RC CHONGOLO APONGEZA UKUSANYAJI MAPATO TRA ILEJE AKIPOKEA CHANGAMOTO.
Na Ibrahimu Yassin,Songwe Serikali imeombwa kukipandisha hadhi kituo cha forodha cha Isongole wilayani Ileje Mkoani Songwe kutoka daraja C kwenda B pamoja na ujenzi wa majengo yenye hadhi mpakani....anaripoti Ibrahim Yassin,Songwe Leo Aprili 28/2024 Afisa mfawidhi kituo cha forodha Isongole katika mpaka wa Tanzania na Malawi Charles Chacha.baada ya mkuu wa Mkoa huo Daniel Chongolo kukaguana kupokea taarifa ya shughuli zinazotekelezwa mpakani hapo. Chacha amesema kutokana na kituo hicho kutokuwa na hadhi ,kwa sasa kinafanya kazi kama pacha na kituo cha forodha chaTunduma mpakani mwa Tanzania na Zambia Chacha amesema serikali inatakiwa kukipandisha hadhi kituo hicho kimekidhi vigezo vya kuongeza wigo wa ukusabyaji mapato kutoka Sh 7.8 milioni mwaka 2019 mpaka kufikia zaidi ya Sh 400 mwaka 2024 licha ya mpaka huo kuwa na vipenyo vinavyopelekea mapato mengi kupotea. Amesema mpaka huo unapitisha bidhaa mbalimbali zinazoingia na kutoka ikiwepo, zao la Mahindi, Soya, Karanga, vinywaji, saruj...