Askari mstaafu (JWTZ) ajikita kwenye kilimo cha kahawa,awa mfano kwa Wakulima Mbozi
VIJANA ZAIDI YA 100 WAPATA AJIRA ZA MKATABA KUOTESHA MBEGU CHOTORA ZA COMPACT.
NZUNDA AWATAKA WAKULIMA WADOGO KUJIFUNZA KILIMO MSETO,SHAMBA LAKE LAWA SHAMBA DARASA.
Na Ibrahim Yassin,Songwe
‘’Nimeingia mkataba na taasisi ya utafiti (TAcRI) Nazalisha mbegu chotara nimeajiri vijana 100 wawalipa mshahara,shamba darasa la mazao mchanganyiko lipo wakulima waje kujifunza kiklimo mseto’’
ASKARI wa jeshi la wananchi (JWTZ) mstaafu aliyekuwa kwenye kitengo cha mizinga Chriss Nzunda,ajikita kwenye kilimo cha Kahawa na kutoa wito kwa wakulima kulitumia shmba darasa lililopo shambani kwake ili walime kilimo chenye tija,
Nzunda ametoa wito kwa wakulma wadogo na walio kwenye ushirika kufika shambani kwake Kijiji cha Masangula kata ya Nyimbili wilayani Mbozi mkoani Songwe ili waone na kujifunza namna ya kulima mazao mchanganyiko katika shqamba moja.
Alisema imezoeleka kuwa wakulima wengi wamekuwa wakima zao moja katika kila heka kumbe kulima mazao mchanganyiko inawezekana,hivyo ili kuondokana na kilimo cha aina hiyo amewataka wakulima wafike kujifuke kujifunza.
‘’Katika shamba langu nimelima Kahawa,parachichi,ndizi na mbogamboga kwa kufuata ushauri wa kuacha nafasi,wakati wa mafuno Napata kipato kikubwa kutokana na mazoa kuwa mengi,na pia nimepanda miche Zaidi ya 100.000 ya Kahawa zitagawiwa kwa wakulima’’alisema.
Alisema baada ya kustaafu Jeshi,alianza kujifunza kilimo na baadae bodi ya Kahawa kupitia Taasisi ya Mbegu (TAcRI) walimuwezesha udongo,mbegu,na uzio na ameajiri vijana 100 wanaofanya kazi hiyo akiwalipa kwa mkataba.
Naye Benard Haonga mkulima wa Kijiji cha Mbozi (,Mbozi Mission) kata ya Igamba,amesema kwa wilaya ya Mbozi kilimo cha zao la Kahawa ndiyo mkombozi wa wakulima na yeye ameanzisha shamba darasa,hivyo kuna kila sababu ya kuongeza uzalishaji.
Alisema baada ya kupata mafunzo kutoka bodi ya Kahawa kupitia taasisi ya utafiti wa mbegu (TAcRI) ameweza kupanda miche laki 1 ya mbegu chotara ya Compact na pia ameandaa shamba darasa la kilimo mseto na kuajiri vijana 50.
Anasema mbali na kuzalisha zao hilo,pia anazalisha miche ya miti ya asili kwa ajili ya kupanda maeneo yenye kuhifadhi uoto wa asili huku halmashauri ya Mbozi kupitia Idara ya misitu wanaichukua miche hiyo na kuipanda maeneo muhimu.
Alisema changamoto iliyopo ni kutojua afya ya udongo,hivyo anaiomba serikali iwaongezee uwezo watafiti ili wafanye utafiti wa afya ya udongo kuhepuka hasara kwa wakulima ambao mazao yao yanaharibika.
‘’Wakulima wamepata muitikio mkubwa mkubwa kutokana na manufaa ya mbegu chotara za Compati,ili kuongeza tija uzalishaji zaaidi wa mbegu ufanyike licha ya wao kuingia makata na TAcRI kwa kupewa udongo,Mbegu na Shed Net,wakaguzi wa ndani na nje wapiti mara kwa mara’’alisema.
Meneja wa kanda ya nyanda za juu kusini wa taasisi ya utafiti wa mbegu (TAcRI) Dismas Pangalas alisema baada ya wakulima kuwa na muitikio mkubwa waliingia mkataba na watu hao kuzalisha miche ili itosheleze wakulima na mpango uliopo ni kuandaa kilimo cha umwagiliaji.







Comments
Post a Comment