Posts

Showing posts from October, 2025

SONGWE DC -YAJIVUNIA KUKAMILISHA USAMBAZAJI UMEME NGAZI YA VIJIJI IKIKARIBIA KUKAMILISHA VITONGOJINI.

Image
Na Ibrahim Yassin,Songwe WANANCHI katika halmashauri ya wilaya ya Songwe mkoani Songwe,wameupongeza uongozi wa shirika la umeme Tanzania (Tanesco) wilayani humo kwa kukamilisha kikamilifu usambazaji wa umeme kwenye vijiji vyote. Wilaya ya Songwe yenye vijiji 43 ikiwa na vitongoji 205 na jimbo moja la uchaguzi huku makao makuu ya wilaya yakiwa katika kata ya Mkwajuni imefikia hatua nzuri ya kukamilisha vitongoji vyote usambazaji umeme katika miezi mitatu ijao. Licha ya upya wake wilaya hiyo iliyomegwa kutoka wilaya ya Chunya mkoani Mbeya miaka kumi iliyopita ilikuwa ikikabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo uhba wa nishati ya umeme lakini katika utawala wa awamu ya sita chini ya Rais Dkt,Samia Suluhu,wamefanikiwa kusambaza umeme vijiji vyote 43. Hayo yamesemwa leo Oktoba 27/2025 na meneja wa shirika hilo wilayani Songwe Mhandisi Michael Kidoto wakati akizungumza na dira kamilifu ofisini kwake na kusema wilaya ina vijiji 43 vyote vinahuduma za umeme na sasa wamehamia kukamilisha usambazaj...

SONGWE DC -YAJIVUNIA KUKAMILISHA USAMBAZAJI UMEME NGAZI YA VIJIJI IKIKARIBIA KUKAMILISHA VITONGOJINI

Image
Na Ibrahim Yassin,Songwe WANANCHI katika halmashauri ya wilaya ya Songwe mkoani Songwe,wameupongeza uongozi wa shirika la umeme Tanzania (Tanesco) wilayani humo kwa kukamilisha kikamilifu usambazaji wa umeme kwenye vijiji vyote. Wilaya ya Songwe yenye vijiji 43 ikiwa na vitongoji 205 na jimbo moja la uchaguzi huku makao makuu ya wilaya yakiwa katika kata ya Mkwajuni imefikia hatua nzuri ya kukamilisha vitongoji vyote usambazaji umeme katika miezi mitatu ijao. Licha ya upya wake wilaya hiyo iliyomegwa kutoka wilaya ya Chunya mkoani Mbeya miaka kumi iliyopita ilikuwa ikikabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo uhba wa nishati ya umeme lakini katika utawala wa awamu ya sita chini ya Rais Dkt,Samia Suluhu,wamefanikiwa kusambaza umeme vijiji vyote 43. Hayo yamesemwa leo Oktoba 27/2025 na meneja wa shirika hilo wilayani Songwe Mhandisi Michael Kidoto wakati akizungumza na dira kamilifu ofisini kwake na kusema wilaya ina vijiji 43 vyote vinahuduma za umeme na sasa wamehamia kukamilisha usambazaj...

BILIONI 300 ZATUMIKA MIRADI YA KIMKAKATI YA UJENZI INAUFUNGUA MKOA WA SONGWE-RAIS DKT,SAMIA ATAJWA..

Image
                      MAKALA Na Ibrahim Yassin,Songwe Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu inaendelea kutekeleza miradi mikubwa ya kimkakati ikiwemo upanuzi wa baraba ra kuu ya TANZAM kipande cha Igawa – Tunduma (Km 218) na Uje nzi wa kituo cha ukaguzi wa pamoja wa magari katika barabara hiyo eneo la Iboya Mkoani Songwe. Shilingi Bilioni Bilioni 4.84 zilitolewa fidia kwa wakazi wa eneo la Iboya kupisha mradi wa ujenzi kituo cha ukaguzi wa pamoja wa magari ambapo ujenzi unatarajiwa kuanza siku za hivi karibuni. Katika kipindi cha miaka miwili iliyopita Mkoa wa Songwe ulikumbwa na changamoto kwenye baadhi ya Barabara kutokana na mvua za El-Nino katika Barabara ya Kamsamba inayounganisha mkoa huo na mkoa jirani wa Rukwa. Kutokana na hali hiyo,Bilioni 32 zilitolewa ili kuondoa changamoto ya maeneo yaliyoathiriwa na mvua za El-Nino ikihusisha Daraja la Mpapa lenye urefu wa mita 60 katika barabara ya Mlowo - Kamsamba kwa shilingi bilioni 7. Mradi mungine ni Daraja la San...

JESHI LA POLISI LAWATOA HOFU WANANCHI LATANGAZA AMANI KWENYE UCHAGUZI.

Image
Na Ibrahim Yassin, Songwe JESHI la polisi mkoani Songwe lime wataka wananchi kutokuwa na hofu siku ya kupiga kura kwani limejipan ga kuhakikisha amani na utulivu utaimarishwa. Tanzania Bara siku ya Octoba 25/20 25 kutakuwa na uchaguzi mkuu wa Madiwani, wabunge na Rais huku jeshi la polisi likijipanga kuhakikisha amani na utulivu unakuwepo. Akizungumza leo Octoba 27/ 2025 ofisini kwake kamanda wa polisi mkoani Songwe Augostino Senga, amesema jeshi la polisi linaendelea kutekeleza majukumu yake. Amesema uchaguzi ni tukio muhimu kwa watanzania wote kutimiza haki yao ya kikatiba ya kupiga kura kwa amani na utulivu. Amesema wananchi wanahimizwa Kujitokeza kwa wingi kushiriki katika Uchaguzi huo muhimu huku jeshi la Polisi likihakikisha kunakuwepo na utulivu na amani katika kipindi chote.  ameongeza kuwa katika kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa amani, jes hi la polisi Mkoa wa Songwe limewe ka mikakati madhubuti ya kiulinzi ikiwa ni pamaja na kupata taarifa za kiintelijensia.  Amesema hatua...

Kuzinduliwa kwa zahanati ya Kalila kwaleta faraja kwa jamii

Image
Anaclara Ngatunga,Nkasi Zahanati ya kalila iliyopo katika Kijiji cha kalila Kata ya Kabwe Wilaya ya Nkasi Mkoani Rukwa, ambayo ilianza kujengwa toka mwaka 2024 imezinduliwa na kuanza kutoa huduma rasmi tarehe 21 oktoba 2025. Zahanati hiyo iliyogharimu kiasi cha shilingi millioni tisini na moja, laki mbili na kumi na nane elfu na miamoja (91,218,100. ),ambazo ni fedha kutoka kutoka serikali kuu, mapato ya ndani ya Halmashauri, pamoja na nguvu za wananchi inayotarajiwa kuhudumia wananchi zaidi ya 2500 wa Kijiji cha kalila na maeneo jirani. Akizindua Zahanati hiyo, Kelvin Nyamonge Tuyi Mkuu wa seksheni afya (W) amewashukuru wananchi pamoja na serikali kuu na mapato ya ndani chini ya Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Nkasi waliochangia ujenzi wa zahanati hiyo hadi kukamilika na kuwataka wananchi wa eneo hilo kutunza miundombinu hiyo ili iendelee kuwahudumia wananchi. “Niwapongeze sana wananchi wa kalila kwa kuja na wazo la ujenzi wa Zahanati na kisha mkachangia Shilingi milioni kum...

MIRADI YA KIMKAKATI YA TANROAD INAUFUNGUA MKOA WA SONGWE-ENG, BISHANGA

Image
Serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inaendelea kutekeleza miradi mikubwa ya kimkakati ikiwemo upanuzi wa barabara kuu ya TANZAM kipande cha Igawa – Tunduma (Km 218) na Ujenzi wa kituo cha ukaguzi wa pamoja wa magari katika barabara hiyo eneo la Iboya Mkoani Songwe. Katika kipindi cha miaka miwili iliyopita Mkoa wa Songwe ulikumbwa na changamoto kwenye baadhi ya Barabara kutokana na mvua za El-Nino katika Barabara ya Kamsamba inayounganisha mkoa huo na mkoa jirani wa Rukwa ambapo Bilioni 32 zilitolewa ili kuondoa changamoto ya maeneo yaliyoathiriwa na mvua za El-Nino ikihusisha Daraja la Mpapa lenye urefu wa mita 60 katika barabara ya Mlowo - Kamsamba kwa shilingi bilioni 7, Daraja la Sange lenye mita 25 na barabara za maingilio kwa gharama ya Shilingi Bilioni 7.3, daraja la Kabalisi lenye urefu wa mita 40 na barabara za maingilio kwa gharama ya Shilingi Bilioni 7.7, na Ujenzi wa barabara ya Zege na kuchoronga milima kwa gharama ya Shilingi Bilioni 8.8 ...

Wapiga kura uchaguzi mkuu Nkasi watangaziwa rasmi siku ya kupiga kura

Image
‎ Na Israel Mwaisaka,Nkasi ‎ ‎Tume huru ya taifa ya Uchaguzi Jimbo la Nkasi Kaskazini na Nkasi kusini kwa mujibu wa kifungu Cha 69 (1)1 imetangaza rasmi Kuwa Oktoba 29,2025 Ni siku ya kupiga Kura kwa wale wote waliojiandikisha katika Daftari la kudumu la wapiga Kura. ‎ ‎Akitoa tangazo hilo leo Oktoba 20,2025 Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Nkasi Kaskazini na Nkasi kusini George Mwahinda amesema kuwa vituo vilivyotumika kuandikisha wapiga Kura ndivyo vitakavyotumika kupigia Kura. ‎ ‎Amesema kuwa pamoja na tangazo hilo katika kila kituo cha kupigia Kura zimebandikwa taarifa mbalimbali ikiwemo karatasi ya mfano yenye majina na picha za kila mgombea pamoja na Nembo ya vyama vyao vya siasa kwa Uchaguzi wa Rais,Wabunge na Madiwani. ‎ ‎Pia nitakuwepo na orodha ya majina ya Wapiga Kura walioandikishwa na tume huru ya taifa ya Uchaguzi ikiwa ni pamoja na orodha ya Wapiga kura walioruhusiwa kupiga Kura moja tu ya Rais ‎ Mwahinda amefafanua kuwa vituo vyote vya kupigia Kura siku ya Uchaguzi vi...

NAIBU KATIBU MKUU ARIDHISHWA SPEEDI YA WAKANDARASI WANAWAKE

Image
-AAHIDI KUWAONGEZEA MIRADI YA BILIONI 50 KUTOKA BILIONI 10 ZA AWALI. AMTAJA RAIS DKT,SAMIA. Na Ibrahimu Yassin,Songwe SIKU chache baada ya Serikali kupitia wizara ya ujenzi kuweka mpango wa kuwawezesha wakandarasi wanawake wazawa kujenga miradi isiyozidi Bilioni 10,hatimaye Naibu katibu mkuu wa wizara hiyo Dkt,Charles Msonde aridhishwa na mwanzo mzuri wa wakandarasi hao. Wizara ya ujenzi chini ya wakala wa barabara mijini na vijijini (Tanroads) mkoani Songwe imetii agizo la Serikali la kuwpatia wakandarasi wanawake wazawa kujenga barabara za Lami ambapo ilitoa tenda ya ujenzi wa kilometa 20 zinazogharimu Tsh,Bilioni 45.447. Kiasi hicho cha fedha kitatumika kujenga barabara ya Ruanda-Idiwili yenye thamani ya Bilioni 45.447 yenye kilometa 20    ambapo kilometa 5 zimetolewa kwa    wakandarasi wanne watakaojenga kilometa tano tano ambapo jana walisaini mikataba ya utekelezaji wa mradi huo Baada ya wakandarasi wa kampuni hizo nne kuanza ujenzi mkoani Songwe,Naibu katibu mkuu Dkt,Msonde,mwis...

Naibu katibu mkuu avutiwa na kasi ya Wakandarasi Wanawake-Songwe

Image
Na Ibrahim Yassin, Songwe Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Dk. Charles Msonde, amepongeza kasi na ubora wa ujenzi wa barabara unaotekelezwa na wakandarasi wanawake wazawa mkoani Songwe, akisema wameanza vizuri na wanaonyesha uwezo mkubwa katika utekelezaji wa miradi ya serikali. Dk. Msonde alitoa pongezi hizo leo, Oktoba 15, 2025, wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya ujenzi wa barabara na madaraja katika wilaya za Ileje na Mbozi. Akiwa wilayani Ileje, alikagua Daraja la Sange, linalojengwa kwa gharama ya Shilingi Bilioni 7.942, ambapo ujenzi unaendelea kwa kasi nzuri. Baada ya kukagua, Dk. Msonde aliagiza wakandarasi kuongeza kasi ya ujenzi, ikiwemo kufanya kazi usiku na mchana ili miradi ikamilike kwa wakati. Akizungumza katika ziara hiyo, Dk. Msonde alisema ameridhishwa na matumizi ya fedha za serikali, akibainisha kuwa fedha zimetumika ipasavyo na miradi inaonyesha tija kwa wananchi. Katika wilaya ya Mbozi, alikagua ujenzi wa Barabara ya Ruanda–Nyimbili–Hasamba–Izyila–Itumba...