Posts

Showing posts from June, 2025

KATIBU MKUU UMOJA WA SHULE ZA SEKONDARI NCHINI ACHUKUA FOMU YA UBUNGE.

Image
''Kugombea ni haki ya kila mtanzania,hivyo nimetia nia ya ubunge kuomba ridhaa kwa chama,nina malengo makubwa ya kuipaisha Mbozi kiuchumi,kuweka mikakati endelevu kwenye zao la Kahawa'' Na Ibrahim Yassin, Songwe Katibu mkuu wa Umoja wa wakuu wa Shule za Sekondari Tanzania Bara na kada lia lia wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Frank Ndile amechukua fomu ya kuomba kuteuliwa na Chama hicho kugombea nafasi ya ubunge Jimbo la Mbozi Mkoani Songwe. Ndile leo June 29,2025 amefika katika ofisi za chama hicho zilizopo wilaya ni Mbozi Mji wa Vwawa mkoani hapa na kukabidhiwa fomu na katibu wa chama hicho wilaya ya Mbozi Julius Mbwiga. Ndile ambaye pia ni meneja wa shule za sekondari Kanan amesema amewiwa kuchukua fomu kugombea ubunge Jimbo la Mbozi kwa lengo la kuwatumikia wananchi ikiwepo kutatua chagamoto zilizopo. katibu wa ccm wilayani Mbozi yenye majimbo mawili Julius Mbwaga akimkabidhi fomu ya kugombea Frank Ndile aliyevaa kofia.katika ofisi za ccm wilayani humo. Alizitaja changam...

NKASI YAPATA HATI SAFI RC MAKONGORO APONGEZA

Image
Na Israel Mwaisaka,Rukwa MKUU wa Mkoa Rukwa Charles Makongoro Nyerere ameipongeza halmashauri ya Wilaya ya Nkasi kwa kupata hati safi na kuwa hicho ni kielelezo cha ushirikiano mzuri kati ya watendaji wa halmashauri ,madiwani na wadau wengine katika kuona halmashauri inasonga mbele. Pongezi hizo amezitoa leo Juni 11,2025 kwenye kikao maalumu cha Baraza la Madiwani kuhusu utekelezaji wa hoja za ukaguzi na mapendekezo ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali kwa mwaka 2023-24 ambapo amesema kuwa katika msimu uliopita kulikua na hoja nyingi za ukaguzi lakini kwa sasa zimepungua mno na kuona kwamba kuna kitu kinafanyika ndani ya halmashauri. Amesema kuwa amefurahishwa na namna ambavyo imekuwa ikijishughulisha na ufutaji wa hoja mbalimbali zilizojitokeza kwa kutolea mfano kuwa kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Aprili 2025 halmashauri ya wilaya Nkasi ilionyesha kuwa na hoja za miaka ya nyuma 21 na hivyo kufanya kuwa na hoja 38 na maagizo 4 yenye vipengele 10 ya kamati ya kudumu y...

WAKILI AJITOSA KUGOMBEA UBUNGE KALAMBO

Image
Na Peti Siame,Rukwa WAKILI,Fortunatus Mpangamila Sichone (45) ametangaza rasmi nia ya kugombea ubunge jimbo la Kalambo lililopo mkoani Rukwa katika uchaguzi Mkuu ujao kupitia CCM. Mbunge wa Jimbo hilo ni Josephat Kandege. Sichone ambaye ni Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Mkoa kupitia Jumuiya ya Wazazi ,akizungumza na HabariLEO alisema kuwa ameamua kugombea ubunge jimbo la Kalambo baada ya kuona hali ya maendeleo ya jimbo hilo ikiwa siyo nzuri kwa miongo kadhaa. " Nimekuwa na ndoto ya kuwakilisha wananchi bungeni tangu nikiwa mtoto miaka 30 iliyopita .... Jimbo la Kalambo lina changamoto kadhaa kubwa ni migogoro ya ardhi imekuwepo tangu nikiwa mdogo hadi sasa " anasisitiza. Aliongeza kuwa wakati ukifika atachukua na kujaza fomu za kugombea ubunge katika Jimbo la Kalambo akisisitiza kuwa atatumia taaluma yake ya Sheria kusaidia kusuluhisha migogoro ya ardhi inayowakabili wananchi wa Jimbo hilo kwa miaka mingi.