Posts

Showing posts from February, 2025
Wananchi wa kata

Jamii yaombwa kutowahusisha Wazee na imani za kishirikina

Image
Na Ibrahim Yassin,Songwe Wananchi wa Kitongoji cha Hawiga Kijiji cha Shaji Kata ya Mlangali wilaya ya Mbozi Mkoani Songwe wametakiwa kuacha tabia ya kuwahusisha wazee wa Kitongoji hicho na imani za kishirikina kwa kuwa vitendo hivyo hupelekea kutendewa. vitendo vya ukatili mkoani Songwe vimekuwa vikishikAa kasi huku wazee wakishutum8wa kitu ambacho kinapingwa vikali na jamii huku jeshi la polisi likiendelee kuiasa jamii kuwapenda wazee. Kauli hiyo ilitolewa Februari 25, 2025 na Polisi Kata ya Mlangali Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Robart Kasunga wakati akitoa elimu kwa wana nchi hao juu ya umuhimu wa kuwatunza na kuwalea wazee kwani kundi hilo kwa sasa ni hazina kubwa katika malezi bora ya jamii ya sasa. "Acheni kuwahusisha wazee au watu wa makamu moja kwa moja na imani za kishirikina kufanya hivyo ni kosa kisheria na atakayebainika kufanya hivyo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hizo" alisema Mkaguzi Kasunga. Sambamba...

ENDELEENI KUSIMAMIA USALAMA NA KUJIPANGA NA UCHAGUZI MKUU, 2025.

Image
Na Ibrahim Yassin Songwe Maafisa na Wakaguzi wa jeshi la polisi Mkoa wa Songwe wametakiwa kujipanga kuhakikisha wana simamia usalama na kuendelea kujipanga na uch haguzi mkuu ujao ambao unatarajiwa kufanyika Octoba 25/mwaka 2025. Hayo yamesemwa Februari 24, mwaka huu  na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Augustino Senga wakati alipofanya kikao kazi na Maafisa na Wakaguzi katika ukumbi wa Polisi uliyopo Vwawa Wilaya ya Mbozi. Senga amesema ni bora maafisa hao wakaen delea kusimamia Askari katika himaya zao ili kutimiza jukumu mama la Jeshi la Polisi kwa kufuata sheria katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku ili jamii iendelee kuwa salama. "Endeleeni kutekeleza jukumu la kusimamia usalama wa raia na mali zao ikiwa ni pamoja na kujipanga na uchaguzi Mkuu, 2025 ili ufanyike kwa amani na usalama bila kujali itikadi ya chama chochote cha Siasa" alisema Kamanda Senga. Kwa upande wao, Maafisa wamemshukuru Ka manda Senga na wameelez...

MSAADA WA KISHERIA WA MAMA SAMIA KUZINDULIWA RUKWA

Image
Katibu tawala wa mkoa Rukwa Msalika Makungu Na Israel Mwaisaka,Rukwa SERIKALI mkoani Rukwa imetangaza kuzinduliwa kwa kampeni ya huduma ya msaada wa kisheria  ya MAMA Samia Leagel Aid itakayozinduliwa siku ya kesho Feb. 25 majira ya saa 2 asubuhi katika viwanja vya stendi ya mabasi ya Sokomatola ambapo wananchi watapata msaada wa kisheria kutokana na changamoto mbalimbali zinazo wakabiri. Akizungumzia uzinduzi wa Kampeni hiyo, Katibu tawala mkoa wa Rukwa Msalika Makungu amesema kuwa lengo la kampeni ni kutoa msaada kwa waathirika wa vitendo mbalimbali ambao wengi wao hawana uwezo wa kufikia huduma za kisheria hivyo wanapaswa kujitokeza kwa wingi ili wakapate huduma hiyo. Aidha amesema kuwa huduma za kisheria zitakazo tolewa kipindi chote cha Kampeni zitakuwa ni bure ambapo kampeni hiyo itafanyika kwa muda wa siku tisa katika halmashauri zote za mkoa na baadhi ya kata katika mkoa wa Rukwa. Kwaupande wake Beatrice Mpembo ambaye ni Mkurugenzi msaidizi wa haki za binadamu kutoka wizara ya ...

Polisi Rukwa kuwasaka waliofukua kaburi na kuondoka na mwili wa marehemu

Image
Na Israel Mwaisaka,Rukwa Jeshi la Polisi mkoani Rukwa linawatafuta Watu waliohusika kufukua kaburi la Julius Ladislaus (24) aliyefariki Novemba mwaka Jana na kuondoka na mwili wa marehemu. Akizungumza na Waandishi wa Habari kamanda wa Polisi mkoa wa Rukwa Shadrack Masija alisema kuwa marehemu alifariki Novemba mwaka Jana wilayani Chunya mkoani Mbeya na mwili wake kusafirishwa mkoani Rukwa na kuzikwa Katika Kijiji cha Lunyala wilayani Nkasi. Amedai kuwa mnamo February 14 ya mwaka huu wa 2025 mwili wa marehemu ulikutwa umefukuliwa Katika kaburi Hilo na mwili kuchukuliwa na kuliacha sanduku na kaburi lake vikiwa wazi huku mwili wa marehemu wakiondoka nao. Hivyo amewaomba Wananchi wote walio na taarifa juu ya Watu waliofanya vitendo hivyo viovu na vya kutisha kutoa taarifa Polisi Ili Watuhumiwa waweze kukamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria. Kamanda Masija Alidai kuwa Polisi wanaendelea na uchunguzi wa kina juu ya suala Hilo na kuwa kimsingi suala Hilo linahusishwa na Imani za kis...

UTATU MTAKATIFU WA VIONGOZI CHANZO SONGWE KUPAA KIMAENDELEO.

Image
"Tumekuwa tukifuata ushauri kwa Dc,uongozi wa mkoa na uongozi wa Chama,tunakusanya vizuri mapato na miradi inasimamiwa vizuri" Na Ibrahim Yassin,Songwe  WANANCHI wa vijiji mbalimbal wilayani Songwe mkoani hapa wameupongeza uongozi wa halma shauri hiyo kwa ukusanyaji mapato na nidhamu nzuri ya matumizi. Nidhamu nzuri ya matumizi ya fedha imepelekea miradi ikamilike kwa wakati na kuifanya Songwe ipae kimaendeleo  Johnson Samson mkazi wa Mkwajuni amesema amekuwa akifuatilia kwa mbali jinsi halmashauri inavyoendeshwa amekundua hali ya maendeleo ilivyo. Amesema kila mradi unaojengwa umekamilika kwa wakati na hakuna malalamiko baina ya waka ndalasi na viongozi wa halmashauri ukilinganisha na halmashauri zingine. Amesema halmashauri zingine ndani ya mkoa wa Songwe ameshuhudia wakurugenzi wakidaiwa fedha na wakandalasi wazawa walizozitumia kukamilisha miradi kwa kuweka miundombinu husika. Jamila Mwashilindi mkazi wa Iseche amessema  wilaya yanSongwe ni moja ya wilaya mpya mkoan i Son...

RC MBEYA AMFANYIA TUKIO MMILIKI SHULE YA HOLLY LAND PRE AND PRIMARY SCHOOL CHUNYA.

Image
Na Ibrahim Yassi, Mbeya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Zuberi Homera amefanya ziara ya kushtukiza akiitembelea shule ya mchepuo wa Kiingereza ya Holly Land iliyopo Mamlaka ya Mji Mdogo wa Makongolosi Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya. Mkuu huyo wa mkoa ameitembelea shule hiyo jana baada ya kufanya vyema kwa kufaulisha wanafunzi wote wa darasa la saba na kushika nafasi za juu hadi ngazi ya Taifa. Lengo la kutembelea shule hiyo ni kuipongeza kwa matokeo mazuri tangu kuanzishwa kwake na uwekezaji mkubwa wa Lawena Nsonda(Baba Mzazi), huku akishauri jitihada zaidi zifanyike. Shule hiyo imedaiwa kuuheshimisha mkoa wa Mbeya na Taifa kwa ujumla kutokana na kufau lisha wanafunzi wote kwa alama One na Two katika mitihani yote. Aidha amewataka wazazi Mkoani Mbeya kuwa peleka watoto shuleni hapo badala ya kuwapeleka mikoa ya mbali kwani shule ina huduma nzuri na malezi mazuri wakiwemo walimu wabobezi. ^Mkurugenzi Lawena Nsonda unayejulikana kwa jina la umaarufu Baba Mzazi, shule yako imetuhe shimisha hivy...

DC Itunda ampongeza DED Kavishe kwa ukusanyaji mapato na nidhamu ya matumizi

Image
" Ushauti wangu katika kikao cha kamati ya ushauri ya wilaya umezaa matunda Songwe sasa haikamatiki kimaendeleo" Na Ibrahim Yassin, Songwe Mkuu wa Wilaya ya Songwe, Solomon Itunda jana alimpongeza mkurugenzi mtengmdaji wa halmashauri ya wilaya ya Songwe Secillia Kavishe kwa makusanyo mazuri ya mapato ya ndani na nidha mu ya matumizi. Alisema anajisikia fahari kuwa na mkurugenzi msikivu ambaye anashaurika na kwamba amekuwa akisimamia vyema miradi na kuhakikisha fedha haipotei. ""Ded Kavishe ni mtu na nusu hivyo naona fahali kufanya kazi nae, miradi yote inatekelezwa vizuri fedha za umma hazipotei, anafanya kazi hadi muda wa ziada", alisema Dc Itunda. Katika siku za hivi karibuni Itunda aliongoza Kikao cha Kamati ya Ushauri ya Wilaya ya Songwe (DCC ) Kujadili mapendekezo ya Mpango na Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2025/2025. Mkuu huyo wa wilaya aliongoza Kikao kilichofanyi ka siku za hivi karibuni katika ukumbi wa Sambila uliopo katika ofisi za Halmashauri ya Wilaya y...

Halmashauri ya wilaya Nkasi yaweka mkakati wa kukabiliana na uhaba madawati

Image
Na Israel Mwaisaka,Nkasi KAIMU mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya Nkasi mkoani Rukwa Steward Vidoga amesema kuwa halmashauri katika kukabiliana na changamoto ya madawati shuleni wametenga Tshs,Mil.80 kutokana na mapato ya ndani na mchakato wa utengenezaji wa madawati huo wa madawati unaendelea. Ameyasema hayo jana alipokuwa akijibu swali la papo kwa hapo kutoka kwa diwani wa kata ya Chala Michael Mwanalinze aliyetaka kujua halmashauri Ina mpango Gani wa kupunguza tatizo la madawati Katika shule za msingi na sekondari ambapo amedai kuwa Hadi sasa katika utengezaji wa viti na meza na katika awamu hii ya kwanza ambayo itakamilika mapema wiki ijayo kwa kukamilisha utengenezaji wa viti na meza 506. Amesema kuwa wiki ijayo wakikamilisha awamu hiyo ya kwanza wataanza kuyatengeneza madawati mengine Ili kuweza kukamilisha Tshs,mil.80 iliyotengwa Katika mwaka huu wa fedha wa 2024-25. Vidoga amefafanua kuwa halmashauri inatambua changamoto kubwa ya madawati katika shule zote za msingi n...