Posts

Showing posts from July, 2024

Mradi wa umeme wa TAZA kuiunganisha Afrika na Umeme

Image
Na Israel Mwaisaka,Rukwa NAIBU waziri mkuu wa jamhuri ya mungano wa Tanzania na waziri wa nishati Dkt,Dotto Biteko ameweka jiwe jiwe la msingi njia ya kusafirisha umeme ya msongo wa Kilovolti 400 kutoka Iringa hadi Sumbawanga na kuunganisha Tanzania (TAZA) pamoja na vituo vya kupoza umeme vya Tangameda,Kisada,IganjoNkangamo na Malangali. Mradi huu umelenga kuunganisha mkoa wa Rukwa na grid ya Taifa ikiwa ni pamoja na kuunganisha na mataifa mengine ya Afrika ili kuwa na umeme wa uhakika kwa asilimia 100. Akizindua mradi huo Dkt.Biteko amesema mkoa wa Rukwa haujaunganishwa na Grid ya taifa toka Nchi ipate uhuru na kuwa kutokana na jitihada mbalimbali zinazofanywa na serikali ni kutaka kuona mkoa Rukwa na mikoa mingine yote nchini Tanzania inaunganishwa kwenye gridi ya taifa ili kuwa na umeme wa uhakika na watu waweze kuutumia umeme katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo na uzalishaji mali. Alisema kuwa mradi huo ni sehemu ya maandalizi ya mwisho kwa mkoa Rukwa kuingizwa kwenye gridi...

TRA Songwe yawapiga tafu Polisi kwa kuwapatia gari ili kusaidia shughuli za kijeshi

Image
Na.Ibrahim Yassin Songwe Afisa Mnadhimu namba 02 wa Polisi Mkoa wa Songwe Mrakibu Mwandamizi wa Polisi SSP Geofrey Munguajuna amepokea gari hilo kutoka mamlaka ya mapato kusaidia shughuri za kijeshi. Afisa huyo akiambatana na Msimamizi wa Magari ya Polisi Mkoa wa Songwe Mkaguzi wa Polisi Kas ibert Kapondo wamepokea Gari aina ya Toyota Mark X lililotumika kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa lengo la kusaidia shughuli za Jeshi la Polisi. Gari hilo limetolewa leo Julai 25, 2024 na Zahor Mohammed Salum ambaye ni Meneja Msaidizi wa Forodha Mkoa wa Songwe kwa ajili ya kusaidia kazi za kila siku za Jeshi la Polisi. SSP Munguajuna ameishukuru Mamlaka ya Mapato Mkoa wa Songwe kwa msaada walioutoa na amewaomba kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi katika harakati za kuzuia na kupambana na uhalifu na wahalifu ili jamii iendelee kuwa salama kwa manufaa na maendeleo ya nchi yetu.7. Jeshi la polisi mkoani hapa limekuwa likifanya kazi kwa ushirikiano na maafisa wa mamlaka hiyo hivyo zawad...

Mbunge Fiyao adhamiria kukuza vipaji vya katika michezo kwa kuanzisha ligi

Image
Na Ibrahim Yassin.Songwe LIGI ya mchezo wa mpira wa miguu mkoani Songwe kwa ajili ya kutafuta na kuibua vipaji inatarajia kuanza siku za hivi karibuni wilayani Ileje na kumalizika Halmashauri ya mji Tunduma. Mchezo huo pendwa wa mpira wa miguu Duniani umedhaminiwa na Mbunge viti Maalum mkoa wa Songwe Stella fiyao huku akitenga kitita cha fedha kwa ajili ya zawadi. Akizungumza leo Julai 26/2024 mbunge Stella Fiyao (CHADEMA) amesema lengo la kuanzisha ligi hiyo ni kuunga mkono jitihada za Rais Dkt, Samia katika sekta ya michezo. Amesema kwa kutambua umuhimu wa mchezo huo jinsi unavyotoa ajira Rais Dkt.Samia ameongeza bajeti ili kufanikisha na kuukuza maradufu mchezo huo pamoja na michezo mingine. "Rais Dkt Samia katika utawala wake mpira wa miguu kwa wanaume na wanawake umekuwa na Nchi imetangazika hivyo namuunga mkono kwa kuanzisha ligi kukuza vipaji vya vijana"amesema Fiyao. Hata hivyo Fiyao amewasihi wazazi kutowakataza watoto zao hasa wa kike kucheza mpira wa miguu akisema ...

NMB yaadhimisha siku ya Mwalimu spesho kwa kuwajengea uwezo waalimu namna njema ya kuitumia mikopo

Image
Na Israel Mwaisaka, Nkasi BENKI ya NMB Imewakutanisha Waalimu zaidi ya 200 wa halmashauri ya wilaya Nkasi katika kuadhimisha siku ya Waalimu ikiwa ni pamoja na kuwajengea uwezo namna ya kuitumia mikopo wanayoipata katika kujiimarisha kiuchumi na kujipanga vyema namna ya kuishi baada ya kustaafu. Akizungumza na Waalimu hao Kaimu meneja wa NMB kanda ya nyanda za juu kusini Daniel Zake amesema kuwa wao kama Benki wameiandaa siku hii ya Mwalimu spesho kama hatua ya kutambua mchango wa Walimu kama Moja ya kundi linalopata huduma za za Benki hiyo na kuwa na mchango mkubwa katika Benki hiyo. Amesema kuwa Moja ya huduma kubwa ni ya mikopo na kuwa wao kama Benki wameamua kukutana nao Ili kuwajengea uwezo namna ya kuitumia mikopo wanayoipata Ili iweze kuwanufaisha na kujiandaa katika maisha ya baadae hasa baada ya kustaafu badala ya kuendelea kuwapatia mikopo Bila ya kuwa na elimu namna njema ya Matumizi ya fedha hizo . Amefafanua kuwa Benki hiyo inatamani kuona maisha ya Walimu yanakua endele...

RC-TUMIENI FURSA YA MRADI WA UMWAGILIAJI KUJIINUA KIUCHUMI

Image
Na Israel Mwaisaka, Nkasi Mkuu wa mkoa Rukwa Charles Makongoro Nyerere amewataka Wananchi wa kata za Kipili, Kirando na Itete wilayani Nkasi kutumia fursa ya mradi wa umwagiliaji unaojengwa katika kata hizo kuinua kipato Chao Huku akiwataka Wananchi kulinda miundombinu ya mradi huo Ili use na manufaa Kwa jamii kama ilivyokusudiwa na serikali. Mkuu huyo wa mkoa ameyasema hayo Jana wakati akishuhudia utiaji Saini na makabidhiano ya mradi wa skimu ya umwagiliaji Lwafi-Katongolo kati ya tume ya taifa ya taifa ya umwagiliaji na mkandarasi M/S Halem Construction Company Limited Alisema licha ya serikali kutumia fedha nyingi kukamilisha mradi huo hautakuwa na maana kama watashindwa kuutunza na kuulinda na kuwa lengo la serikali ni kutaka kuona uzalishaji unapanda na Wakulima kuweza kulima kilimo Cha kibiashara na kujikwanua kiuchumi na kubwa ni kutaka kuona jamii inabadilika Kwa kuwa na maisha bora. Akitoa taarifa ya mradi huo Mhandisi Lucas Mganda ambaye pia ndiye msimamizi mkuu wa mradi huo...

Wavuvi Mwalo wa Kafyofyo ziwa Nyasa Kyela waomba banda la majokofu ili waondokane na uuzaji samaki kwa bei ndogo

Image
Na Ibrahim Yassn Kyela. WAVUVI na wafanya biashara ziwa Nyasa mwalo wa Kafyofyo uliopo kijiji cha Njisi kata ya Kajunjumele wilayani Kyela mkoani Mbeya wameiomba serikali kuwatatulia kero sugu ikiwemo kuwajengea banda la majokofu kukuza vipato vyao. Mwalo wa Kafyofyo ni kitega uchumi kikubwa cha mapato ya halmashauri huku vijana wengi wakipata ajira ya uvuvi na wengine wakiacha kukaa vijiweni wakianzisha biashara ya samaki na kujiingizia vipato. Kikwazo kikubwa cha kukwamisha jitihada hizo ni ukosefu wa miundombinu rafiki ikiwemo ukosefu wa barabara ,banda la kupumzikia na la kuhifadhia samaki,umeme na vyoo. Mwalo huo wa Kafyofyo ni chanzo kikubwa cha mapato ya halmashauri inayodaiwa kuwa na wavuvi na wamiliki wa vyombo vya uvuvi na nyavu 500 wanunuzi wakiwa 2500. Katika Mwalo huo wenye wavuvi na wanunuzi zaidi ya 3.000 wamekumbwa na changamoto hizo na wapo hatarini kukumbwa na magonjwa ya milipuko ikiwemo kuhara na kipindupindu. Peter Mwantimwa ni mfanyabiashara katika mwalo huo a...

Shonza awaasa Watumishi wa idara ya afya kuwa na lugha za staa kwa Wagonjwa

Image
Na Ibrahim Yassin.Songwe. Mbunge wa viti maalum mkoa wa Songwe Juliana Shonza (CCM) ametoa wito kwa watumishi idara ya afya mkoani Songwe kuwa na lugha za staa kwa wagonjwa. Shonza aliyasema hayo jana wakati akigawa zawadi kwa akina mama wajawazito na watoto katika hospitali ya wilaya ya Mbozi mkoani Songwe pamoja na kukagua ujenzi wa jengo la mama na mtoto lililotolewa Milioni 900. Alisema siku za nyuma akiwa na uongozi wa chama alifika hospitalini hapo na kukuta malalamiko mengi ikiwemo lugha za matusi kwa wajaw azito wanaofika hapo kujifungua. Alisema mgonjwa anahitaji faraja ili aweze kujifungua salama na hilo alilifikisha kwa waziri wa afy a Ummy Mwalimu hali iliyohamisha watumishi katika hospitali hiyo. " Nawaomba tuwe na lugha za staa kwa akina mama hawa, na ni marufuku pia kuwatoza fedha akina mama wajawazito na watoto chini ya miaka 5 kama inavyoeleza sera ya afya ya mwaka 2007 "alisema.Shonza. Alisema anaamini kwa sasa.baada ya kuondole wa baadhi ya watumishi kati...

SERIKALI YATOA MIL.900 KUJENGA JENGO LA MAMA NA MTOTO KUPUNGUZA CHANGAMOTO ZINAZOWAKUMBA AKINA MAMA.

Image
Na Ibrahim Yassin.Songwe.  Kutokana na uwepo wa uhaba wa baadhi ya majengo ikiwemo la mama na mtoto hospitali ya wilaya ya Mbozi mkoani Songwe hatimaye serikali imet oa Tsh.Milioni 900 kujenga jengo jipya kumaliza tatizo hilo. Halmashauri ya wilaya ya Mbozi ni moja ya halmashauri kongwe nchini lakini imekuwa ikikabiliwa na upungufu wa baadhi ya majengo katika hospitali hiyo hali iliyolazimu akina mama kubanana wakisubiri huduma. Wananchi wakiwemo mama wajawazito wameipongeza serikali kwa ujio wa fedha hizo wakisema itawaondolea kadhia ya kubanana kutokana na ufinyu wa jengo huku wengine wakiongelea kutozwa fedha. Stija Sande mjamzito aliyekuwepo hospitalini hapo alisema licha ya uwepo wa sera ya nchi kuwa mama mjamzito na mtoto chini ya miaka 5 kutibiwa bure lakini wamekuwa wakiambiwa wakanunue dawa. Alisema wananchi wengi wamekuwa na bima ya  afya ya jamii ya Tsh,30.000 lakini wakifika hospitalini wanapewa dawa za bei ya chini dawa za bei ya juu wanaambiwa wakanunue madukani hali inay...

SIKU 7 ZA RAIS DKT,SAMIA ZILIVYOACHA HISTORIA NA ALAMA MIKOA YA KATAVI ,RUKWA NA SONGWE

Image
                     MAKALA AZINDUA MIRADI MIKUBWA NA YA KIMKAKATI KATAVI NA RUKWA WANANCHI HAWAKUTAKA AONDOKE. Na Ibrahim Yassin,Songwe Zimekua siku 7 za moto zenye kishindo cha maendeleo toka Julai 12 hadi wiki hii Jumatano Julai 87, 2024 ambapo Rais wa Jamhuri ya Muunga no wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan alikua na ziara kubwa na ya kimkakati kwenye mikoa miwili ya Nyanda za Juu Kusini. Takribani siku 6 alizokuwepo kwenye mikoa hii ya pembezoni mwa nchi yetu zimetuma ujumbe kwa kila Mtanzania jinsi kazi kubwa ya maendeleo inavyozidi kufanyika kila kona ya Taifa Rais Dkt,Samia alipokuwa na timu yake mikoa ya Katavi na Rukwa kasha akapita mkoa wa Songwe siku ya 7.  Miaka ya nyuma kulikua na msemo kuwa mikoa ya pembezoni mwa nchi yetu ilikua kama ni mikoa iliyoachwa nyuma kimaendeleo, lakini leo miaka mitatu ya Rais Samia madarakani imefuta misemo hiyo kwa kuangalia jinsi miradi mikubwa ya kutoa huduma kwa wananchi ilivyotekelezwa kwenye mikoa hiyo huku Rais Samia akiizundua. Katik...

JINSI M-NEC MWASELELA ALIVYO ACHA ALAMA ZANZIBAR AKITOA MISAADA LUKUKI.

Image
Na Ibrahim Yassin.Zanzibar Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa (NEC) kutoka Mkoa wa Mbeya Ndele Mwaselela ameacha historia ya kusisimua Zanziar alikoenda kwenye kazi za chama akiwa mgeni maalumu Kuanzia Julai16/,2024 Mjumbe Ndele Mwaselela alihitimisha ziara yake ya siku nne Visiwani Zanzibar na kuacha tabasamu kwa wakaazi wa visiwa huvyo ambao hawakutaka aondoke. Siku ya kwanza ya ziara yake aliagua shughuli mbalimbali za maendeleo yaliyofanywa na Ser ikali inayoongwa na Rais Dkt. Hussen Mwinyi ikiwemo kujionea huduma za Hospitali ambapo wagonjwa walieleza wazi kuwa wanatibiwa bure na kupatiwa chakula mara tatu kwa siku bure. Pia alijionea  jinsi kila kitanda kikiwa na sehemu ya mawasiliano kati ya mgonjwa na daktari hali inayorahisisha daktari kujua hali na mahitaji ya mgonjwa kirahisi. Kiongozi huyo pamoja na kupongeza jitihada hizo za serikali ya mapinduzi Zanzibar hakusita kutaja moyo jina la Rais Mwinyi na kuwasihi wananchi kuendelea kumuunga mkono na kuunga mkono chama chake ...

Mama Samia na Wafanyabiashara Songwe wampa 5 Mbunge Fiyao kwa namna anavyoshughulika na kero za Wananchi

Image
Na Ibrahim Yassin.Songwe Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu amepongeza mbunge wa viti maa lum mkoani humo Stella Fiyao kwa kutekeleza ma jukumu yake pamoja na kutambua kazi zilizofaan ywa na serikali. Dkt, Samia aliyasema hayo jana wakati akiwas alimia wananchi wa mkoa wa Songwe eneo la Tunduma akitokea mikoa ya Katavi na Rukwa alikokuwa kwenye ziara ya kikazi. Alisema Mbunge Fiyao wa Chadema ametambua kazi zilizofanywa na serikali ni jambo zuri na kwak utambua umuhimu wa demokrasia walifanya meri dhiano na vyama vyote na sasa wanafanya kazi kwa kushirikiana. Awali akizungumza baada ya kupanda kukwaani mbunge Fiyao alisema anaipongeza serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt,Sam ia.kwa kwa kuleta maendekeo kwani Tanzania kwa sasa inang'ara. Alisema kwa upande wa vyama vya upinzani wamekuwa wakinena rugha moja wanakula na kukaa.pamoja ukilinganiaha na miaka ya nyuma ambapo waliishi kwa chuki. Fiyao alitumia jukwaa hilo kumueleza Rais Samia kupitia ...

Mbunge Fiyao atoa msaada wa Mil 3 kwa Wagonjwa na Wafungwa huku Wananchi wakitoa pongezi

Image
Na.Ibrahim Yassin Songwe WANANCHI wa wilaya zilizopo mkoani Songwe wamempongeza mbunge viti maalum mkoani humo Stella Fiyao (CHADEMA) kwa kutoa misaada ya mashuka,madishi,mchele,Maharage na taulo za kike kwa wafungwa na wagonjwa vikiwa na thamani ya Tsh Milioni zaidi ya Milion 3. Wakizungumza.leo Julai 19 /2024.wananchi hao wamesema kwa kitendo alichokifanya Mbunge huuo kwa kutoa misaada hiyo Mungu atampa maisha marefu kwani kitendo cha wafungwa magerezani na wagonjwa hospitalini kupewa mahitaji wanapata faraja. Samweli Mtafya mkazi wa Ileje amesema alipo ona mbunge huyo amefika wilaya ya Ileje kutoa misaada hiyo kwa wagonjwa alifurahi na kusema huo ni mfano wa kuigwa kwa wadau wengine kuona umuhimu wa kusaidia wenye uhitaji. Sarafina Nashihuya mkazi wa Ileje amesema wana kila sababu ya kumpongeza Mbunge Fiyao kwa kuona wafungwa na wagonjwa wanahitaji mahitaji muhimu hivyo amefanya jambo jema kuwapa misaada wenye uhitaji. Kwa upande wake Mbunge Stella Fiyao amesem a.yeye kama kiongozi...

Watendaji wa jeshi la Polisi Songwe wapewa mafunzo ya kisayansi

Image
Na IbrahimYassin.Songwe Kamishina wa uchaguzi wa kisayansi CP Shabani Hiki ameendesha mafunzo ya uchaguzi wa Kisayansi kwa watendaji wa jeshi la polisi mkoani Songw e. Mafunzo hayo yamefanyika leo Julai 19 mwaka huu katika ukumbi wa jeshi hilo mkoani hapa huku maafisa mbalimbali wa jeshi hilo wakiudhuria mafunzo hayo. Waliohudhuria pia katika mafunzo hayo ni watendaji wa taasisi mbalimbali zinazofanya kazi na jeshi la polisi ambao ni madaktari,wanasheria , na ofisi ya Taifa ya mashitaka mkoa wa Songwe. Mafunzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa Polisi uliopo Vwawa Mbozi yakiwa na lengo la kuwajengea uwezo katika upelelezi wa matukio ya jinai, na ukusanyaji wa ushahidi na vielelezo kwa kutumia uchunguzi wa Kisayansi. Kwa mujibu wa afisa habari wa jeshi hilo mkoani hapa Issa Mwandagala ni kuwa uongozi unaoendesha mafunzo hayo ni watazungumza na vyombo vya habari pindi mafunzo yatakapofikia tamati.

Mwaselela atafsiri maono ya Rais Samia katika sekta ya michezo kwa kudhamini ligi kwa Mil.18

Image
Na Ibrahim Yassn Mbeya MOJA ya jukumu na kazi za Mjumbe wa halmash auri Kuu ya CCM ya Taifa (NEC) ni pamoja na ku toa uongozi wa Siasa ya CCM kwa jumla kwa Tan zania nzima, uwezo wa kubuni, kujadili, kuamua na kutoa Miongozo ya Siasa ya CCM katika mam bo mbalimbali. (2) Kueneza Itikadi na Siasa ya CCM, mafunzo ya Siasa ya CCM na kukuza nadharia na Itikadi ya CCM ya Ujamaa na Kujitegemea. Ndele Mwaselela ni Mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM Taifa (NEC) kutoka Mkoa wa Mbeya ame kuwa ni mdau wa maendeleo akisaidia jamii katika nyanja mbalimbali. Ni kiongozi kijana mwenye uwezo mkubwa wa kutafsiri kwa vitendo maono ya Mwenyekiti wake wa CCM Taifa na kuwafikishia wananchi nchi nzima. Hivi karibuni kafanya ziara zake katika Wilaya ya Mbeya Vijijini pamoja na Visiwani Zanzibar. Mbeya Vijijini pamoja na mambo mengine kafani kisha kuwaweka pamoja vijana wa Wilaya nzima kwa kuwaanzishia Ligi ya Mpira wa miguu inayoju likana kwa jina la Dr. Samia Mbeya DC Mshikama no CUP. Ligi hiyo itagharimu zai...

Mnec Mwaselela-Dkt,Samia Suluhu na Dkt,Mwinyi ni viongozi wa kuigwa Afrika

Image
Na Ibrahim Yassin,Mbeya. Mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM Taifa (NEC) Ndele Mwaselela (MNEC) amesema.Rais Dkt,Sam ia Suluhu na Dkt,Husein Mwinyi ni mfano wa kuig wa katika utekelezaji wa shughuri za maendeleo. Mwaselela akiwa ameongozana na mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM Taifa NEC jana kuwakilis ha Kundi la Vijana Muhusin Ussi (MNEC) Wamefi ka wilayani Dimani amesema kazi zinazofanywa na viongozi hao ni kubwa mno. Amesema amejionea utekelezaji mkubwa ea Ilani ya Chama Cha Mapinduzi Upande Wa Bara na Visi wani ambapo miradi mikubwa na ya kati imejeng wa kw kasi. Amesema viongozi hao wa kitaifa wamekuwa mfano bora wa Kuigwa barani Afrika katika kubo resha na kuibua fulsa za miradi mikubwa Inayole ta maendeleo kwa Taifa hili kama vile Barabara Kujengewa, Maji Kufika majumbani kwa wananchi umeme hadi ngazi ya Vijijini. Mwaselela ambaye alikuwa ni mgeni rasmi, katika hafla ya kufunga mafunzo ya darasa la Itikadi, am bapo amewapongeza wahitimu Wote na kuwa tun uku vyeti. Pia ametumia jukwa...