CCM Songwe wazungumzia mikakati ya uchaguzi,yawapoga pini wanaopitapita majimboni
‘’wabunge waliopo madarakani waache woga,hata wao wakati wanasaka ubunge walipita majimboni,kama walishindwa kutimiza ahadi wajiandae kuwa na hoja nyingi za kujibu kwa wananchi’’.
Na Ibrahimu Yassin,Songwe
CHAMA cha mapinduzi (CCM) mkoani Songwe kimeeleza mikakati iliyojiwekea kufuatia uchaguzi mkuu ujao huku kikiwapiga pini makada wanaodaiwa kupita majimboni na kwenye kata kujitangaza ili kujiwekea mikakati mizuri ya ushindi.
Akizungumza jana na waandishi wa habari,Katibu wa Siasa itikadi na mafunzo mkoani Songwe,Mwl, Yusuph Rajabu alisema mkoa umejiandaa vizuri kuhakikisha katika uchaguzi ujao hakuna kata wala jimbo watakalo lipoteza huku akisisitiza wanaccm kufuata sheria zilizopo kuhepuka migogoro.
Alisema ikiwa ccm inajipanga ili kuyalinda majimbo na kata zote wamepata taarifa za baadhi ya wagombea kupita pita kwenye majimbo na katakabla ya muda huku wengune wakitoa fedha na wengine wakidiliki kuwapa mabarozi laki 3 ili waachie nafasi zao na kupatikana mabarozi na wajumbe watakaokuwa upande wao.
Alisema kanuni ya itifaki ya ccm hairuhusi mambo hayo,na kwamba atakaye bainika atakatwa jina lake bila kujali yeye ni nani kwani mchakato wa utoaji fomu utaanza Juni 28/2025 utakuwa mchakato wa siku 5 na majina matatu ndiyo yatakayopitishwa.
Alisema chama kimeongeza idadi ya wajumbe zaidi ya 13.000 kutoka wajumbe 4.000 hivyo atashangaa kama kuna mgombea ataweza kuwahonga wajumbe wote hao’’ccm iliona ili ipate wabunge na madiwani wazuri bila kutoa hongo imeongeza idadi ya wajumbe.
‘’Ccm inajivunia mafanikio yake kupitia ilani yake kutekelezwa kwa vitendo katika kila idara na kujenga imani kwa wapiga kura wake,tunapinga vikali rushwa na uvunjifu wa kanuni zilizowekwa,natoa onyo kwa watakaopita na kufanya kampeni kabla ya muda majina yao hayatarudi’’.
Hata hivyo,baada ya kumalizika kwa kikao hicho cha waandishi wa habari,baadhi ya wanaccm ambao hawakutaka majina yao yaandikwe walisema baadhi ya wabunge wamekuwa na hofu ya kutorudi bungeni ndiyo maana wamekuwa wakilalamika pale wanapohisi wapinzani wao wanapita majimboni.
Walisema hata wao wakati wanasaka ubunge walipita kabla ya muda na wabunge waliokuwepo wakati huo hawakuweza kulalamika,na kuwa hawaoni sbabu ya wao kuwa na hofu,kama walishindwa kutekeleza ahadi kwenye majimbo yao wajiandae kuwa na hoja nyingi za kujibu kwa wapiga kura.
Walisema CCM kupitia kwa mwenyekiti wake ambaye ni Rais wa Jamhuri wa muungano wa Tanzania Dkt,Samia Suluhu amefanya kazi kubwa ya kujenga miradi mikubwa na midogo katika kila idara na ametimiza ahadi alizoahidi kwa wapiga kura wakati wakifanya kampeni yeye na mtangulizi wake Hayati Dkt,John Magufuli.
Walisema kutokana na Rais kutimiza ahadi na kujenga miradi inayogusa jamii,wabunge wengi na madiwani nchini walioshindwa kutimiza ahadi zao kwa wananchi wamekuwa wakidandia miradi iliyotekelezwa na Rais wakijisema wao ndiyo wameitekeleza hali ya kuwa wao hakuna walichokifanya.
‘’Ndugu mwanahabari,ubunge ni taasisi,Mbunge anaweza kutafuta fedha kwa wahisani kujenga miradi ama kutatua changamoto jimboni mwake,pia kupitia mshahara wa Milioni 18 anazopokea anaweza kujenga japo visima 5 vijijini akitumia sehemu ya mshahara wake na si kusubiri fedha za serikali pekee’’walisema



Comments
Post a Comment