Mradi wa maji Myunga kunufaisha watu 5,000 kuepuka kunywa maji yaliyochanganyikana na mizoga
Meneja wa Ruwasa mkoani Songwe Charles Pambe akiwa kwenye moja ya miradi ya maji wilayani Momba,(Picha na Ibrahim Yassin
Na Ibrahim Yassin,Momba
‘’Tulikunywa maji ya mto yaliyopo kilometa 3 kutoka hapa,yaliyochanganyi kana na vinyesi,mizoga kwa muda mrefu,tuliuguma homa za matumbo na kuharisha,Rais Dkt,Samia ametukomboa tutaulinda mradi huu’’
WAKAZI Zaidi ya 5,000 wa vijiji vilivyopo kata ya Kapele wilayani Momba mkoani Songwe,wamehepuka na na kadhia ya kunywa maji ya mto Momba yaliyochanganyikana na mizoga ya Wanyama baada ya serikali kujenga mradi wa maji safi na salama.
Wilaya ya Momba ni moja ya wilaya iliyokuwa ikikabiriwa na uhaba mkubwa wa maji safi kwa miaka ya nyuma hali iliyowalazimu kunywa maji ya kwenye madimbwi Pamoja na mifugo,lakini ujio wa Rais Dr,Samia wamehepukana na kadhia hiyo.
Consolata Sikamanga mkazi wa Kijiji cha Myunga jana alisema awali walikuwa wakitembea umbali wa kilometa 3 hadi kwenye mto Momba,maji ambayo yalichanganyikana na vinyesi,mizoga watu walifua visepe na maji hayohayo waliyatumia kupikia na kunywa.
Joliti Simpasa mkazi wa Kijiji hicho alisema serikali imefanya kazi kubwa kuwajengea kisima,ilikuwa kazi kubwa kubeba maji mtoni kwenda nayo zahanati,tuliugua homa za matumbo ikiwemo kuhara kwa kunywa maji yenye vinyesi na mizoga iliyooza.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Myunga Abia Sichone alisema siku mradi wa kisima ulipokamilika na kuanza Kutoa maji walifanya sherehe na kuimba nyimbo za kumsifu Rasi Dkt,Samia,wameondokana na kadhia ya kunywa maji machafu kwani kisma hicho kimekuwa ni moarobaini kwao.
Hata hivyo mwenyekiti huyo,alieleza kuwa kutokana na Jiografia ya kata hiyo wanaomba waongezewe kisima kingine kwani watu waliopo ni wengi ukichukulia wanavituo vya kutolea tiba shule na chou ambavyo vinahitaji maji mengi.
‘’Siku tuliyozindua maji hayo walipanga kuchangia Tsh,50 kwa kila ndoo ya lita 20 .siku hiyo zilipatikana Tsh,100.000 ambazo kupitia kamati iliyochaguliwa na Kijiji fedha hizo zinatunwa benki kwa ajili ya kurekebisha miundombinu pindi itakapoharibika’’alisema Sichone.
Meneja wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira (RUWASA) mkoani Songwe, Mhandisi Charles Pambe alisema kisima hicho ni mpango wa serikali wa kila jimbo kuwa na visima 5 ambapo majimbo yote ya mkoa wa Songwe tayari yamechimbiwa visima.
Alisema kazi iliyopo ni kuhakikisha wananchi wanaitunza miundombinu ya maji ili fedha iliyotolewa na serikali isipotee na kwamba ofisi ya wilaya na mkoa zilifanya kazi kubwa ya kufuatilia miradi,hivyo wananchi wahakikishe wanailinda kwa hali na mali.




Comments
Post a Comment