WAKUFUNZI SCOUT WAJENGEWA UWEZO KUENDANA NA MTAALA MPYA WA ELIMU-ELIMU YA AMALI



Na Israel Mwaisaka,Rukwa

WAHITIMU wa mafunzo ya Scout wilaya Nkasi wametakiwa kuitumia elimu waliyoipata katika kuwajenga vijana wa Scout mashuleni Ili yaweze kuwanufaisha katika maisha Yao hasa katika kipindi hiki ambacho kina mtaala mpya wa Elimu ya mafunzo ya amali.

Hayo yamesemwa na kaimu afisa elimu sekondari wilaya Nkasi Fortunatus Kaguo alipokuwa akifunga Kambi ya siku Nne ya Scout Wakufunzi katika shule ya sekondari.

Nkasi ambapo amedai kuwa wao kama wahitimu Wakufunzi wanayo nafasi kubwa ya kuyatumia mafunzo hayo katika kuwajenga vijana wa Scout na kuwa Watu makini na wenye uwezo mkubwa katika kuchakata masuala mbalimbali ya kimaisha.



Amesema kuwa Scout inayo nafasi kubwa ya kumtengeneza kijana kuwa mbunifu na hakiri na kuwa katika kipindi hiki ambacho mtaala mpya wa Elimu unakwenda kufanya kazi wa Elimu ya amali mafunzo ya Scout yanayo nafasi kubwa ya kuwatengeneza vijana.

Mkufunzi wa mafunzo kitaifa ALT. Edmak Mwamalala kwa upande wake amesema kuwa wahitimu wa mafunzo hayo wamepata mafunzo ya kutosha ambayo yatawawezesha kutoa mafunzo stahiki kwa Watoto na wakawa bora zaidi.

Amesema kuwa mafunzo hayo yamejikita Katika maeneo mbalimbali yatakayowawezesha Wakufunzi hao kutoa elimu ya kutosha kwa vijana ambayo yatawasaidia kwa kiasi kikubwa vijana kuwa wakakamavu ikiwa ni pamoja na uwezo wa kukabiliana na maisha kulingangana na mazingira watakayokuwepo.

Awali kamishina wa Scout mkoa Rukwa Hassan Shaban Kikoloma alidai kuwa wahitimu wa mafunzo hayo ya PTC wapo 20 kutoka katika shule mbalimbali za sekondari na kuwataka Wazazi wawaruhusu Watoto wao kujiunga na mafunzo ya Scout kutokana na umuhimu wa mafunzo hayo Katika kuwajenga vijana kuja kuwa Watu makini kwa ujenzi wa taifa.

Pia amedai kuwa Ili Scout iweze kufanya vizuri inahitaji Sana ushirikishwaji wa Wadau mbalimbali na kuwa ni muhimu kwa Kila mmoja katika nafasi yake kushiriki katika kuona kwamba Scout inaendelea na kuleta tija na kuweza kuyafikia malengo yake

Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa