BIL,6 ZA RAIS SAMIA KUJENGA MRADI WA MAJI MOMBA WANANCHI WAPAGAWA.
Na Ibrahim Yassin,Momba
WANANCHI wa vijiji vitatu vilivyopo kata ya Msangano wilayani Momba mkoani Songwe,wameanza kupata matumaini ya kuondokana na kero ya maji baada ya serikali kujenga mradi mkubwa wa Msangano Naming’ongo kujengwa.
Wakazi wa maeneo hayo jana walimueleza katibu tawala wa mkoa wa Songwe,kuwa mradi huo utakapo kamilika utakuwa ni muarobaini kwao kwani wamekuwa wakitumia maji ya kwenye madimbwi kwa muda mrefu ambayo si safi na salama.
Sophia Silumbwe mkazi wa Msangano,alisema tatizo la ukosefu wa maji liliwasumbua muda mrefu walilazimika kutembea kilometa 4 kusaka maji ya kwenye madimbwi,hivyo aliiomba serikali kuharakisha mradi huo ili waanze kunufaika.
Julias Mtafungwa mkazi wa Naming’ongo’ alisema wametumia maji yasiyosalama kwa muda mrefu na kuugua homa za matumbo huku wakiwa na ugomvi wa kindoa baada ya wake zao kutoka usiku wa manane kusaka maji,hivyo mradi huo utakuwa ni mkombozi kwao.
Akizungumza wakati wa ziara ya katibu tawala mkoani humo.Kaimu meneja wa wakala wa maji na usafi wa mazingira (RUWASA) Mhandisi Beatus Katabazi alisema mradi huo wa maji Naming’ng’o Msangan o,unatekelezwa kwa fedha za serikali kuu ukiwa katika kata mbili yaani Msangano,Namin’ongo na Chitete.
Alisema vijiji vitakavyonufaika ni na mradi huo ni Msangano,Ipata,Ntinga,Chindi,Nkala,Makamba,Nami ng’ong’o na Yala,mkandarasi akiwa ni Jamta Construction Investment na Vumwe General za jijini Dar es Salaam.
Alisema kazi zinezotekelezwa ni ujenzi wa tenki lenye ujazo wa lita 1,000.0000.ujenzi wa nyumba ya mitambo,ufungaji wa Transifoma.ufungaji wa pampu,vituo vya kuchotea maji,uchimbaji wa mitaro na ulazaji wa mabomba yenye mtandao wa kilometa 74,978,
Katabazi alisema mradi huo unatekelezwa kwa gharama ya Tsh,6,132,891,450.00 na kuwa hadi sasa Tsh,1,723,372,930.50 zimelipwa ambapo Tsh,919,933,717.50 ni malipo ya awali (Advance payment) na Tsh,803,439,213.00 ni sehemu ya hati ya kwanza ya malipo (Internal payment setificate no 1) yanya thamani ya Tsh,2,503,527,645.38.
Aliongeza kuwa mradi huo unatekelezwa kwa siku 450 (miezi 15) ambapo umepangwa kukamilika Juni 30/2025 hata hivyo mkandalasi aliomba kuongezewa muda kutokana na changamoto mbalimbali ambapo amekubaliwa na kazi zinaendelea.
Alisema wanamshukuru Rais Dkt,Samia kwa kutoa kiasi hicho cha fedha kukamilisha mradi huo utakaoenda kumaliza tatizo la maji kwa wakazi wa vijiji hivyo ambao awali watumia maji yasiyo salama wakiyafuata umbali wa kilometa 4 hadi makolongoni.
Naye meneja wa wakala wa maji na usafi wa mazingira (RUWASA) Charlers Pambe aliwataka wananchi hao kuilinda miradi hiyo kwa kutunza mazingira kwenye vyanzo vya maji kwani serikali imesikia kilio chao,imeleta fedha kujenga mradi isitokee mtu ama watu kuharibu miundombinu na mazingira.
Katibu tawala mkoani Songwe Happines Seneda baada ya kuukagua mradi huo alipongeza nidhamu ya matumizi ya fedha na ubora wa mradi huku akimuagiza mkandarasi huyo kuongeza kasi ili wananchi waanze kuyatumia maji hayo.




Comments
Post a Comment