BIBI MJANE AMUANGUKIA RAIS DR,SAMIA KUPOKWA MALI ALIZOACHIWA NA MUMEWE IKIWEMO HEKARI 31 ZA ARDHI.
MAKALA APANGA KWENDA IKULU KUONANA NA RAIS DR,SAMIA KUELEZA ANAVYONYANYASIKA JUU YA MALI ALIZOACHIWA NA MUMEWE mjane Mariam Kalupande akizungumza na mwandishi wa habari jinsi ardhi yake inavyotaka kuporwa. Na Israel Mwaisaka WAKATI serikali ya awamu ya sita ikiongozwa na Rais Dr,Samia Suluhu Hassan ikiwaagiza viongozi ngazi zote kuhakikisha inamaliza migogoro ya ardhi nchini,hali hiyo imekuwa tofauti kwa wilaya ya Mbozi mkoani Songwe ambako bibi mjane ananyanyasika juu ardhi zake. Ardhi inathamani kubwa katika kuendeleza maisha ya binadamu ambayo inatumika kwa kujenga nyu mba za biashara ,viwanda,Taasisi ,makazi na kuendesha shughuli za kilimo kwa mazao ya biashara na chakula hivyo endapo inatokea migogoro inaweza kuzuka mapigano na kuhatarisha uhai wa watu. Hali hiyo imeikumba familia ya mzee Leston Kalupande aliyeanzisha taasisi ya kusaidia jamii ambaye kwa sasa ni marehemu ,baada ya kifo chake kumezuaka mgogoro mzito ambapo mdogo wake anadaiwa kunyang’anya mali za taasisi na sasa y...