumu yao kwa kuacha kuzalisha madeni ikiwemo kutohamisha watumishi bila uwepo wa bajeti. Aidha ametumia fursa hiyo kuwataka watumishi wa umma kujenga utamaduni wa kuwahi kazini na kuondoka kulingana na muda uliopangwa na serikali na kusisitiza watumishi kuacha tabia ya kutamani kuhama na badara yake wajikite katika kujiimarisha kiuchumi kwa kuazisha shughuli mbliambali za uwekezaji na uzalishaji ambazo zitawawezesha kuongeza vipato vya...

MAAFISA MICHEZO WALIOGOMA KUSHIRIKI MAFUNZO YA MICHEZO YA MPIRA WA MIKONO WAONYWA.

Image
Baraka Lusajo,Kalambo Mkurugenzi mtendaji halmashauri ya Kalambo mkoani Rukwa shafi Mpenda amewaonya maafisa michezo waliogomea kushiriki kozi ya michezo ya mpira wa mikono (handball) licha ya serikali kugharamia ada na fedha za uendeshaji na kuelekeza kuchukuliwa hatua za kinidhamu ikiwemo kujieleza kwa maandishi pamoja na kubadirishiwa majukumu yao ya kazi. Ameyasema hayo wakati akihitimisha kozi ya mpira wa mikono(handball) yaliofanyika wilayani humo kwa kushirikisha maafisa michezo 45 kutoka mikoa ya Rukwa, Songwe, Njombe na Iringa,Kozi iliyofanyika katika shule ya Sekondari Matai na kuwakilishwa na Afisa Utawala na Rasilimali Watu Ndugu Amandus Mtani na kusisitiza maafisa michezo kuzingatia nidhamu na uwajibikaji mahali pa kazi. Aidha amesema serikali itaendelea kutoa vifaa vya michezo ikiwemo mipira na kwamba katika mwaka wa fedha 2025/2026 serikali imetenga fedha kiasi cha shilingi 37,641,760 kwa ajili ya kuimarisha michezo wilayani humo na kusisitiza maafisa michezo kuendelea ...

VIONGOZI WA DINI WAKERWA NA MANENO YA KUSUSIA UCHAGUZI

Image
Na Israel Mwaisaka,Nkasi JUMUIA ya Maridhiano na amani (JMAT) wilayani Nkasi mkoani Rukwa inayoundwa na viongozi wa dini mbalimbali wameitaka jamii kutosikiliza maneno mbalimbali yanayotolewa na baadhi ya watu juu ya kuzuia uchaguzi na kuwa maneno hayo yana madhara makubwa na badala yake watafute namna nzuri na sahihi ya kusuruhisha jambo hilo badala ya kuzuia uchaguzi usiwepo. Akizungumza kwenye kikao chao cha kawaida Mwenyekiti wa jumuia hiyo Sheikh wa wilaya Nkasi Hadhiri Daruweshi amedai kuwa neno la “No reform no election) linaweza kuonekana ni neno dogo na kuwasihi viongozi wa dini katika maeneo yao kuhakikisha wanaijenga jamii wanayoizunguka na kuyakataa maneno hayo ambayo yanaweza kuleta mpasuko mkubwa katika taifa utakapofika wakati wakati wa uchaguzi. Aliwataka wanaoeneza sumu ya kutofanyika kwa uchaguzi kutafuta namna iliyo njema kwa kukaa na serikali kuona namna ya kurekebisha yanayodaiwa ili ifikapo oktoba ya mwaka huu wa 2025,wananchi washirriki uchaguzi mkuu na kuweza...