MAAFISA MICHEZO WALIOGOMA KUSHIRIKI MAFUNZO YA MICHEZO YA MPIRA WA MIKONO WAONYWA.

Baraka Lusajo,Kalambo

Mkurugenzi mtendaji halmashauri ya Kalambo mkoani Rukwa shafi Mpenda amewaonya maafisa michezo waliogomea kushiriki kozi ya michezo ya mpira wa mikono (handball) licha ya serikali kugharamia ada na fedha za uendeshaji na kuelekeza kuchukuliwa hatua za kinidhamu ikiwemo kujieleza kwa maandishi pamoja na kubadirishiwa majukumu yao ya kazi.

Ameyasema hayo wakati akihitimisha kozi ya mpira wa mikono(handball) yaliofanyika wilayani humo kwa kushirikisha maafisa michezo 45 kutoka mikoa ya Rukwa, Songwe, Njombe na Iringa,Kozi iliyofanyika katika shule ya Sekondari Matai na kuwakilishwa na Afisa Utawala na Rasilimali Watu Ndugu Amandus Mtani na kusisitiza maafisa michezo kuzingatia nidhamu na uwajibikaji mahali pa kazi.

Aidha amesema serikali itaendelea kutoa vifaa vya michezo ikiwemo mipira na kwamba katika mwaka wa fedha 2025/2026 serikali imetenga fedha kiasi cha shilingi 37,641,760 kwa ajili ya kuimarisha michezo wilayani humo na kusisitiza maafisa michezo kuendelea kuwawezesha wanafunzi ili kuinua vipaji vyao ambavyo vitawawezesha kujiajiri wenyewe kupiti michezo.

Maafisa michezo waliohudhuria kozi hiyo,wameipongeza serikali kwa kuwezesha upatikanaji wa mafunzo hayo ambayo yatawesha kuinua vipaji vya wanafunzi shuleni.

Kozi hiyo imefanyika kwa muda wa siku nne yakishirikisha maafisa michezo 45 yakiwa na lengo ya kuwajengea umahili walimu wa michezo pamoja na kupata makocha na waamuzi bora wa mchezo wa mpira wa mikono (Handball).


Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa