Posts

Showing posts from November, 2025

Watendaji kata na vijiji waaswa kusimamia amani

Image
Na Israel Mwaisaka,Nkasi Mkuu wa wilaya ya Nkasi Mkoani Rukwa Peter Lijualikali amewataka Maafisa watendaji kata na vijiji kuhakikisha wanasimamia suala Zima la amani katika maeneo yao ili wananchi waendelee kufanya kazi na kujiletea maendeleo. Akizungumza kwenye kikao kilichowajumuisha watendaji hao na viongozi wa kamati ya ulinzi na usalama wa wa wilaya kwenye ukumbi wa Mkurugenzi Mtendaji wa wilaya November 28, 2025, amesema kuwa wao kama viongozi, moja ya jukumu lao kubwa ni kuhakikisha suala zima la amani na utulivu linakuwepo katika maeneo yao, ikiwa ni pamoja na kusimama miradi yote ya maendeleo inayotekelezwa katika kata na vijiiji vyao. Amedai kuwa hivi karibuni Waziri Mkuu Dk.Mwigulu Lameck Nchemba, alitoa agizo la Kila mtumishi wa Umma kuwajibika katika nafasi yake hivyo wao kama watendaji wanalo jukumu la kuhakikisha kuwajibikaji kwa watumishi wanaowaongoza unakuwepo. Aidha Mkuu huyo wa wilaya amewataka watendaji hao kuwatumia watu maarufu katika maeneo yao wakiwemo wazee ...

WATUMISHI WA MAKAO MAKUU OFISI YA MKURUGENZI WAPATIWA ELIMU YA MAGONJWA YA AFYA YA AKILI.

Image
Na Asha Hassan,Nkasi Magonjwa ya afya ya akili ni miongoni mwa magonjwa yanayosababisha msongo wa mawazo kwa watumishi walio wengi, na kusababisha majukumu yao kutoyatekeleza vizuri. Ili kuhakikisha tatizo hilo linadhibitiwa kwa Watumishi, Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Nkasi Mkoani Rukwa Leo Novemba 24,2025 kwakushirikiana na Mtaalamu wa afya ya akili wilayani humo wameandaa mafunzo kwa watumishi wa Halmashauri hiyo ili kukabiliana na tatizo hilo. Akizungumza katika mafunzo hayo Mratibu wa Magonjwa yasiyoyakuambukiza (W) Nkasi Richard Kauzeni amesema kuwa lengo la mafunzo hayo kwa watumishi nikuwaelimisha ili waweze kujua changamoto na athari  za msongo wa mawazo zinatokana na Nini na namna ya kukabiliana nazo mahala pa kazi. Aidha ameongeza kuwa kwa sasa Watumishi wengi wanakabiliwa na tatizo hilo mahala pa kazi, hivyo mafunzo hayo yatawasaidia kutatua tatizo la msongo wa mawazo. Sambamba na hayo ameeleza kuwa changamoto ya msongo wa mawazo kwa watumishi ina...

WAPAKISTAN SABA WASHIKILIWA KWA KUKIUKA MASHARTI YA VIZA

Image
Na Moses Ng’wat, Songwe. Idara ya Uhamiaji mkoani Songwe inawashikilia raia saba wa Pakistan kwa tuhuma za kukiuka masharti ya viza walizopewa walipoingia nchini. Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari, Novemba 22, 2025, Kaimu Afisa Uhamiaji Mkoa wa Songwe, Mrakibu wa Uhamiaji, Rose Mulaga Magesa, amesema watuhumiwa hao ni miongoni mwa raia tisa wa Pakistan waliokamatwa Novemba 18, 2025 katika katika msako maalumu uliofanyika katika mji wa Tunduma, Wilayni Momba. Magesa, alisema masharti ya visa yalielekeza raia hao kwenda jijini Dar es Salaam katika maeneo ya  Mbweni kwa shughuli za matembezi, lakini waliondoka na kufika hadi mkoani Songwe kwa shughuli ambazo hazikuainishwa, huku raia wengine wawili wa nchi hiyo walikamatwa kwa kutokuwa na vibali vya kuingia nchini. Magesa aliwataja waliokiuka masharti ya viza pamoja na namba zao za pasipoti kuwa ni Khizar Hayat (JJ6171151), Muhammad Rehman Rasheed (GU9842383), Muhammad Raza (YB9899821),Araiz Chand (YB9899821), Ahmed Ali (TF1832401),A...

Maafisa ugani Nkasi watakiwa kutoa elimu ya kilimo kwa Wakulima wakati huu wa masika

Image
Na Asha Hassan,Nkasi Afisa kilimo, Mifugo na Uvuvi (W) Nkasi, Mkoani Rukwa Dkt.John S. Tlatlaa amewataka Maafisa Ugani wilayani humo kuendelea Kutoa elimu ya kilimo cha Ufuta na Mbaazi kwa wakaazi wa mwambao wa Ziwa Tanganyika na kata zingine zilizofanyiwa utafiti kwa ajili ya kilimo cha mazao hayo. Akizungumza katika kikao kazi cha maandalizi ya msimu wa kilimo kwa mwaka 2025/2026, kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya (W) Nkasi Novemba 20, 2025, Dkt. Tlatlaa amesema kuwa Halmashauri imekusudia kuendeleza zao la Ufuta na Mbaazi kutokana na fursa za masoko ya mtandao uliopo. "Kama tulivyoahidi kwamba kutakuwa na mashamba darasa kadhaa kama 39 kwa maeneo yote ya kata za mwambao amabayo yataanzishwa kwa mwaka huu katika mazao ya Ufuta kwa hiyo wale Maafisa kilimo wa hizo kata katika maeneo yenu mnapokutana kwenye vikao hata vile vya Kijiji basi muendelee Kutoa elimu ya watu kulima zao la Ufuta lakini pia waandae mashamba ya Ufuta " Aidha amewaomba Maafisa kilimo hao k...

RAIS DKT,SAMIA NI MTU NA NUSU RAIS WA WAKANDARASI WANAWAKE WAZAWA NCHINI

Image
Na Ibrahimu Yassin,Songwe RAIS wa wakandarasi Wanawake wazawa nchini Judith Odunga leo amesemea Rais wa Jamhuri ya mungano wa Tanzania Dkt,Samia Suluhu ni mtu na nusu kutokana na kuwaheshimisha wakandarasi wanawake kwa kuwapa tenda za kujenga miradi ya barabara ambayo awali ilifanywa na wanaume pekee. Odunga amesema wanawanachama 460 nchi nzima ambao wanajihusisha na ujenzi wa miradi mbalimbali ikiwemo ya barabara,madaraja na makaravati ambapo awali baada ya kujisajili walipeleka hoja ya utambuzi kwa Rais Samia wakati akiwa Makamu. Amesema baada ya Rais Dkt,Samia kuwa Rais kamili,alikubali hoja zetu na kuwapatia ujenzi wa barabara kilometa 20 zilizopo mkoani Songwe kama kipimo huku akijinasibu kuishangaza Dunia kwa kujenga barabara yenye viwango vya juu. Amesema ujenzi wa barabara ya Lami kilometa 20 waliyopewa mkataba wake ni wa mwaka mmoja ambapo wao wamejipanga kuikamilisha kabla ya wakati na kwa ubora wakiwa na lengo la kupewa kilometa nyingi Zaidi. ‘’Kulikuwa na hoja kuwa wanawak...

WAKULIMA ILEJE –MBOZI WAMPA 5 RAIS DKT,SAMIA UJENZI BARABARA YA LAMI RUANDA IDIWILI HADI ITUMBA.

Image
Na Ibrahim Yassin,Songwe ‘’Tulilazimika kuuza mazao kwa walanguzi kutokana na barabara kuwa mbovu,ujenzi huu ukikamilika tutaongeza usalishaji na kuuza bei ya juu kwenye masoko ya nje ya mkoa’’ WAKULIMA katika wilaya za Ileje na Mbozi wameipngeza Serikali kwa kuona umuhimu wa kujenga baraara ya Lami katika maeneo yao ambayo ni bingwa kwa kilimo cha mazao mbalimbali na ufugaji ikiwemo upasuaji na usafirishaji wa mbao. Serikali inatekeleza Ujenzi wa barabara ya Ruanda-Nyimbili-Hasamba-Izyila hadi Itumba wa kilometa 76.67 na Mahenje – Hasamba hadi Vwawa-kilometa 31.9 ni barabara iliyounganisha Vwawa na Tunduma ikiwa ni muhimu katika shughuri ya kiuchumi na kijamii. Ujenzi huo ukikamilika utachochea na kuongeza thamani ya kiuchumi hasa kwa wakulima ambao wengi wao wanalazimika kuuza mazao yao kwa bei ya chini kutokana na kushindwa kumudu ghamarama za usafirishaji wa mazao kwenda kwenye masoko yaliyopo nje ya mkoa. Wakizungumza leo kwa nyakati tofauti,wakulima hao,wamesema kwa sasa wameanza...

WANAKIJIJI 240 WAPATA AJIRA KATIKA UJENZI WA BARABARA YA LAMI RUANDA IDIWILI,WASIFU USIMAMIZI WA TANROADS.

Image
Na Ibrahim Yassin,Songwe WANAKIJIJI Zaidi ya 240 wanaozunguka mradi wa ujenzi wa barabara ya Ruanda Idiwili wilayani Mbozi mkoani Songwe wamepata ajira za mikataba za kufanya kazi mbalimbali huku wakipata fedha zinazoendasha Maisha yao ya kila siku. Wakizungumza leo kwa nyakati tofauti katika vijiji hivyo,wamesema ujio wa mradi huo umekuwa ni fursa kwao kwani wamepata ajira na kujipatia kipato huku vijiji hivyo vikiendelea kupanda thamani hasa katika sekta ya ardhi kutokana na watu wengi kununua maeneo ya uwekezaji. Rashford Mtafya mkazi wa Iyura amesema awali viwanja vya kujenga nyumba za makazi vilikuwa vikiuzwa kati ya laki 4 hadi 5 laikini kwa sasa vinauzwa Zaidi ya milioni 2 kutokana na ujio wa barabara hiyo. Jangson Mwamengo mkazi wa Idiwili amesema pindi barabara hiyo itakapo kamilika vyombo vya moto vitaongezeka na nauli zitapungua kwani kwa sasa wanalazimika kutoa nauli isiyorafiki kutokana na changamoto ya barabara. Amesema sambamba na hilo,pia wamefurahi kuona vijana wao wa...

WANANCHI WAWAHARAKISHA WAKANDARASI WANAWAKE WAZAWA KUKAMILISHA MRADI KWA WAKATI.

Image
Na Ibrahim Yassin,Songwe WANANCHI katika vijiji vilivyopo wilaya ya Mbozi na Ileje mkoani Songwe,wamewaharakisha Wakanda rasi wanawake wazawa kukamilisha ujenzi wa barabara kwa wakati wakiwa na uchu wa kukuza uchumi kwenye sekta ya usafirishaji mazao. Wamesema wamejipanga kuhakikisha wanaitumia barabara hiyo kukuza uchumi kwa kusafirisha bidhaa kutoka mashambani kwenda kwenye masoko yaliyopo nje ya mkoa wa Songwe wakitumia barabara hiyo hali iliyopelekea wawe na uchu wakitaka ujenzi ukamilike. Serikali ya Tanzania ilitoa kiasi cha shilingi Bilioni 45 kujenga barabara ya Lami kilometa 20 kuanzia Ruanda hadi Idiwili ikiwa na lengo la kuondoa changamoto ya mindombinu ya barabara na kukuza uchumi kwa jamii. Katika ujenzi huo makampuni manne ya wanawake wazawa walipewa tenday a ujenzi ambapo kila kampuni ilipewa kilometa 5 huku yakiungana kuongeza nguvu ya pamoja kujenga mradi huo ambapo wamejinasibu kukamilisha kabla ya muda uliowekwa. Sehemu ya kwanza ya ujenzi ni Ruanda -Idiwili  ikijeng...

WANANCHI WAWAHARAKISHA WAKANDARASI WANAWAKE WAZAWA KUKAMILISHA MRADI KWA WAKATI.

Image
Na Ibrahim Yassin,Songwe WANANCHI katika vijiji vilivyopo wilaya ya Mbozi na Ileje mkoani Songwe,wamewaharakisha Wakanda rasi wanawake wazawa kukamilisha ujenzi wa barabara kwa wakati wakiwa na uchu wa kukuza uchumi kwenye sekta ya usafirishaji mazao. Wamesema wamejipanga kuhakikisha wanaitumia barabara hiyo kukuza uchumi kwa kusafirisha bidhaa kutoka mashambani kwenda kwenye masoko yaliyopo nje ya mkoa wa Songwe wakitumia barabara hiyo hali iliyopelekea wawe na uchu wakitaka ujenzi ukamilike. Serikali ya Tanzania ilitoa kiasi cha shilingi Bilioni 45 kujenga barabara ya Lami kilometa 20 kuanzia Ruanda hadi Idiwili ikiwa na lengo la kuondoa changamoto ya mindombinu ya barabara na kukuza uchumi kwa jamii. Katika ujenzi huo makampuni manne ya wanawake wazawa walipewa tenday a ujenzi ambapo kila kampuni ilipewa kilometa 5 huku yakiungana kuongeza nguvu ya pamoja kujenga mradi huo ambapo wamejinasibu kukamilisha kabla ya muda uliowekwa. Sehemu ya kwanza ya ujenzi ni Ruanda -Idiwili  ikijeng...

Maafisa maendeleo ya jamii Nkasi wakabidhiwa Pikipiki

Image
‎ Na Israel Mwaisaka, Nkasi ‎ ‎Halmashauri ya wilaya Nkasi mkoani Rukwa imekabidhi pikipiki mbili kwa Maafisa maendeleo ya jamii ngazi ya kata kwa lengo la kurahisisha majukumu yao ya kuwahudumia Wananchi. ‎ ‎Akikabidhi Pikipiki hizo kwa Maafisa maendeleo ya jamii wa kata za Kizumbi na Ninde kaimu mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya Nkasi Valeriana Mwampasi amewataka Maafisa hao kuzitunza vyema Pikipiki hizo na kuzielekeza kwenye matumizi sahihi Ili ziweze kutoa huduma kwa Wananchi wanaoishi katika kata hizo. ‎ ‎Amesema kuwa lengo la wizara ya maendeleo ya jamii na makundi Maalum kutoa Pikipiki hizo ni kutaka jamii ifikiwe kwa haraka na uhakika hivyo Ni muhimu kwa Pikipiki hizo kutunzwa vyema Ili ziweze kutoa huduma kwa jamii kwa muda mrefu. ‎ ‎Awali Afisa maendeleo ya jamii wilaya ya Nkasi jumaa AweSo amezitaja kata hizo Kama zilizo katika mazingira magumu na ndiyo maana walionelea wapewe Pikipiki hizo Ili ziwarahisishie kazi zao kwa kuweza kuwafikia Wananchi wengi zaidi. ‎Hi...