Mwanafunzi wa kidato cha Nne ajifungua na kumtupa Mtoto chooni
Na Israel Mwaisaka, Rukwa
Jeshi la Polisi mkoani Rukwa linaendelea kufanya uchunguzi wa kina juu ya binti ambaye ni Mwanafunzi wa kidato cha Nne (18) wa shule ya sekondari Nkasi ambaye amejifungua mtoto na kumtupia chooni .
Akizungumzia tukio Hilo Kamanda wa Polisi mkoani Rukwa Shadrack Masija amesema kuwa wiki iliyopita Mwanafunzi huyo akiwa mjamzito bila ya mtu yeyote kufahamu..
alijifungua mtoto Kisha mtoto huyo kumtupia kwenye choo cha shimo na yeye kuelekea shuleni kuendelea na masomo.
Amesema kuwa Watu walisikia sauti za mtoto huyo zikitoka ndani ya choo hicho na taarifa hizo ziliwafikia Polisi ambao walifika eneo la tukio na kumuokoa mtoto huyo ambaye yupo hai Hadi sasa.
Amesema kuwa baada uokozi huo uliofanyika mtoto huyo alikimbizwa hospitali kwa ajiri ya matibabu huku wakifanya uchunguzi wa aliyefanya kitendo hicho ndipo walipombaini Mwanafunzi huyo.
Kamanda Masija amedai kuwa binti huyo baada ya kuhojiwa alikiri kufanya tukio Hilo na kudai kuwa halifanya hivyo bila ya kujitambua na hajui Nini kilimfanya amtupe mtoto huyo chooni mara tu baada ya kujifungua .
Alidai kuwa kwa sasa Mwanafunzi huyo amekabidhiwa mtoto wake huyo kwa ajili ya kumnyonyesha na kuwa katika kuuliza uliza kwa Wataalamu wa afya wanadai kuwa huenda binti huyo alikumbwa na tatizo la afya ya hakiri wakati akijifungua .
Amesema kuwa Kuna wakati Mwanamke anapokuwa mjamzito ukumbwa na matatizo mbalimbali ya kiafya ikiwemo la afya ya hakiri na kuwa ndiyo maana wao kama jeshi la polisi wanalifanyia uchunguzi wa kina suala Hilo na kama itabainika kuwa alifanya kitendo hicho kwa kukusudia hatua Kali za kisheria zitachukuliwa ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani.

Comments
Post a Comment