Posts

Showing posts from November, 2024

Radi yaua mmoja aliyekua amejihifadhi kwenye mti akijikinga na Mvua

Image
Na Ibrahim Yassin,Chunya Mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Gilagwenda dadii (27) mkazi wa kitongoji cha Itumpi kata ya Matundasi wilayani Chunya mkoani Mbeya amefariki dunia baada ya kupigwa na radi. Akizungumza leo 28/ Novemba 2024 ndugu wa marehemu huyo Rashid Samwel amesema ilikua saa 10 jioni ndugu yake alienda kutengeneza baiskeli kwa fundi alikutwa na umauti baada ya kupigwa na radi. Amesema akiwa chini ya mti uliokaribu na fundi huyo mvua ilianza kunyesha kwa kasi takribani dakika 30 ilikuja radi iliyosababisha umeme ukatike kwa muda na kusababisha kifo hicho. Amesema baada ya kifo hicho watu mbalimbali wakiwemo viongozi wa kata walisogea na nilipo mpekuwa mfukoni nilimkuta na pesa 50.000 na vidonge vya kutuliza maumivu kwani alikuwa ana fanya vibarua kuweka marudio kwenye Planti. Afisa mtendaji wa kata ya Matundasi Salu Ngele alisema yeye sio msemaji wa tukio hilo hivyo hawezi kuzungumza chochote licha ya kuwepo eneo la zahanati ulipopelekwa mwili huo. Diwani wa kata ya Matu...

Madereva halmashauri Nkasi wapewa somo kuyatunza magari na kufuata kanuni za kazi

Image
Na Israel Mwaisaka,Nkasi Kufuatia uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajia kufanyika Novemba 27 ya mwaka huu Halmashauri ya wilaya Nkasi imekarabati magari yote yaliyokua yameharibika huku madereva wakipewa somo namna ya kuyatunza magari hayo Ili yaweze kudumu Kwa muda mrefu. Akizungumza na Madereva hao afisa usafirishaji wa Halmashauri ya wilaya Nkasi Rashid Hand Masud amewataka Madereva hao kufuata kanuni za kazi yao ya udereva Kwa kuhakikisha magari hayo yanatunzwa na kuendesha Kwa ustadi huku wakiongozwa na kanuni za Utumishi wa Umma. Amesema dereva yeyote ambaye ataonekana kuendesha magari hayo kinyume na utaratibu unaowaongoza atanyang'anywa gari na kukabidhiwa mtu ambaye atakua na uwezo wa kuyaendesha magari hayo Kwa kufuata misingi ya kazi na kanuni za Utumishi wa Umma. Amemshukuru mkurugenzi mtendaji wa wilaya Afraha Hassan Kwa uamuzi wake wa kuyafufua magari yote yaliyokua yameharibika kiasi kwamba Kwa Sasa Kila dereva ana gari lakini pia itarahisisha shughuli za Halmash...

Wasimamizi wa vituo vya kupigia kura Kalambo wametakiwa kuwa waadilifu na wazalendo

Image
Na Baraka Lusajo,Kalambo Msimamizi wa uchaguzi Halmashauri ya Kalambo Mkoani Rukwa Ndg.Shafi Mpenda amewataka wasimamizi wa vituo vya Uchaguzi Wilayani humo kuzingatia nidhamu na uadilifu ikiwa ni pamoja na kujiepusha na ulevi wakati wa zoezi la uchaguzi wa Serikali za mitaa linalotarajiwa kufanyika Novemba 27/2024. Ameyasema hayo wakati wa semina ya kuwajengea uwezo wasimamizi wa vituo vya kupigia kura Wilayani humo na kusisitiza wasimamizi hao kuzingatia nidhamu ikiwemo kufungua vituo vya kupigia kura kwa wakati sambamba na kujiepusha na uchukuaji wa video na picha kwenye nyaraka za Serikali. Mkuu wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Wilayani humo Bi. Lupakisyo Mwakyolile ametumia fursa hiyo kuwataka wasimamizi wa vituo vya kupigia kura kuzingatia miongozo iliotolewa na Serikali ikiwemo kulifanya zoezi hilo kwa uaminifu na kwa uadilifu sambasambana kujiepusha na vitendo vya Rushwa kwa lengo la kupata viongozi bora na wenye tija katika jamii na taifa kwa ujumla. Awal...

DC ITUNDA AWATAKA VIJANA KUSHIRIKI SHUGHULI ZA MAENDELEO NA KUPAMBANA DHIDI YA UKATILI.

Image
Na Ibrahimu yassin,Songwe Mkuu wa Wilaya ya Songwe, Mhe. Solomon Itunda amewataka vijana hususani wahitimu wa mafunzo ya Jeshi la Akiba kushiriki shughuli za maendeleo na kupambana dhidi ya wanaofanya ukatili katika jamii. Dc Itunda mbali na kuwataka vijana hao kushiriki shughuri za maendeleo pia amawataka  kuimarisha ulinzi na kuwa kielelezo cha matendo mema katika jamii zao. Mhe. Itunda alitoa wito jana  wakati akifunga mafunzo ya  Jeshi la Akiba 2024 katika Kata ya Gua  Wilayani Songwe. Vijana 119 wamehitimu leo mafunzo ya awali ya Jeshi la Akiba katika Wilaya ya Songwe baada ya kupata mafunzo kwa miezi minne. Akizungumza katika hafla hiyo, Mhe. Itunda amewataka vijana hao kuzingatia mafunzo hayo ili yakawe na tija katika maisha yao na jamii. Amesema kuwa vijana hao 119 wamepata stadi mbalimbali za kuwasaidia katika maisha yao ambao pia watasaidia kuimarisha usalama katika Kata ya Gua hali itakayochochea kukua kwa uchumi. Mkuu huyo wa Wilaya amewasisitiza wahitimu hao kufanyia kazi ...

Wataalamu wa hospitali ya Rufaa ya kanda Mbeya wawasili Chunya kwenye kambi ya matibabu ya mtoto wa jicho,zaidi ya Wagonjwa 500 kunufaika na kambi hiyo

Image
Wataalamu kutoka Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya leo wamewasili wilayani Chunya Mkoa wa Mbeya kutoa huduma mkoba ya matibabu ya kibingwa ya mtoto wa jicho kwa siku 7, ambapo zaidi ya wagonjwa 500 wanatarajiwa kunufaika na kambi hiyo inayoratibiwa na Shirika la Helen Keller International (HKI) kwa kushirikiana na Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya, Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya, na kufanyika katika Hospitali ya Wilaya ya Chunya, ikiwa ni juhudi za kupunguza tatizo la upofu nchini Tanzania inatarajiwa kufanyika kwa siku saba Akiongea na washiriki wa kambi hiyo Daktari Bingwa wa macho na Kiongozi wa timu ya wataalamu hao Dkt. Barnabas Mshangila ameeleza kuwa kambi hiyo inatoa fursa kwa wagonjwa wengi ambao hawana uwezo wa kugharamia matibabu ya Mtoto wa jicho na kuwasaidia kuondokana na matatizo hayo na kuboresha maisha yao kupitia upasuaji wa mtoto wa jicho. “Timu imejipanga vizuri katika kutoa huduma za matibabu ya kibingwa. Tumejipanga kwa kila hali na tunatarajia kutoa huduma ...

GOVERNMENT CANCELS 1,505 MINING BLOCK LICENSES, SMALL-SCALE MINERS TO BENEFIT

Image
By Ibrahim Yassin,Chunya The government, through the Ministry of Minerals, has revoked 1,505 mining block licenses in Chunya District, Mbeya Region. The blocks, previously abandoned by wealthy miners, will now be redistributed to Mbeya small-scale miners (Mberema).   Chunya District, known for its mining economy, heavily relies on gold extraction for its financial stability.   This announcement was made during an interview with Saddam Kyando, the newly elected chairman of the small-scale miners' association, in his office in Chunya.   Kyando expressed his delight at the government's decision, noting that redistributing these blocks will create opportunities for small-scale miners, many of whom lack mining licenses. He emphasized the need for miners to join Mbelema to ensure they benefit from this initiative.   "Our focus is to unite miners and resolve issues through structured channels, avoiding protests. We plan to visit every ward to encourage miners to register under ou...

LEZENI ZA VITALU 1,505 ZA VIGOGO ZAFUTWA, MBELEMA KUNUFAIKA.

Image
Na Ibrahim Yassin, Chunya SERIKALI Kupitia wizara ya madini yafuta jumla ya leseni za vitalu 1505 wilayani Chunya mkoani Mbeya baada ya kutelekezwa na badala yake vitagawiwa kwa wachimbaji wadogo (MBELEMA). Imeelezwa kuwa vitalu hivyo vilikua vikimilikiwa na wachimbaji wenye fedha nyingi (Madigala) na  utaratibu wa kuwagawia wachimbaji wadogo unafanyika. Wilaya ya Chunya ni moja ya wilaya inayounda mkoa wa kimadini nchini ambayo asilimia kubwa ya uchumi wake unatokana na uchimbaji wa madini ya dhahabu. Hayo yamebainika  jana katika mahojiano na mwenyekiti mteule wa chama cha wachimbaji wadogo Saddam Kyando ofisini kwake wilayani humo. Kyando amesema kitendo cha Serikali kutoa vitalu hivyo kwa wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu yaliyokuwa yakimilikiwa na watu wenye uwezo mkubwa kifedha kimewafurahisha. Ameeleza vitalu hivyo vitatoa fursa za kwa wachimbaji ambao wengi wao hawana leseni na kwamba kazi yao kwa sasa ni kuhamasisha wachimbaji kujiunga na Mbelema ili wasipitwe na fursa hi...

UMOJA WA WANAWAKE SOKO LA DHAHABU CHUNYA WATOA MISAADA KWA YATIMA.

Image
Na Ibrahim Yassin, Chunya  UMOJA wa Wanawake (Chunya Queens) katika soko la madini ya dhahabu wilayani Chunya mkoani Mbeya, wametoa misaada ya vitu mbalimbali vikiwemo vyakula vyenye  thamani ya zaidi ya Milioni 2 kwa watoto yatima. Akizungumza  jana na Dirakamilifu, mwenyekiti wa umoja huo  Jelroline Charles amesema wao ni wafanyakazi wanawake katika soko la ununuzi wa madini, wameanzisha umoja huo kwa ajili ya kusaidiana. Amesema licha ya kusaidiana kwenye shida na raha pia wameweka ajenda ya kusaidia yatima na watu waishio kwenye mazingira magumu . Amesema hivi juzi tu walienda kwenye kituo cha kulelea watoto yatima kilichopo Itua jijini Mbeya ambapo walitoa mchele, unga, sukari, mafuta, sabuni na Pedi zikiwa na thamani ya zaidi ya milioni 2. Amesema baada ya kutoa vitu hivyo pia waliweza kula nao chakula pamoja ikiwa ni pamoja na kuwatia moyo watoto hao ambao wengi wao ni walemavu wa viungo. Nae katibu wa kikundi hicho Dolla Gibson amesema lengo kuu la umoja huo ni kusaidiana kweny...

Wanunuzi wa dhahabu Chunya waomba kuwekewa huduma za kibenki kurahisisha kazi zao

Image
Na Ibrahim Yassin ,Chunya WANUNUZI wa madini ya dhahabu katika soko la.madini wilayani Chunya mkoani Mbeya, wameiomba serikali kupitia wizara ya madini kuweka huduma za kibenki katika soko hilo ili kurahisisha ufanyaji kazi. Akizungumza jana na DiraKamilifu Msafiri Miraji amesema soko hilo ni kubwa na lina wanunuzi hai 52 hivyo waliomba vyumba vingine vitengwe kwa ajili ya kuwekwa matawi ya taasisi za kibenki. Amesema ili kurahisisha ufanyaji kazi na usalama wa fedha zao ni bora ofisi za kibenki ziwekwe kwenye soko hilo kama ilivyo soko la Geita ambapo wataweza kuendesha shughuri zao kiurahisi zaidi. Aidha Miraji amesema ipo haja serikali kupitia wizara ya madini kutoa elimu kwa wachimbaji wadogo juu yanuelewa wa matumizi ya kemikali migodini ili wajue matimizi sahihi kuhepuka mad hata. Kwa upande wake Sayenda Haroun mnunuzi wa madini amesema licha ya kuhitaji taasisi za kibenki kuwepo kwenye soko hilo pia aliomba ofisi ya madini kuongeza kipimo cha madini kupunguza msongamano. Harou...

MADIWANI NKASI WAMEWAFUKUZA KAZI WATUMISHI WAWILI KWA UTORO KAZINI

Image
Na Israel Mwaisaka,Nkasi BARAZA la Madiwani la halmashauri ya Nkasi mkoani Rukwa limewafukuza kazi watumishi wawili wa idara ya afya kwa utoro kazini. Akitoa taarifa ya kufukuzwa kwa watumishi hao baada ya baraza hilo kujigeuza na kuwa kamati mwenyekiti wa halmashauri Pankrasi Maliyatabu aliwataja Watumishi hao kuwa ni Atanasi Ignas Mgunda Mteknolojia msaidizi na Japhet Masud Kimondo ambaye ni tabibu msaidizi. Amesema kuwa Watumishi hao wawili wamekua watoro kazini kwa kipindi kirefu ambapo atanasi Mgunda yeye ni mtoro kazini tangu Januari 2024 na Japhet Kimondo yeye hajaonekana kazini toka March,2024. Mwenyekiti huyo wa halmashauri aliutumia mwanya huo kuwatahadharisha watumishi wazembe na watoro kuwa watashughulikiwa huku akidai kuwa sheria inaelekeza kuwa mtumishi mtoro kazini shauri lake lianze kusikilizwa ndani ya siku 5 za utoro wake na siku 90 afukuzwe kazi. Mkurugenzi mtendaji wa wilaya Afraha Hassan kwa upande wake alidai kuwa halmashauri yake kwa sasa kati ya mambo inayoyas...

TCB Supports Sports Development in Songwe Region.

Image
By Ibrahim Yassin ,Songwe The Tanzania Commercial Bank (TCB) has donat ed sports equipment, including jerseys and balls, to Songwe Region in an effort to boost the growth of sports in the area.   Speaking on behalf of the bank's Chief Executive Officer, Daniel Mihayo, Simon Mlelwa, the Manage r of TCB Mwanjelwa Branch in Mbeya Region, said they received a request for sports equipment to promote sports development in the region.   "As TCB, we have a practice of giving back to the community to address various challenges affectin g our society," Mlelwa said. He added that through its Corporate Social Responsibility (CSR) program, the bank focuses on health, education, and social welfare.   Receiving the equipment, Songwe Regional Com missioner Daniel Chongolo commended TCB for their support and highlighted that Songwe, being a newly established region, faces multiple challen ges and needs additional assistance to achieve its goals.   "As regional leaders, we have a resp...

TCB BENKI YAUPIGA JEKI MKOA SONGWE VIFAA VYA MICJEZO

Image
Na Ibrahim Yassin, Songwe Katika kuendeleza tasnia ya michezo Mkoa wa Songwe, Benki ya Biashara Tanzania yaani Tanzania Commercial Bank (TCB), imetoa vifaa mbali mabli vya michezo kama jezi na mipira kwa mkoa wa Songwe. Simon Mlelwa Meneja wa TCB Tawi la Mwanjelwa, Mkoa wa Mbeya, kwa niaba ya Mtendaji Mkuu wa benki hiyo Daniel Mihayo, alisema walipokea ombi la vifaa vya michezo katika kudumisha michezo. “Na sisi kama TCB kila mwaka tuna utaratibu wa kurudisha faida kwa jamii kutokana na kile tuna chekipata katika biashara tunayoifanya ya fedha, ili kuweza kutatua changamoto zinazoikumba jamii yetu,” amesea Mlelwa. Amesema kuwa katika program ya kurudisha faida kwa jamii (CSR)imejikita katika maeneo matatu ambayo ni afya, elimu na ustawi wa jamii. Kwa hiyo, kama maombi yaliowafikia benki hiyo wamefika leo kukabidhi vifaa vya michezo ambavyo ni jezi pesa kadhaa na mipira katika kuhakik isha Mkoa wa Songwe mbele kimichezo. Akipokea vifaa hivyo, Mkuu wa Mkoa wa Songwe Daniel Chongolo amese...