Watumishi wa Umma wametakiwa kutunza siri za seriikali na uwajibikaji


Na Baraka Lusajo,Rukwa

Katibu tawala mkoani Rukwa Msalika Makungu amewataka watumishi wa umma katika Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo kuzingatia sheria na maadili ya utumishi wa umma kwa kuimarisha ushirikiano na uwazi wakati wa utekelezaji wa majukumu yao mahali pakazi ili kuongeza ufanisi wa kiutendaji.


Ameyasema hayo wakati akiongea na watumishi wa umma wilayani Kalambo mkoani Rukwa kupitia ziara yake ya kusikiliza na kutatua changamoto za watumishi mahali pa kazi na kuwataka wakurugenzi mkoani humo kufuata miongozo ya serikali wakati wa utekezaji majukumu yao kwa kuacha kuzalisha madeni ikiwemo kutohamisha watumishi bila uwepo wa bajeti.

Aidha ametumia fursa hiyo kuwataka watumishi wa umma kujenga utamaduni wa kuwahi kazini na kuondoka kulingana na muda uliopangwa na serikali na kusisitiza watumishi kuacha tabia ya kutamani kuhama na badara yake wajikite katika kujiimarisha kiuchumi kwa kuazisha shughuli mbliambali za uwekezaji na uzalishaji ambazo zitawawezesha kuongeza vipato vyao kawani Mkoa wa Rukwa una fursa nyingi za kiuchumi ikiwemo ardhi yenye rutuba kwa ajili ya kilimo, ufugaji na uwepo wa ziwa Tanganyika kwa ajili ya Uvuvi.


Kwa upande wake Katibu Tawala Msaidizi Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu mkoani humo ndugu Donald Nssoko ametumia fursa hiyo kwa kuwahimiza na kuwakumbusha watumishi wa umma kufanya kazi kwa kuzingatia maadili ya utumishi wa umma ikiwa ni pamoja na kujiepusha na viotendo vya utoaji wa siri za serikali kwani kufanya hivyo ni kosa kisheria.

Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa