Posts

Showing posts from June, 2024

Wafungwa jela maisha kwa kosa la ubakaji

Image
Na Israel Mwaisaka, Nkasi MAHAKAMA ya wilaya Nkasi Mkoani Rukwa imemhukumu kifungo Cha maisha jela Kelvin Pungama (23) mkazi wa Kijiji Cha Karundi Kwa kosa la kumbaka mtoto wa miaka Minne wa darasa la awali katika shule ya msingi Fyengerezya. Akitoa hukumu hiyo leo hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya wilaya Nkasi Adamu Mwanjokolo amesema anamtia hatiani mtuhumiwa chini ya kifungu Cha sheria (130) na (2) (e) na 131 (1) na (3) Cha kanuni ya adhabu sura ya 16 marejeo ya mwaka 2022 ni baada ya mahakama kuridhishwa na maelezo na ushahidi uliotolewa upande wa jamuhuri pasipo kuacha shaka yoyote Awali upande wa mashitaka ukiongozwa na Waendesha mashitaka wa serikali Irene Mwabeza na Cedric Mashauri waliieleza mahakama hiyo kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo Septemba 5,2023 katika Kijiji Cha Karundi ambapo mtoto huyo alikwenda kumsalimia Dada yake na wakati wakiwa shambani alimuacha mtoto huyo nyumbani na ndipo kijana huyo alipomshika na kumpeleka chumbani kwake na kuanza kumbaka. Waendesha ...

TAKUKURU Nkasi yataka ushirikiano kukabiliana na vitendo vya rushwa

Image
Na Israel Mwaisaka,Nkasi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) wilaya Nkasi mkoani Rukwa Shem Mgaya amewataka Wananchi kushirikiana na taasisi hiyo katika kutoa taarifa mbalimbali ya vitendo vya rushwa. Amesema kwamba mapambano dhidi ya Rushwa yanawategemea sana Wananchi wenyewe kutoa taarifa na wao kazi yao ni kuzifanyia kazi taarifa hizo na kubwa kwao ni kutaka kukabiliana na vitendo hivyo vya rushwa. Amesema kuwa ofisi ya Takukuru wilaya Nkasi ipo wazi wakati wote na kuwataka Wananchi kuitumia ofisi hiyo kutoa taarifa sahihi juu ya rushwa ili kuweza kutokomeza vitendo hivyo vya rushwa ambavyo vimekua vikitatiza watu kupata haki zao wanazozistahili Akizungumza na Wananchi wa kijiji cha Katongolo kata ya Kipili jana kwenye ziara ya mkuu wa mkoa Rukwa Charles Makongoro Nyerere alipokuwa akisikiliza kero za Wananchi mkuu huyo wa Takukuru alilitumia jukwaa hilo kutoa elimu ya rushwa na kuomba ushirikiano wa kutosha katika kukabiliana na rushwa. Shemu Mgaya amesisi...

MBARONI KWA KUMTUPA MTOTO CHOONI BAADA YA KUJIFUNGUA

Image
Na Israel Mwaisaka,Rukwa Jeshi la Polisi Mkoani Rukwa linamshikilia Mwanamke mmoja aliyefahamika Kwa jina la Anifa Mwanawima (36) mkazi wa Kijiji Cha Mashete wilayani Nkasi Kwa kosa la kumtupa mtoto wake chooni baada ya kujifungua. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi mkoa Rukwa Shadrack Masija ni kuwa tukio Hilo limetokea Jana baada ya kubainika kuwa mtoto mchanga ametupwa chooni kutokana na harufu Kali iliyokuwa ikitokea chooni ambapo Mama mwenye nyumba alitoa taarifa Kwa majirani zake ikiwa ni pamoja na Kwa viongozi wa Kijiji. Amesema kuwa kufuatia hari hiyo baada ya kujiridhisha kuwa kilichopo ndani ya choo ni mtoto walitoa taarifa Polisi ambao walishirikiana kuiopoa maiti ya kuchangia huyo kutoka ndani ya choo Huku ikiwa umeharibika na kutoa harufu Kali. Kamanda Masija amesema kuwa baada ya uchunguzi wa haraka ilibainika kuwa alikuwepo Mwanamke aliyekua mjamzito aliyekua akiishi katika nyumba hiyo lakini walipomtizama hawakuuona tena ujauzito na kumtilia shaka na...

Halmashauri ya Kalambo yapata hati safi kwa miaka mitano mfululizo

Image
Na Israel Mwaisaka,Rukwa Mkuu wa mkoa wa Rukwa Makongoro Nyerere ameipongeza halmashauri ya Kalambo kwa kupata hati inayoridhisha kwa kipindi cha miaka mitano mfululizo na kumtaka mkurugenzi mtendaji halmashauri hiyo Shafi Mpenda kuhakikisha fedha zote zinazo kusanywa zinawasilishwa benk kwa wakati Ameyasema hayo kupitia kikao cha baraza la madiwani la halmashauri ya Kalambo kuhusu utekelezaji wa hoja za ukaguzi na mapendekezo ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali kwa mwaka 2022/2023 kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri ya Kalambo, ambapo alipiga marufuku halmashauri kutumia fedha mbichi na kuagiza hatua dhidi ya watumishi waliotumia fedha mbichi na kufanya udanganyifu kuchukuliwa hatua za kinidhamu na kisheria. ‘’Vilevile katika ufuatiliaji uliofanywa na mkoa umebaini kuwa yapo mapato katika mfumo wa LGRCIS yaliyokusanywa na watendaji wa halmashauri katika kipindi cha mwaka 2022 hadi 2023 kiasi cha shilingi 243,458,600 ambayo hayajawasilishwa benk hadi sasa "N...

DC NKASI APONGEZWA KWA UTEKELEZAJI MZURI WA ILANI YA CCM

Image
Na Israel Mwaisaka ,Nkasi Kamati ya siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Nkasi imempongeza mkuu wa wilaya Nkasi Peter Lijualikali Kwa namna anavyosimamia utekelezaji wa ilani ya CCM . Pongezi hizo zimetolewa Jana na Mwenyekiti wa CCM wilaya Nkasi Ally Sud Kessy akiwa na kamati ya siasa ya wilaya kwenye ukaguzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na serikali wilayani Nkasi. Alifika hatua hiyo baada ya kuukagua mradi wa maji Namanyere unaotekelezwa na mamlaka ya maji mjini Namanyere NAUWASA ambapo utekelezaji wake unaenda vizuri na mkuu wa wilaya kuonekana kuufahamu sana mradi huo na hiyo ni kutokana na namna anavyoufuatilia utekelezaji wake. Kamati hiyo ya siasa licha ya kuukagua mradi huo wa maji pia waliukagua mradi wa ujenzi wa daraja la Kipundukala,ujenzi wa kituo Cha afya Kabwe,daraja la Nangulukulu -Korongwe na mradi wa maji Korongwe unaotekelezwa na mamlaka ya maji mjini na vijijini RUWASA ambapo miradi yote ikionekana kutekelezwa vizuri na kutoa pongezi hizo...

Mdau wa maendeleo achangia Mil.1 kuvuta maji shuleni na ukarabati wa Bweni

Image
Na Ibrahim Yassin,Songwe MDAU wa maendeleo mkoani Songwe Ombeni Nanyaro ametoa kiasi cha Ths,Milioni 1 kianzio zinazotumika kuvuta maji ya kukarabati bweni la wanafunzi wa shule ya sekondari Kamsamba wilayani Momba mkoani Songwe. Nanyaro ametoa kiasi hicho cha fedha baada ya kufanya ziara kuite mbelea shule hiyo inayomilikiw a na jumuiya ya wazazi (CCM) baada ya kuona wanafunzi wakitembea kilometa 3 hadi mtoni kusaka maji ambayo hata hivyo si safi na salama. Akizungumza leo  mara baada ya kutoa fedha hizo amesema ameona jinsi watoto wanavyo tembea umbali mrefu kusaka ma ji mtoni na kuamua kuwaita mafundi kuvuta maji na kutoa mifuko ya saruji na mchanga kwa ajili ya ukarabati wa bweni. Nanyaro ambaye pia ni mjumbe wa bodi ya shule hiyo na pia ni mjumbe wa mkutano mkuu ccm mkoa amesema tayari ameunga nisha maji safi na wanafunzi wameanza kuyatumia. Mbali na uwekaji wa maji hayo pia amesema mpango uliopo ni kunu nua vitanda na mago doro ikiwemo kulikarabati bweni la wana funzi kwani lime...

STAMICO YAJINASIBU KUKUSANYA BILIONI 4.147 BAADA YA KUFUNGA MITAMBO MIPYA.

Image
Na Ibrahimu Yassin,Songwe SHIRIKA la madini (STAMICO) linalochimba madini ya makaa ya mawe kupitia mlima Kabulo limejinasibu kukusanya Bilioni 4.147 kwa mwezi baada ya kufunga mitambo mipya huku wananchi wanaozunguka mgodi huo wakianza kunufaika.. Shirika hilo baada ya kusimama kutoa huduma miaka ya nyuma limeanza tena kufanya kazi ya uzalishaji kwa kufunga mitambo mipya inayorahisisha kuchakata makaa ya mawe tani za kutosha. Baada ya mgodi huo kuanza kuzalisha kwa kasi jitihada mbalimbali za kuuboresha mgodi huo zimeanza na hata viongozi mbalimbali wa kitaifa,kimkoa na kiwilaya wamekuwa wakiutembelea mradi huo na no kuona kasi ya uzalishaji. Ombi kubwa la wadau wa maendeleo ni kuona majengo pia yakiboreshwa kwani yamechakaa licha ya awali majengo hayo yakiwa katika ubora picha zake zilitumika kwenye baadhi ya noti za kitanzania ikiwemo noti ya Tsh,1,000. Siku za hivi karibuni,Mkuu wa mkoa Songwe Daniel Chongolo alifanya ziara ya kuutembelea mgodi huo akiwa na timu nzima ya usalama ya ...

Auawa kwa kuchomwa na moto polisi wahaha kubaini chanzo

Image
Na Ibrahimu Yassin,Songwe KIJANA mmoja ambaye hajafahamika mara moja, amekutwa ameuawa na mwili wake kutupwa na kuchomwa moto kitongoji cha Mpakani karibu na reli ya TAZARA Kata ya Hasanga,Mbozi mkoani Songwe usiku wa kuamkia leo.. Watu walioshuhudia leo asubuhi kwa kuukuta mwili wamesema kijana huyo ameungua maeneo ya mwili mzima na kwamba upo uwezekano kwamba aliuawa kwanza kabla ya kuchomwa moto. Diwani wa Kata ya Hasanga  Malick Nzowa amefika eneo la tukio na kuthibitisha tukio hilo. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Augustino Senga amedhibitisha kuwepo kwa tukio hilo na kisema analaani kitendo cha watu kujichukulia sheria mkononi. Amesema kitendo cha watu kuchukua sheria mkononi kwa kuua ni kosa na aliyehusika akikamatwa atashitakiwa kwa mauaji."Tumekuwa tukitoa elimu mara kwa mara maeneo mbalimbali mkoani hapa. Matukio ya mauaji yamekithiri hivyo bado tunakazi kubwa kuhakikisha tunatoa elimu watu waache vitendo viovu" amesema kamada Senga. Hata hivyo kamanda Senga a...

RAIS -DKT,SAMIA AWAFUTA MACHOZI WACHIMBAJI WADOGO AKIWAONDOLEA KERO SUGU

Image
                        MAKALA VITALU 19  VYA UCHIMAJI DHAHABU VYALETA UNAFUU WA MAISHA KUPUGUZA VITEDO VYA UHALIFU WILAYANI SONGWE ZAIDI ya vijana 12,000 kutoka Wilaya ya Songwe Mkoani Songwe wamepata fursa ya ajira katika migodi ya wachimbaji wadogo na wa kati baada ya Serikali kugawa vitalu 19 kwa wachimbaji huku ikilezwa kuwa vimechochea ukuaji wa uchumi pamoja na kupunguza migogoro na uhalifu katika jamii ya wachimbaji,,anaripoti Ibrahim Yassin,Songwe. Wachimbaji wa dogo ni nguzo muhimu katika sekta ya madini wanaoingiza pato kubwa kwenye bajeti ya serikali na kuwezesha vijana kujiajili,lakini licha ya umuhimu huo vijana hao walisahaulika na hata kero zao hazikupata kutatuliwa. Akizungumza leo Juni 16/2024 mwenyekiti wa wachimbaji wadogo mkoa wa kimadini Emmanuel Kamaka anasema upatikanaji wa maeneo ya uchimbaji ilikuwa ni changamoto na kwamba wakati wa utawala wa Hayati Dkt,Magufuli Rais Dkt,Samia akiwa makamu wake alifika wilayani humo kusikiliza kero. Amesema hata walipoenda Da...

Wenyeviti wa vijiji wapewa wiki mbili kuwasomea Wananchi Mapato na matumizi

Image
Na Israel Mwaisaka,Rukwa MKUU wa wilaya Nkasi Peter Lijualikali ametoa wiki mbili toka sasa kwa viongozi wa vijiji kuhakikisha kuwa wanaitisha mikutano mikuu ya vijiji na kuwasomea Wananchi mapato na matumizi kabla ya kuufikia uchaguzi wa serikali za mitaa mwishoni mwaka huu. Agizo hilo amelitoa jana kwenye kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika kwenye ukumbi wa halmashauri ambapo ameda kuwa ni lazima wenyeviti wa vijiji na watendaji wa vijiji kuhakikisha wanawasomea Wananchi mapato na matumizi ya vijiji vyao ili wananchi weweze kujua maendeleo ya vijiji vyao. Hivyo amewaagiza Maafisa tarafa na watendaji wa kata kuhakikisha katika maeneo yao wanayoyaongoza wenyeviti wote wa vijiji wawe wameitisha mikutano mikuu ya vijiji na kuwasomea wananchi mapato na matumizi. Alidai kuwa mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi ni vyema kabla ya kuingia kwenye uchaguzi Wananchi wakayajua mapato yao ikiwa ni pamoja na kujua mipango endelevu ya Kijiji chao na kutokufanya hivyo kutawaacha Wananchi na sintof...