Posts

Showing posts from February, 2026

Skauti waadhimisha kuzaliwa kwa mwanzilishi wa Skauti duniani kwa kupanda miti na matendo ya huruma

Image
‎ Na Israel Mwaisaka,Rukwa ‎ ‎Katika kuadhimisha kumbukizi ya kuzaliwa kwa mwanzilishi wa Skauti duniani Sir Roberth Barden Powell Skauti mkoa Rukwa wameiazimisha siku hiyo kwa kupanda miti na kufanya matendo ya huruma katika hospitali ya Wilaya Nkasi. ‎ ‎Akiongoza zoezi hilo Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya Nkasi ambaye pia Afisa uhamiaji wa Wilaya Nkasi Mrakibu mwandamizi Aloyce Fuko alisifu Wazo hilo kwani linaenda sambamba na matamanio ya Rais Dkt,Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha tunakabiliana na mabadiliko ya tabia Nchi kwa kupanda miti. ‎Alisema kuwa kutokana na shughuli nyingi za kibinadamu miti mingi imekua ikikatwa na kutuweka katika mazingira hatarishi yanayotokana na uharibifu huo wa mazingira na kuwa kitendo Cha Skauti Cha kuja na Wazo hilo katika kukumbuka mwanzilishi wa Skauti duniani ni kulitendea haki taifa. ‎ ‎Awali kamishina wa Skauti mkoa Rukwa Hassan Kikoloma alisema kuwa licha ya zoezi hilo la kupanda miti pia watawatembelea wagonjwa wa hospitali ya wilaya Nkasi na ...

Ukarabati wa uwanja wa ndege wa Sumbawanga wafikia asilimia 96

Image
‎ Na Israel Mwaisaka,Rukwa ‎ ‎Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Mwakiposa Kihenzile, ametoa wito kwa sekta binafsi na makampuni ya ndege kuwekeza katika huduma za usafiri wa anga. ‎ ‎ Kihenzile ametoa wito huo Jana Februari 21, 2026 akiwa mkoani Rukwa, ambapo amekagua hatua mbalimbali za maendeleo ya ukarabati wa Kiwanja cha Ndege cha Sumbawanga. ‎ ‎Naibu Waziri huyo alieleza kuwa Serikali inaendelea kuboresha viwanja vya ndege ili kuimarisha miundombinu ya sekta hiyo. ‎ ‎Aidha ameeleza kuwa wito huo unalenga kupunguza changamoto zilizopo na kufungua fursa zaidi za kiuchumi kwa wananchi na wawekezaji. ‎ ‎Akitoa taarifa ya maendeleo ya kazi ya ukarabati, Kaimu Meneja wa TANROADS Mkoa wa Rukwa na msimamizi wa mradi huo, Mhandisi Joseph Jemonge, amebainisha kuwa kiwanja hicho kimefikia asilimia 96 ya ukamilishaji, huku kazi zilizobaki zikihusisha hatua za mwisho kabla ya kuanza kutumika rasmi. ‎ ‎Naibu Waziri pKihenzile amesisitiza umuhimu wa kukamilika kwa wakati kwa kazi zilizobakia ili ...
Wwwwe
Xhhhh

Madiwani Nkasi watakiwa kubadilika baada ya mafunzo

Image
Na Israel Mwaisaka,Nkasi ‎ ‎MADIWANI wametakiwa kubadilika kwa kufanya kazi kisasa baada ya kupata mafunzo ya kiuongozi yaliyotolewa na chuo Cha Serikali za mitaa Hombolo. ‎ ‎Hayo yamesemwa leo Februari 21,2026 na Mwakilishi wa Katibu tawala wa mkoa Rukwa Vaileth Shirima alipokuwa akifunga mafunzo ya tatu kwa Madiwani wa halmashauri ya Wilaya Nkasi. ‎ Amesema kuwa mafunzo hayo waliyoyapata yakawaimarishe kiutendaji na kuwa wapya kwa kuongeza nguvu katika kuwahudumia Wananchi waliowachagua. ‎ ‎Alidai kuwa Madiwani wapya ni wengi ukilinganisha na waliorudi katika awamu hii nyingine hivyo anatarajia kuona wote wanajua wamoja na kuhakikisha majukumu Yao hayaingiliani na ya Watu wengine ili kuondoa migongano inayoweza kuzalisha migogoro isiyokuwa ya lazima. ‎ ‎ Mashaka Makuka afisa tawala mwandamizi OWM-TAMISEMkwa upande wake amesema kuwa Imani yake ni kuwa mafunzo hayo waliyoyapata yatakwenda kuibadili halmashauri kwa kuiwezesha kuwa bora zaidi na Kutoa huduma stahiki kwa Wananchi. ‎ Al...

NKASI YAJIPANGA NA MASHINDANO YA LIGI YA WANAWAKE DARAJA LA TATU NGAZI YA MKOA

Image
‎ Na Israel Mwaisaka, Nkasi ‎ ‎Wilaya Nkasi mkoani Rukwa inajiandaa kuwa mwenyeji wa mshindano ya mpira wa miguu kwa Wanawake ligi daraja la tatu huku maandalizi yakiwa hatua za mwisho. ‎Akizungumza na Majira katibu wa chama cha mpira wa miguu wilayani Nkasi (NFA) Michael Charahani amedai kuwa mashindano hayo yanatarajia kuanza mwezi Marchi ya mwaka huu. ‎ ‎alisema kuwa wilaya Nkasi ambayo inatarajia kuwa mwenyeji wa mashindano hayo itapeleka timu tatu ambazo ni Nkasi Queens, Chala Princess na Kirando Queens. ‎ ‎Charahani amedai kuwa wao kama wenyeji wa mashindano hayo wamekamilisha karibia maandalizi yote na viwanja viwili vinatarajia kutumika katika mashindano hayo. ‎ ‎amevitaja viwanja hivyo kuwa ni uwanja wa Sabasaba mjini Namanyere ikiwa ni pamoja na uwanja wa shule ya sekondari Nkasi na kuwa Sumbawanga Manispaa na wilaya ya Kalambo zinatarajia kupeleka timu zao wilayani Nkasi ili kuweza kushiriki mashindano hayo. ‎ ‎katibu huyo wa NFA amefafanua kuwa licha ya maandalizi ha...

Watumishi wawili halmashauri ya Nkasi wafukuzwa kazi kwa utovu wa nidhamu

Image
Na Israel Mwaisaka, Nkasi ‎ ‎Baraza la madiwani Wilayani Nkasi Mkoani Rukwa, limewachukulia hatua za kinidhamu watumishi wawili wa kada ya Afya kwa kuwafukuza kazi kwasababu ya utoro wa muda mrefu katika vituo vyao vya kazi ‎ ‎Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa kikao cha Mashauri ya kinidhamu kilichoketiwa na madiwani hao, Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Richard Leonard Masai alisema wamejiridhisha na taarifa za watumishi hao za kuwa watoro wa muda mrefu katika maeneo yao yakazi, hivyo wanakila sababu ya kuwafukuza kazi ili iwe fundisho kwa wengine. ‎ Watumishi waliofukuzwa kazi ni Lyangawe Charles Lutu muuguzi daraja la II kituo cha afya Kirando na Gaudensia Fredrick Lukago muuguzi msaidizi daraja II kituo cha afya Kabwe. ‎ ‎Pia Baraza hilo la madiwani , jana limepitisha mapendekezo ya rasimu ya mpango na bajeti ya Halmashauri hiyo kwa Mwaka wa fedha 2026/2027 ambapo Halmashauri inakadiria kukusanyana na kutumia jumla ya shilingi billion 47.3. ‎ ‎Akiwasilisha mapendekezo ya ras...

Bodaboda Nkasi wakabidhiwa refrector za Takukuru kuchagiza mapambano dhidi ya rushwa

Image
Na Israel Mwaisaka, Nkasi ‎ ‎Katika jitihada za kupambana na vitendo rushwa taasisi ya Kuzuia na Kupambana rushwa (TAKUKURU) wilayani Nkasi mkoani Rukwa imekabidhi reflector kwa Madereva wa Bodaboda zenye ujumbe mahususi juu rushwa. ‎ ‎Akizungumza kwenye hafla fupi ya kukabidhi vifaa hivyo afisa Mchunguzi Mkuu wa TAKUKURU wa Wilaya Nkasi Fauzi Mponda amesema kuwa wameamua kukabidhi reflector hizo kama njia mojawapo ya kufikisha ujumbe kwa jamii na kueleza ubaya wa vitendo vya rushwa katika jamii. ‎ ‎Amesema kuwa Bodaboda ni moja ya kundi kubwa katika jamii na kwamba na wao ni moja ya washawishiwa Kutoa rushwa hivyo ujumbe uliopo kwenye reflector hizo utapelekea kukumbuka kuwa nao wapo kwenye mapambano dhidi ya rushwa. ‎ Mkuu wa Wilaya Nkasi Peter Lijualikali kwa upande wake amewataka Bodaboda hao wakawe mabalozi wema katika vita hiyo dhidi ya rushwa na kuwa mstari wa mbele kukataa vitengo vyoyote vya rushwa iwe ni Kutoa Wala kutokea rushwa. ‎ ‎Amesema kuwa rushwa ina madhara makubwa ...

Watoto wawili wafariki kwa kusombwa na maji wakitoka kuchunga mifugo

Image
Na Israel Mwaisaka,Nkasi ‎ ‎Watoto wawili wa vijiji vya Kasu " A" na Kasu "B" wamefariki Dunia baada ya kusombwa na maji ya mto Mtoze walipojaribu kuuvuka walipokuwa wakirudi kutoka katika jukumu la kuchunga Ng'ombe. ‎ ‎Wakizungumzia tukio hilo wenyeviti wa vijiji hivyo Filbert Teofilo wa kijiji Cha Kasu "B" na Edwin Mpokezi wa Chala " A" ni kuwa tukio hilo limetokea Juzi Februari 3,2026 majira ya saa 12 jioni wakati Watoto hao walipokuwa wakirejea nyumbani na mifugo wakitoka marishoni. ‎ ‎Wamesema kuwa wakati wakivuka mto huo ghafla maji mengi yalifulika katika mto huo kutokana na mvua nyingi zilizokuwa zikinyesha na kupelekea mto huo kutiririsha maji mengi na kuwasomba Watoto hao ambao hadi Sasa hawajapatikana ‎ ‎Afisa mtendaji wa kijiji Cha Chala "A" Faraja Mwakyembe amewataja Watoto hao waliofariki kuwa ni Michael Kanyepo (6) na Haroun Kifunda (15) ‎ ‎Amedai kuwa toka Jana walipiga mbiu na kuwataka Wananchi wote wa Kasu kuing...