TAcRI yatakiwa kujikita kwenye utafiti wa afya ya udongo ili kuongeza uzalishaji wa kahawa
MAKALA
.SERIKALI IWAONGEZEE UWEZO WATAFITI WA UDONGO/MBEGU KUONGEZA TIJA KWA WAKULIMA,MADADIRIKO YABIA YA NCHI YATAJWA.
.UONGOZI NA WADAU WA KILIMO WAPAMBANA KUREJESHA HESHIMA YA SONGWE KWENYE ZAO LA KAHAWA,MIKAKATI UGAWAJI MBEGU CHOTARA YAFANA.
Na Ibrahim Yassin,Songwe
WAKULIMA na wadau wa zao la Kahawa mkoani Songwe wameiomba serikali kupitia taasisi ya utafiti wa Mbegu (TAcRI) kuwawezesha wataalam kufanya tafiti za afya ya udongo ili kuongeza tija ya zao hilo..
Mkoa wa Songwe kupitia wilaya ya Mbozi inashika nafasi ya pili kitaifa kwa uzalishaji wa zao la Kahawa licha ya siku za hivi karibuni uzalishaji wake ulisuasua huku wakulima wakiwa na uhaba wa mbegu.
DISMAS Pangalas ni meneja wa kanda wa Taasisi ya utafiti wa Mbegu (TAcRI) licha ya kukiri changamoto ya uhaba wa mbegu,lakini anaeleza mikakati waliojiweka kukabiliana na uhaba huo.
Anasema licha ya kuzalisha mbegu nyingi lakini haitoshelezi kwani mwaka jana walizalisha miche Milioni 8 kwa kanda nzima na wilaya ya Mbozi pekee walizalisha miche Milioni 3.36 lakini hata hivyo haikutosha.
Anasema kutokana na hilo, wamewaunganisha wakulima wakubwa na wa kati wamewa jengea uwezo na elimu kisha wamewapatia udongo na mbegu na wamezalisha miche itakayogawiwa kwa wakulima wadogo kupitia vyama vyao.
Kwa wilaya ya Mbozi pekee anasema kuna vyama 18 vya ushirika ambapo kikanda kuna vyama 26 na kuwa walifanya tafiti za aina 19 za mbegu na sasa wamepanda zaidi mbegu chotara aina ya Compact inayoimili magonjwa.
Anasema katika miaka ya hivi karibuni uzalishaji wa kahawa Mbozi ulishuka kutokana na hali ya Tabia nchi ikiwemo mvua kutonyesha kwa mbangilio kwani kahawa inatakiwa ipate mvua kwa miezi 6.
Anasema tatizo lingine ni kupitiliza kwa joto kwani mwaka 2023,/2024 kulikuwa na nyuzi joto 30 hadi 33 ambayo ni tatizo ilitakiwa iwe chini ya hapo ndiyo maana wameandaa mkakati wa kuleta kilimo cha umwagiliaji.
‘’Ndugu wanahabari serikali inatambua hilo hivyo mpango uliopo ni kujenga mabwawa kwenye mashamba ili kahawa iwe inamwagiliwa kukabiliana na mtawanyo mbaya wa mvua’’anasema Pangalas
HISTORIA YA ZAO LA KAHAWA NCHINI.
Meneja Pangalas anasema zao la kahawa liliingizwa nchini mwaka 1880 kupitia bandari ya Kilwa na wamishonary kutoka visiwa vya sherisheri baada ya kupandwa ikaungua lakini ikapandwa tena wilayani Moshi ilikubali.
Anasema kwa wilayaya ya Mbozi Kahawa iliingia mwaka 1910 hadi 1915 na kupandwa kijiji cha Mbozi (Mbozi mission) na Mr, Jesuit Benchman kutoa nchi za ulaya,na kuanza kusambaa maeneo mbalimbali na soko lake kubwa lipo ncini Japan na kungineko.
Anasema katika eneo la utafiti wa mbegu kanda ya nyanda za juu kusini makao makuu yapo wilayani Mbozi mkoani Songwe kijiji cha Mbimba likiwa na hekta 132 wakiwa na lengo la kuzalisha mbegu milioni 8 hadi 10 kwa mwaka.
Mbali na kuwa na mipango hiyo anasema walitoa elimu kwa wakulima kupanda mazao mseto (Mazao mchanganyiko) katika ekali moja wachanga nye migomba,Kahawa,Parachichi,mbogamboga na miti ya kivuli.
WAKULIMA WALIOWEZESHA KUPANDA VITALU WAELEZA.
Benald Haonga mkazi wa kijiji cha Mbozi (Mbozi Mission) anasema yeye ni mkulima wa Kahawa ambaye analima kilimo mseto kwa kuchanganya na parachichi pamoja na migomba huku akijikita zaidi katika uzalishaji wa miche ya kahawa na miti ya asili.
Anasema kutokana na zao hilo kushuka kwa wilaya ya Mbozi,wameingia mkataba na bodi ya Kahawa ikiwawezesha vifaa ikiwemo udongo,mbegu na uzio ambapo mwaka jana alifanikiwa kuzalisha miche 300,000 na mwaka huu amezalisha miche laki 3.5.
Mbali na kujihusisha na kahawa pia anasema anajishughurisha na upandaji wa miche ya miti ya asili kwa ajili ya kupanda maeneo yenye vyanzo vya maji ili kulinda uoto wa asili na kulinda mazingira akishirikiana na maafisa wa TSF.
Anasema changamoto iliyopo ni ukosefu wa elimu ya afya ya udongo ambapo wakulima wengi wanapanda kwenye udongo wenye wadudu na kupelekea kupata hasara kwa mazao yao kutochipua na hata ikichipua inkauka na kushambuliwa na wadudu.
Anasema miche hiyo inagawiwa kwa wakulima kupitia vyama vyao lengu likiwa ni kukabiliana na uhaba wa mbegu kwani taasisi ya utafiti TAcRI inapozalisha mbegu hazitoshelezi hivyo wameweka utaratibu wa kuwezesha wakulima wa kati kuzalisha mbegu ili kuondoa uhaba uliopo.
Chriss Nzunda mkulima kutoka kijiji cha Masangula anasema yeye pia aliingia mkataba na Taasisi ya utafiti wa mbegu na amefanikiwa kuzalisha miche laki 1 huku akiajili vijana wanaowezesha kufanya kazi hiyo.
Anasema yeye anashamba darasa la mazao mseto yaani Kahawa,mi gomba na parachichi ambavyo vimepandwa katika shamba moja na wakulima wadogo wanafika kujifunza namna ya upandaji huo.
Naye Tinson Nzunda mkulima kutoka kijiji cha Masangula ambaye nae ameingia mkataba na taasisi hiyo,yeye amezalisha miche 300.000 ambapo miche hiyo itagawiwa kwa wakulima ili kupunguza changamoto ya uhaba wa mbegu kutokana na muitikio mkubwa kwa wakulima kupanda Kahawa.
Nae Aloyce mdalavuma diwani na mkulima wa kata ya Bara,anasema amepanda miche laki 1 ya mbegu chotara ya Compac inayohimili magonjwa huku akipongeza bodi ya kahawa kwa kuwa karibu nao.
Ili zao hilo liendelee kuleta uchumi mkubwa kwa wakulima na kwa serikali kwa ujumla,ipo haja serikali kwa kuwawezesha watafiti wa udongo kuwaondoklea hasara wakulima na kupeleka pembejeo ikiwemo mbolea kwa wakati.
yassin.ibrahimu@yahoo.com 0718382817.




Comments
Post a Comment