Viongozi wa vijiji waonywa kujigeuza mahakama
Na Israel Mwaisaka,Nkasi MWENYEKITI wa halmashauri ya wilaya Nkasi Pankrasi Maliyatabu amewataka viongozi wa vijijji na kata kuacha kuutumia muda mwingi kukaa ofisini na kusikiliza kesi na kuacha jukumu lao la msingi la kuhamasisha na kusimamia maendeleo na jukumu hilo la kesi wangeziachia Polisi na Mahakama. Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara katika vijijji vya Mkole na Ipanda kata ya Nkomolo amedai kuwa shughuli nyingi za maendeleo zimekuwa zikisuasua na kumbe viongozi wa vijiji na kata wamejigeuza na kuwa ni Polisi na Mahakama wakati mamlaka hizo zipo na kupelekea shughuli za maendeleo kukwama katika maeneo yao. Hilo limekuja baada ya mkazi mmoja wa kijiji cha Ipanda Michael Mhoja kumweleza mwenyekiti wa halmashauri kuwa kukwama kwa ujenzi wa zahanati kijijini hapo kumetokana na viongozi wao wa kijiji kuutumia muda mwingi kusikiliza kesi ofisini na kushindwa kabisa kusimamia shughuli za maendeleo. Kufuatia hari hiyo mwenyeki wa halmashauri aliutumia mwanya huo kuwapiga marufuku v...