Posts

WANANCHI KYELA WAIHARAKISHA MIRADI YA MAJI HASA CHANZO CHA ZIWA NYASA KULINDA AFYA ZAO.

Image
                       MAKALA ‘’Tumechoka kuugua homa za matumbo kwa kunywa maji yasiyo salama,mchakato wa chanzo cha ziwa nyasa uharakishwe,tulinde afya zetu’’. Na Ibrahim Yassin,Kyela WANANCHI wa Tarafa zote mbili za Unyakyusa (Kyela mjini, na Ntebela Kyela vijijini) zilizopo wilayani mkoani Mbeya,wameiangukia Serikali wakihitaji miradi ya maji iharakishwe wajikwamue na kuugua homa za matumbo kwa kunywa maji yasiyo salama. Asilimia kubwa ya wakazi wa Kyela hasa vijijini wanatumia maji ya visima vilivyochimbwa kienyeji ambavyo usalama wake kiafya ni mdogo huku maji ya bomba yakiwa ya shida hali inayopelekea waugue homa za matumbo. Kwa wakazi waliopo Kyela mjini baadhi yao wamekuwa wakiyatibu maji kwa kuweka dawa katika visima na wale wasiokuwa na uelewa huo nao wameingia kwenye tatizo hilo la kuugua homa za matumbo hasa watoto wadogo. Wilaya ya Kyela yenye kata 37 za kichama na kata 33 za kiserikali ikiwa na Tarafa mbili,Ntebela Kyela vijijini na Unyakyusa Kyela mjini ikiwa na vitongo...

Wananchi kata ya Mkinga wajenga ofisi tano za kisasa za vijiji kwa kujitolea

Image
‎ Na Israel Mwaisaka, Nkasi ‎ ‎Kamati ya maendeleo ya kata (WDC) kata ya Mkinga wilayani Nkasi mkoani Rukwa imefanikiwa kuwahimiza Wananchi kujenga ofisi za Kijiji za kisasa kwa Kila Kijiji kwa njia ya kujitolea na ofisi hizo kukamilika. ‎ ‎Akizungumza na Waandishi wa habari Diwani wa kata hiyo Mohammed Zaid alisema kuwa mpango huo uliazimiwa kwenye vikao vya maendeleo ya kata na Wananchi wakaupokea mpango huo kwa moyo mmoja na kuanza utekezaji wa mpango huo ‎ ‎Alisema kuwa viongozi wa vijiji waliamua kuusimamia mpango huo kwa weredi ambapo waliweka utaratibu wa uchangishaji wa Fedha ikiwa ni pamoja na nguvu za Wananchi. ‎ ‎Alisema kuwa kutokana na jitihada zilizoonyeshwa na Wananchi halmashauri kupitia mfuko wa jimbo iliamua kusapoti jitihada hizo kwa Kutoa mifuko 20 ya saruji kwa Kila kijiji ambazo zilitumika kwenye umaliziaji wa ujenzi na kufanikiwa kuwa na ofisi nzuri na za kisasa kwa Kila Kijiji. ‎ ‎Awali Mwenyekiti wa Kijiji Cha Mkinga Alex Maziku alidai kuwa ofisi zao za Kiji...

Matumizi ya stendi kuu ya mabasi Katumba kuanza Julai mosi mwaka huu

Image
Na Benjamini Mwamwezi, Rukwa ‎ ‎Serikali imeahidi kuboresha sekta ya usafiri na usafirishaji katika Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga kwa kuanza rasmi matumizi ya Stendi Kuu ya Mabasi Katumba kuanzia Julai 1, 2026. ‎ ‎Hatua hiyo itaenda sambamba na kufungwa kwa stendi ya Sokomatola ili kupisha utekelezaji wa mipango mingine ya maendeleo iliyokusudiwa na Serikali. ‎Mpango huo unakuja kufuatia maombi ya Wananchi yaliyotolewa Machi 8, 2026 wakati wa ziara ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, ambapo walisisitiza matumizi kamili ya stendi ya Katumba iliyogharimu Shilingi Bilioni 8.993. ‎ ‎Akizungumza katika kikao na wadau wa usafirishaji Aprili10, 2026, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga Nassir Kirusha, amewapongeza wadau hao kwa juhudi zao za kujiletea maendeleo na kusisitiza kuwa Serikali inaendelea kuimarisha miundombinu na fursa za maendeleo kwa lengo la kufungua fursa za kiuchumi kwa wananchi. ‎Amesema matumizi ya st...

CCM Mbozi yataka kuimarishwa kwa usimamizi wa miradi ya maendeleo.

Image
Na Moses Ng’wat, Mbozi. KAMATI ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mbozi imeridhishwa na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa wilayani humo, huku ikitaka kuimarishwa zaidi kwa usimamizi ili kudhibiti kasoro ndogo ndogo. Kauli hiyo ilitolewa Aprili 1, 2026 na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mbozi, Majaliwa Mlawizi, kwa niaba ya wajumbe wa kamati hiyo, wakati wa ziara ya kukagua miradi ya maendeleo katika Jimbo la Mbozi, chini ya Halmashauri ya Wilaya hiyo. Akizungumza baada ya kukagua mradi wa ujenzi wa vyumba viwili vya maabara katika Shule ya Sekondari Msanyila, Mlawizi alisema kamati imeridhishwa na hatua iliyofikiwa na kusisitiza umuhimu wa kuendelea kusimamia miradi hiyo kwa umakini zaidi ili kuhakikisha inakamilika kwa ubora unaotakiwa. Aidha, aliwapongeza watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi pamoja na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya, chini ya Mkuu wa Wilaya, Hamad Mbega, kwa usimamizi mzuri wa miradi inayotekelezwa kwa fedha kutoka Serikali Kuu. Kwa...

FIFA, TFF waanza utambuzi wa vipaji Rukwa.

Image
Na Israel Mwaisaka, Nkasi. Zoezi la utambuzi wa vipaji vya soka kwa watoto wa kike na kiume wenye umri wa miaka 12-16 limeanza mkoani Rukwa, likilenga kuandaa wachezaji wa baadaye wa timu za taifa. Zoezi hilo linaendeshwa chini ya wataalam kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA), ambapo mchakato wa awali wa ulianza rasmi ngazi ya halmashauri katika wilaya nne za mkoa wa Rukwa kuanzia Machi 12, 2026. Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa zoezi hilo, Mkuu wa Idara ya Utambuzi wa Vipaji kutoka TFF, Gidion Ngereza, alisema kuwa jumla ya watoto 180 walichaguliwa kuendelea kwenye hatua ya mkoa, iliyoanza Machi 16, 2026 na kuendelea kwa siku tano mkoani humo. Ngereza alisema kuwa lengo kuu la zoezi hili ni kutafuta wachezaji wa kike na kiume wenye vipaji ambao wanaweza kuingia kwenye timu ya taifa ya vijana. Aliongeza kuwa zoezi hili linafanyika katika mikoa 32 na halmashauri 184 kote nchini. Aidha, Ngereza aliwahimiza wazazi na...

SERIKALI KUWEKA UZIO WA UMEME KUTHIBITI TEMBO HIFADHI YA LWAFI. ‎

Image
‎ Na Israel Mwaisaka, Nkasi  ‎ ‎Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Nkasi Mkoani Rukwa Ndugu Afraha Hassan amesema Serikali inakusudia kuweka uzio wa umeme wenye thamani ya shilingi Billioni 7 katika kata tano (5) zinazozunguka maeneo ya hifadhi ya Lwafi ambao utasadia kudhibiti Wanyama waharifu aina ya Tembo kuharibu mazao ya wananchi. ‎ ‎Aliyasema hayo wakati wa mkutano wa hadhara uliokuwa na lengo la kusikiliza na kutatua kero za wananchi katika maeneo hayo na kusema uwepo wa uzio huo utakuwa suluhisho la kudumu katika kuwadhibti Wanyama hao na kuwataka wananchi kuendelea kuwa na subra wakati swala hilo likiendelea kufanyiwa kazi. ‎ ‎‘’suluhisho la kudumu litapatikana baada ya kuwekwa uzio wa umeme ni waya mfupi unaopitishwa kwenye vigingi, unakuwa mmoja au miwili, tembo akifika unampiga shoti,hivyo anakuwa anashindwa kuvuka Gharama yake ni kubwa ni takribani Billion saba hivi’’alisema Hassan. ‎ ‎Kwa upande wake Afisa Wanyama Poli Wilayani humo  Anod Shadrack Ngagashi,al...

WAZIRI MKUU KUANZA ZIARA MKOANI RUKWA KUANZIA MARCHI 8 HADI 10 AMBAPO ATAKAGUA MIRADI YA MAENDELEO NA KUZUNGUMZA NA WANANCHI

Image
‎ ‎Na Israel Mwaisaka,Rukwa ‎ ‎Waziri Mkuu, Dkt,Mwigulu Lameck Nchemba, anatarajia kufanya ziara ya kikazi Mkoani Rukwa kuanzia Machi 8 hadi 10, 2026. ‎ ‎Akitoa taarifa ya ziara hiyo mbele ya waandishi wa habari leo Machi 7, 2026, Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Charles Makongoro Nyerere, amesema ziara ya Mheshimiwa Waziri Mkuu inalenga kukagua maendeleo ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo, kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi na kusikiliza wananchi kupitia mikutano ya hadhara. ‎ ‎Katika taarifa yake, RC Makongoro ameeleza kuwa tarehe 8 Machi Waziri Mkuu atatembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Sumbawanga na Soko la Kimataifa la mazao Kanondo, na kisha kufanya mkutano wa hadhara katika Mji Mdogo wa Laela, Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga. ‎ ‎Tarehe 9 Machi Waziri Mkuu anatarajia kutembelea Wilaya ya Nkasi, kuweka jiwe la msingi la Shule ya Amali ya Mkoa iliyoko Namanyere na kufanya mkutano wa hadhara ambapo Pia atakagua Bandari ya Kasanga na kuzungumza na wa...