JAMII YAASWA KUPANDA MITI YA ASILI KWENYE VYANZO VYA MAJI NA KINGO ZA MITO KULINDA UOTO WA ASILI
JAMII YAASWA KUPANDA MITI YA ASILI KWENYE VYANZO VYA MAJI NA KINGO ZA MITO KULINDA UOTO WA ASILI
''Mimi ni mkulima wa mazao mseto.pia naotesha michw ya miti ya asili, kutokana na uzoefu nilioupata,nahitaji kuwafundisha vijana ili nikifa vizazi vijavyo viweze kufanya kama anavyofanya kuhepuka majanga na kuendeleza kilimo''..
Na Ibrahim Yassin,Songwe
JAMII nchini imetakiwa kulinda vyanzo vya maji na kingo zake kwa kupanda miti ya asili kulinda na kutunza mazingira ili uoto wa asili usipotee na kusababisha majanga yanayoweza kuzuilika.
Imekuwa ni kawaida kwa baadhi ya jamii kuharibu mazingira kwa kuendesha kilimo hadi kwenye kingo za maji ikiwemo kukata miti ovyo na kuchoma mikaa hali inayosababisha kuzuka kwa ukame wa mvua na mazingira kuharibika.
Kauli hiyo imetolewa jana na mkulima bora wa khawa anayelima kilimo mseto Benard Haonga kutoka kijiji cha Mbozi kata ya Igamba wilayani Mbozi mkoani hapa wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye bustani za kuoteshea Miche ya Kahawa na miti ya asili lililopo Mbozi Mission.
Alisema jamii inatakiwa kutambua umuhimu wa kuilinda na kutunza mazingira ili kukabiriana na ukame kwani maeneo yaliyoharibiwa mazingira kwa kukata miti kumekuwa na ukame wa mvua na kusababisha inyeshe kwa mafungu.
‘’Mimi ni mkulima wa mazao mseto ninalima Kahawa,parachichi,Migomba na mboga mboga katika shamba moja, ninapovuna napata mazao mengi ya aina tofauti,ili nifanikiwe kuvuna mazao mengi mvua inatakiwa inyeshe ya kutosha hivyo endapo mazingira yataharibiwa tutaweza kukosa mvua’’alisema.
Alisema miungoni mwa miti anayoiotesha,ni ipunungu inatoa matunda ,parachichi ,machungwa, limao,mapera kwa ajili ya matunda na mkuyu,mpegere (zambarawe pori) Alibiziam na mikangazi (kaya) ni kwa ajili ya kupanda kwenye vyanzo ili kulinda uoto wa asili.
Haonga aliendelea kusema kuwa anafanya shughuri hizo kwa ushirikiano mkubwa wa halmashauri ya wilaya ya Mbozi kupitia maafisa kilimo ambao ndiyo wanaofika na kuichukua miti hiyo na kuipanda kwenye vyanzo,hivyo ameiomba jamii ifike shambani mwake kuchukua miche hiyo ili wakaipande badala ya kuiachia serikali pekee.
‘’Miti nafaida nyingi,ikiwemo kupata kivuli,hewa safi,kulinda mazingira na uoto wa asili,ili jamii ione umuhimu wa kupanda miti inatakiwa elimu kubwa ifanyike katika maeneo mbalimbali ikiwemo vijijini,mimi nimeweza kutembea maeneo mbalimbali kufanya kazi na taasisi nyingi na kupata uzoefu wa kutosha.
Aliongeza kuta kutokana na uzoefu alioupata anahitaji kuwafundisha vijana ili yeye atakapokufa vizazi vijavyo viweze kufanya kama anavyofanya kuhepuka majanga na kuendeleza kilimo..
Charles Ndimbwa Afisa wanyama pori kutoka ofisi ya mazingira wilayani Mbozi,anasema Haonga ni mdau muhimu wa mazingira na amekuwa akiotesha miche mingi ikiwemo ya asili,lakini ni ngumu mtu kuppanda kwenye vyanzo vya maji licha ya kuwapa hamasa.
Alisema suala la upandaji miti kwenye vyanzo ni la serikali kupitia idara ya kilimo lakini wamekuwa wakitoa elimu ya kupanda miti kwa kushirikiana na wadau kupitia viongozi wa vijiji na vitongoji na endapo miti inahitajika wanwaelekeza waifuate miche hiyo kwa kuwa ni bora na inazalishwa na kikundi cha Ndelule





Comments
Post a Comment