UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA KUANZA JANUARI 12 MKOANI RUKWA
Na Israel Mwaisaka,Rukwa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi imetangaza ratiba ya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwenye mikoa ya Rukwa, Njombe, Songwe na Ruvuma ambapo zoezi hilo litafanyika kwa siku saba kuanzia tarehe 12 hadi 18 Januari, 2025. Hayo yameanishwa kwenye hotuba ya Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Mhe. Jacobs Mwambegele iliyosomwa kwa niaba yake kwenye mikutano ya Tume na wadau wa uchaguzi iliyofanyika leo tarehe 31 Desemba, 2024 kwenye mikoa ya Rukwa, Njombe, Songwe na Ruvuma. Mhe. Mwambegele ambaye aliwakilishwa na wakurugenzi mbalimbali wa Tume kwenye mikutano hiyo, amesema mikoa hiyo itafanya uboreshaji kwenye mzunguko wa tisa na kwamba tayari Tume imekamilisha uboreshaji kwenye mikoa 19 ambayo ilijumuisha mizunguko nane kati ya mizunguko 13 ambayo imepangwa kukabilisha zoezi hilo nchini. “Leo tupo hapa Rukwa na wenzetu wapo kwenye mikoa ya Njombe, Ruvuma na Songwe ikiwa ni maandalizi ya uboreshaji wa Daftari kwenye m...